Busu la Kikwere.....

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493
Jana jioni nikiwa na kazi muhimu umeme umenisumbua sana ile kukatika katika mara kadhaa kwenye majira ya jioni ilikuwa ni kero kubwa. Ilinifanya nikumbuke shida yote hii ilianzia kwenye Richmond. Iwapo ile tume iliyoongozwa kwa Mbwembwe na Dr Mwakyembe na Makamu wake Stella Manyanya ingefanya kazi yake na kuweka ukweli hadharani basi tusingefika kuingia kwenye hizi shida za umeme wa mgao kwa taifa hili lenye zaidi ya miaka 50 ya uhuru ifikiapo Dec 9 mwaka huu.

Mwakyembe na Stella Manyanya kwa sababu zao, kuna taarifa hawakuweka wazi, shida ya umeme imeendelea kuwepo mpaka sasa, nafasi zao zina wasuta hawakuwatendea haki watanzania wenzao kwa kutumia kodi yetu. Sawa Mzee wa Monduli aliachia ngazi kwa kustaafu kutokana na ajali ya kisiasa.

Lakini bado tuna shida ya umeme na jamaa hawa Dowans na Symbion wamezaliwa. Hii ni kutokana na kukosekana kwa uzalendo wa ile kamati kuficha baadhi ya taarifa muhimu kwa taifa. Matokeo ya hawa jamaa kumpa shavu Mh wa Msonga naye amewapa mabusu Mwakyembe kwa kazi ya kinafiki ni naibu waziri wa miundo mbinu na ujenzi na busu la Stella Manyanya eti Eng ni Ukuu wa mkoa wa Rukwa lol! Kwa kazi nzuri ya kuficha ukweli kwenye serikali ya kisanii.

Tabia ya kusema kile wasichoakiamini mioyoni mwao, bali kufurahisha wasikilizaji hiki ndicho kinachomsumbua Mh Mwakyembe ooohh nataka uawawa! Mnafiki huyu, Mimi nimewekewa sumu, ooohhh mimi kwangu ni muongo anatafuta faraja ya moyo wake kwa kutulaghai watanzania kwa kuficha kwake taarifa muhimu za uchunguzi wa Richmond

Binafasi sina msamaha na ile kamati

Tanzania haitakiwi iwe gizani, leo hii thamani ya shs yetu inashuka, inflation inakaribia kuzidi ile ya Zimbabwe, kumbukeni hao jamaa hawana hata mgao wa umeme.

Nina hasira sana na hizi taratibu zetu za kimfumo.

Rev Fr Masa K
 
chama cha magamba wote ni watu wa ovyo sana, hakuna unafuu kwenye magamba... yaani badala ya kusonga tunarudi eti tumethubutu tumeweza. lakini wadanganyika ni wajinga pia... umeme kila siku umeme tumechoka sasa tunataka umeme wa uhakika.
 
Jamaa akiwapa mabusu uwezo wa kufikiri haupo tena! Nnape anafurahia busu kutoka kwenye UDC masasi Hadi uenezi magambani
 
Kaaz kwel kwel! Huo upuuzi na kuficha ficha mambo na kubebana ndiyo umetufikisha kwenye matatizo haya ya sasa na bado tunapalilia matatizo makubwa zaidi ya kimfumo. Tutaanza kurithishana uongozi wa juu wa kisiasa na wa vyama, mwisho wa siku ni kuendelea kufichiana maovu na hali ya watanzania masikini kuendelea kuwa mbaya.
 
Nimekuwa nikiona humu JF wengine wakimsifia Mwakyembe na wengine bila haya wakimpigia chapuo Mamvi 2015, ishu nyengine kwa kweli tunazikriet sisi wenyewe kwa uvivu wetu wa kufikiri na kufanya maamuz sahihi. At least 30% ya watz wangekuwa na utamaduni wa kuzishirikisha akili zao ktk maisha ya kila siku tungekuwa mbali sana.
 
