jaykiwele
JF-Expert Member
- May 22, 2013
- 552
- 414
Kwa mara ya kwanza namsikia nilipatwa na hisia kwamba huenda alitaka kufurahisha hadhira kama sio kuchangamsha ambalo lilikuwa serious mnoo kujadili hoja za msingi ila baada ya kumsikia tena katika mkutano wa wafanyabiashara ulifanyika hapo jana akiongea na waandishi wa habari akisisitiza serikali iangalie vizuri kilimo cha bangi kwa mara ya kwanza nilishtuka na kupata wasiwasi kama ni kweli watu walipanga mstari kumpigia kura huyu ambaye inadhihirisha wazi ni mtumiaji kama sio mfanyabiashara haramu wa hizi bangi ambazo zimethibitishwa kitaalam kuwa na madhara kwa binadamu hasa kusababisha magonjwa ya akili. Kweli wakat watu wanajadili imekuwaje nchi ya Vietnam ambayo miaka ya zamani ilithibitika kuja kuchukua samaki na korosho pamoja na kujifunza kubangua korosho Tanzania imefanikiwa kuendelea na kupiga hatua kubwa kwenye ufugaji wa samaki na kilimo cha korosho je sisi tulikosea wap na tujifunze nini? Wewe uliyechaguliwa na wananchi unaongelea kilimo cha bangi na mirungi kiukweli mtanisamahe ila kwa hili nimewadharau sana kama huyu ndo anawawakilisha na mkapigia kura kiukweli mmepeleka jiwe sio mwakilishi..........