utaifakwanza
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 14,193
- 2,812
Ni live kutoka ukumbi wa mikutano wa Diamond jijini DSM, wanaongea kwa uchungu mno. fuatilia LIVE kupitia TBC1 NA HAPA JF KATIKA UZI HUU
=======
Anaeongea kwa sasa ni mgeni Rasmi, mzee Butiku na anasema hata wakati wa mwalimu madini yalianza kuchimbwa. Mwalimu aliamua kusitisha kwa maelezo kwamba wasubiri vijana wasome kwanza.
Butiku: Miaka ya hivi karibuni migodi yote imefufuliwa, mashaka hayajaanza na Rais Magufuli. Yalianza na Mwalimu, mashaka haya yapo pia kwa nchi nyingine kama DRC, kwamba hatupati stahili yetu, si hiyo tu hata mashaka ya mafuta. Rais Museveni hakuruhusiwa kuyasafisha pale, yalitakiwa kuyasafirishwa nje na kazi wapate huko.
Baada ya majadiliano wakamruhusu kuyasafisha kiasi. Mwalimu alisema zuia bwana, wenzake wakasema chimbeni bwana.
Wa sasa akasema zuieni kwanza, akaunda kamati. Aliekabidhiwa mamlaka ya kulinda haki za wananchi ni Rais, sio mimi hata ningekuwa waziri, kazi yake ni kumshauri tu. Tume ikafanya kazi kisha ikaleta matokeo.
Wajibu wetu ni kumuunga mkono, hawezi akaenda peke yake, tumemtambulisha kwa maadui wengi. Amefanya hii kazi, jambo la pili ni kutangaza matokeo haya. Tulishawahi kuwa na tume ya jaji Bomani, nani anajua matokeo yake?
Wakati anatoa ile ripoti alisema tupo katika vita, pamoja na kusoma na kujenga vyuo vikuu. Hatujaweza kuwa na teknolojia ya kutosha, hivi miaka 55 hatuwezi kujenga mtambo wa kuchambua mchanga wa madini? Hiyo nayo tumeshindwa? Mbona mzee alisema ngoja wasome?
Msomi mmoja tumepata, Rais Magufuli. Katika hili la kutangaza tumshukuru, hata katika ngoma huwa kuna anaeianzisha. Tunacheza ngoma ya dhahabu kwa sababu Rais ametusaidia kutuambia kuna tatizo hilo na mie nimefanya hivi, ujasiri huo lazima tuupongeze.
Kumetokea ubishi, wataalam wetu wanasema madini ambayo tumewekeana mkataba, ambacho tumeambiwa ndicho kilichomo ni kidogo. Nimesikia watu wa Acacia wanasema tumesema ni kweli yote, kuna kaubishi kadogo hapo. Lakini ukiwasikiliza watu wa Acacia kwa makini wanasuasua, wanasema hawana hakika, wanakubali.
Vita hii ya uchumi, sisi ndio yumeanzisha vita hiyo. Rais wetu ndio ametusaidia kuingia katika mazungumzo haya. Tumsikilize, tujipange, tusiogope.
Katika kujua uvunguni kwangu kuna akiba gani, hilo tunajua. Hawa wana utaalamu mkubwa sana na wamefanya kazi katika nchi nyingi, hilo tunawapongeza maana ni binadamu wenzetu na wametuzidi lakini tuwaambie Rais wetu ni Rais wa wawekezaji wote.
Rais wa Tanzania ni Rais wa Acacia, anawapa ulinzi. Na kama ni Rais wao, akitoa kauli hadharani, cha kwanza kabisa ni kuiheshimu na atapotoa kauli kashawaambia wananchi, ametoa nafasi ya mhadhara kwa hio tunazungumza ndio maana tupo hapa leo.
Mazungumzo baada ya habari yanaweza kuwepo tukishakubaliana msingi huo, sisi wote ni watu, tuheshimiane, nawaomba hata hao Acacia wamuheshimu Rais wetu.
Tunataka wanaosema sema waache kusema tu, watoe ushahidi.