Mtu anayemsifia Mwakyembe ama Yule Mzee wa Urambo samwel Sita nadhani hawana ufahamu na hawa Jamaa ! Membe, lowassa, Mwakyembe na Sita ni msiba kwa taifa
 
Polepole mkuu sasa hivi utaambiwa si great thinker kwa kuwasema hawa akina Mwakyembe,Sitta na wale wapambanaji eti wa ufisadi kumbe ni njaa tu wanayoipigania.Hivi inatakiwa kiwango gani cha elimu ili mtu aelewe kuwa Hawa akina Mwakyembe,Sitta na wenzao mwisho wa sku walitusaliti???walikuwa na kipele wakaambiwa wakipeleke hospitali wakaataa,leo limekuwa jipu tena kubwa wanalalama,issue hii ya umeme wala isingefika hapa tunapolazimika kuilipa dowans na bado umeme sio wa uhakika.Dawa ya tatizo ni kulitibu na sio kujalibu kulitibu kiujanja ujanja kwa maslahi binafsi.Kwangu mimi hawa ni wachumia matumbo tu,bado nchi hii hatujapata watu wenye uchungu na nchi hii,kibaya kinachotughalimu ni kufichiana maovu ndani mfumo huu ulioasisiwa na ccm,Mwakyembe hakutaka kumtaja kiongozi wa nchi eti kwa kuhofia serikali ingeanguka hapa kwa maslahi ya nani???Sitta nae akafanya sarakasi za aina yake pale bungeni kuzima suala la richmondi kuendelea kujadiliwa leo analalama dowans isilipwe,hawa ni wasomi wazuri wana digrii za kueleweka nadhani hapa jf wangekuwa na heshima yao sana,isitoshe ni wanasheria duuuu!!!!!!hapa tukubali tu kuna laana inayotutafuna,kuondokana na hilo maombi ya kuomba na kufunga nchi nzima.
 
Never believe official version in most cases..

And that what happens kwenye hiyo report yao..offical version imeficha reality
 
Viongozi wetu wanapopewa wadhifa hufunga midomo nahoja nzito na zenye manufaa. Kwa taifa zinaisha kweli tuinahitaji kufunga na kuomba.
 
Laana ya watanzania na watoto wetu inawaandama. Mwisho wa siku watakufa kama Gaddafi na watasifiwa kwa hiana. Lakini ukweli unabaki palepale kuwa kichwa cha nazi cha bagamoyo kisipo tafuta kichwa kingine cha kufanana nacho kinakachoficha ukweli nina hakika wengi wa hawa tunaowaona mashujaa wa leo wataishia kuwa mashujaa wa jera kesho.
 
jana jioni nikiwa na kazi muhimu umeme umenisumbua sana ile kukatika katika mara kadhaa kwenye majira ya jioni ilikuwa ni kero kubwa. Ilinifanya nikumbuke shida yote hii ilianzia kwenye richmond. Iwapo ile tume iliyoongozwa kwa mbwembwe na dr mwakyembe na makamu wake stella manyanya ingefanya kazi yake na kuweka ukweli hadharani basi tusingefika kuingia kwenye hizi shida za umeme wa mgao kwa taifa hili lenye zaidi ya miaka 50 ya uhuru ifikiapo dec 9 mwaka huu.

Mwakyembe na stella manyanya kwa sababu zao, kuna taarifa hawakuweka wazi, shida ya umeme imeendelea kuwepo mpaka sasa, nafasi zao zina wasuta hawakuwatendea haki watanzania wenzao kwa kutumia kodi yetu. Sawa mzee wa monduli aliachia ngazi kwa kustaafu kutokana na ajali ya kisiasa.

Lakini bado tuna shida ya umeme na jamaa hawa dowans na symbion wamezaliwa. Hii ni kutokana na kukosekana kwa uzalendo wa ile kamati kuficha baadhi ya taarifa muhimu kwa taifa. Matokeo ya hawa jamaa kumpa shavu mh wa msonga naye amewapa mabusu mwakyembe kwa kazi ya kinafiki ni naibu waziri wa miundo mbinu na ujenzi na busu la stella manyanya eti eng ni ukuu wa mkoa wa rukwa lol! Kwa kazi nzuri ya kuficha ukweli kwenye serikali ya kisanii.

Tabia ya kusema kile wasichoakiamini mioyoni mwao, bali kufurahisha wasikilizaji hiki ndicho kinachomsumbua mh mwakyembe ooohh nataka uawawa! Mnafiki huyu, mimi nimewekewa sumu, ooohhh mimi kwangu ni muongo anatafuta faraja ya moyo wake kwa kutulaghai watanzania kwa kuficha kwake taarifa muhimu za uchunguzi wa richmond

binafasi sina msamaha na ile kamati

tanzania haitakiwi iwe gizani, leo hii thamani ya shs yetu inashuka, inflation inakaribia kuzidi ile ya zimbabwe, kumbukeni hao jamaa hawana hata mgao wa umeme.

Nina hasira sana na hizi taratibu zetu za kimfumo.

Rev fr masa k

sasa ebu tueleze alificha taarifa gani?
 
Back
Top Bottom