Business Plan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Business Plan

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mbogela, Jul 25, 2011.

 1. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Unamahitaji ya mchanganuo wa wa biashara (Business Plan)? Tunatengeneza business plan kwa bei ndogo na inaweza kupatikana katika kipindi cha wiki 2. Business plan zetu zinafuata standard ya UK. Kwa mahitaji wasiliana niPM nikupe contact tukubaliane namna ya kumove forward.
   
 2. CONSULT

  CONSULT JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Nashukuru sana mtaalam, Hii ni professional work ni bora wateja kujua uwezo/elimu na hata uzoefu na mafanikio ya kikazi ili kuwajengea imani naamini kwa namna hiyo utapata wateja wengi humu mm mojawapo.
   
 3. l

  lily JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  asanre sana mkuu, kuna rafiki tangu anakaa nje(UK) ni mtanzania but kaolewa na mbritish, anataka kuja tanzania kufanya business, mme wake ni mjenzi na mama ni manager wa hotel! huku UK, je ushauri mfupi wa business plan, uwezo wa pesa upo
   
 4. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2011
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Asante sana kwa ushauri wako. Ningependa niwasiliane na mteja moja kwa moja juu ya CV yangu na wenzangu ninaoshirikiana nao. Lakini kwa ufupi Mimi mwenyewe nina masters ya Management, Economics and Consumer studies ya Wageningen University and Research Centre, Uholanzi na pia nina BSc. ya Food Science and Technology kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine Morogoro. Nina kozi mbali mbali za management, Business na enterpreneurships. Nimefanya kazi na NGOs (local and International) kama Mratibu na Mkurugenzi nikihusika na kubuni miradi na kuiandikia proposal zake. Pia nimefanya kazi za kujiriwa Tanzania na Botswana. Sasa hivi mimi na wenzanngu tumeamua kufanya kazi za kibiashara zaidi na kupunguza kazi za non for profit and services.

  Mimi mwenyewe nipo full time kwa kazi hizi, nashirikiana na wenzangu wawili wanaonipa msaada part time, wa kwanza ni MBA ya ESAMI (makao makuu yake yapo Arusha chini ya Maastricht school of Business Management ya Uholanzi na mfanyakazi wa kiwanda cha cement. Mwingine ni MBA ya London University na mfanyakazi wa zaidi ya miaka 10 katika board ya kahawa wakisaidia wakulima, wanunuzi, wauzaji, exporters wa kahawa nje na ndani ya nchi. Ana uzoefu mkubwa wa biashara za mazao. Pia tunamtumia one of a friend with BA ya Mzumbe na mhasibu mmoja kutoka TIA.

  Terms. Ukitaka tukuandikie mradi wako, utawajibika kutupa details mbali mbali (jambo linaloweza kufanyika kwa simu na mails) lakini kwanza utajibu maswali 6 ya kwanza ili tuweze kuset na kukubaliana terms and conditions.
  1. Aina ya Biashara unayotaka kuandikiwa Biz-Plan
  2. kama biashara yako ndio inaanzishwa (start up Biz) au ni biashara ambayo ipo tayari? (kwa mfano unataka kupanua)
  3. Biz-Plan itakuwa ya kazi gani? mathalani kuombea mkopo au unataka kuitumia kama tool/guide
  4. Unataka kuanza biashara yako lini?
  5. Mtaji na ukubwa wa biashara yako?
  6. Wajibu wetu baada ya kumaliza kazi ya kukuandikia Bz-Plan (kama tutwajibika kutoa consultancy zingine katika biashara yako)

  Tukisha pata majibu ya maswali hayo pamoja na maswali mengine yanayoweza kujitokeza kama follow up questions tutaweza kujua tutakuwa na workload kias gani. Kwa mfano tutajua kama kazi yako itahitaji kusafiri, kufanya research kama kuwaconsults CHAMBER, TCI, board mbali mbali nk. Tutajua muda inaochukua na pia tutajua out put itakuwa katika ubora gani. (We quarentee ubora unaokubalika at International standards)

  Tukisha kudetermine hayo tutakupa kiwango chetu cha fee ya kufanyia kazi hiyo, Muda wa kuderiver product (bila visingizio vya umeme) kama tutakubalina terms tutasaini mkataba wa kazi. Na fee yetu inalipwa kwa awamu 3.
  Awamu 1. Kabla ya kuanza kwa kazi (kiasi kidogo usually robo ya malipo yote)
  Awamu 2. Baada ya kumaliza First Draft na kupitiwa na mteja na kujiridhisha kuwa tupo in the right direction according to his/her wishes)
  Awamu 3. Baada ya kukabidhi final product.

  Wakati wa mchakato huo tutakuwa na mikutano miwili ya ana kwa ana na mteja (tupo tayari kusafiri kumfuata mtaje alipo)
  1st. Meeting. Kumpa First Draft na kujadiliana juu ya marekebisho muhimu ya kufanywa
  2nd Meeting. Kukabidhi Final Product. (Katika mkutano wetu wa mwisho tunafanya power point presentation na tunamruhusu mteja kualika watu anaopenda washiriki kwenye presentation hiyo, hasa watalaam anaoamini wanaweza kumpa critical advices) Kama kutakuwa na marekebisho ya lazima yatafanywa within 24 hrs na mteja atapewa kazi yake iliyokamilika.

