figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mara kwa kosa la kusafirisha magunia 15 ya mirungi.
Watu Wawili wanashikiriwa na jeshi la polisi,Butia maMkoani Mara. Wadakwa Wakisafirisha kilo 500 za Mirungi kwa Kutumia Gari Dogo
Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Ramadhani Ng'anzi ame sema watuhumiwa hao wamekamatwa katika kijiji cha Muryaza Wilayani Butiama. Kamanda amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Elias Charles na Briston Ngaga wakazi wa Nyegezi Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza.
Aidha watuhumiwa hao wamekamatwa na askari wa doria wakiwa na gari ndogo Toyota Carina yenye namba T 784 DFB ikiwa na mirungi hiyo gunia 15.
Hata hivyo, aliwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kusaidia kuwakamata watu wanaokiuka sheria na taratibu za nchi.
Baadhi ya wakazi wa mjini hapa wamesema udhibiti wa dawa za kulevya ni jukumu la kila Mtanzania kwa sababu madhara yake husababisha athari katika jamii inayozunguka eneo husika.