  Final product ni:
  1. Two hard copies (soft bind/or spiral) coloured printed
  2. Soft copy in PDF

  Karibu sana, nitumie maswali kwenye PM au mbogela@yahoo.com
  Napatikana kwa namba 0787410315/0754 247915
   
 5. m

  mjasiria JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 3,790
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu nimeipenda hii. kazeni buti nitawatafuta nitakapowahitaji
   
 6. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimekubaki kwa jinsi ulivyotoa maelezo ya kina. Nashauri uweke na bandiko lingine kwa kiingereza, lenye maelezo ya kina kuhusu operating model yenu.
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Asante ndugu.

  Unatumia kigezo gani kupanga fee?
   
 8. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  mkuu unaonyesha uko fit, weka sample moja tuone!
   
 9. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2011
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Dada WOS Asante sana kwa swali lako. Ndio tumeamua kuwa kibishara zaidi mwaka huu, kabla tulikuwa tunaandika miradi kwa ajili ya NGO na CBO kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa hiyo hatukuwa tunacharge fee yoyote. Sasa baada ya kubadirika kutoka kuwa volunteers na kuanza kurender hii huduma kwa pesa bado hatujaanza kucharge a serious profesional fee. Fee setting Method yetu hutegemea sana aina ya assignment tuliyopewa na mteja. Kutegemeana na assignment ya Mteja huwa tuna vigezo kama tatu hivi za kupanga fee.
  1. Muda unaotumika/per unit time (Mara chache sana tume apply hii njia, huwa mara nyingi inakuwa ni gharama sana)
  2. Lump sum fee - Mteja atatulipa kutokana na kukamilisha kazi yake.
  3. wakati mwingine hata tukikamilisha kazi bado huwa hatulipwi na husubiri kama mteja amepata matokeo aliyokuwa anategemea kutoka katika business plan yetu kwa mfano kama Biz-Plan ilikuwa kwa ajili ya kuombea mkopo basi wakati mwingine huwa tunasubiri mteja apate mkopo ndio atulipe kama hajapata mkopo huo inakula kwetu sote (kwa mtindo huu fee huwa inakuwa ni % ya amount ambayo mtu anatagemea kukopa).

  Lakini kubwa sana huwa tunaangalia workload, kwa nchi za wenzetu data nyingi unaweza kuzipata online, lakini kwetu hapa nitahitaji kuwatemebelea wenye data hiz moja kwa moja, au kuwapigia simu au e-mail, kama mawizara, ushirika, wenye viwanda, tanzania Chamber of commerce kwa hiyo nitahitaji muda mwingi na itanilazimu kuchaji pesa kubwa kidogo. Kama una nia ya kupata Biz-plan usisite kuwasiliana nasi tutakupa terms nzuri, bei zetu sio mbayakwa serious investment.
   
 10. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2011
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mkuu Asante kwa kutuamini, Lakini bahati mbaya sana nasikitika kuwa hatuwezi kuweka sample kwani kazi tulizonazo ni kazi za wateja na tunamakubaliano kuwa baada ya mteja kutupa wazo la biashara hatutalitoa kwa third party bila idhini ya mteja wetu. Samahani sana mkuu hatuwezi kuvunja makubaliano na wateja wetu.
   
 11. Kibirizi

  Kibirizi JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 602
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Vipi mna uzoefu na hizi bussines plan za BDG nataka niwape kazi. Otherwise naona mpo fresh.
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nawapongezni sana kwa mwelekeo huu mzuri.Halafu watu wanasem ati hakuna ajira? Mmeonyesha mfano mzuri sana.
   
 13. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mwana JF Kibirizi, Asante kwa kuona na kutambua uwezo wetu. Nadhani unamaanisha Business Development Gateway (BDG)? Kama unamaanisha hao experience yetu ni ya kiwango kifuatacho, Tumeandika michanganuo mitatu ya watu walioomba mikopo kupitia Juhudi Loan Scheme ya National Microfinance Bank (LTD), Lakini pia kama utatupa kazi tun advantage moja ya kuweka mradi wako katika hali ya kukopesheka vizuri zaidi kwani tunaye rafiki yetu ambaye tunaweza kumuingiza on Board, Huyu rafiki yetu ana BCOm (UDSM, 1990 ) yeye alikuwa mmoja wa Trainers wa Business skills training course iliyokuwa inaenda sambasamba na Juhudi Loans Scheme ya NMB. Training hizi zilikuwa organized na NMB na kuwa facilitated na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF). Mkuu Tupe hiyo kazi nasi tutafanya kila liwezekanalo kkupa desired results.
   
 14. Ngwanakilala

  Ngwanakilala JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Maelezo yenu yameni-impress. Nikija Tanzania kuna kazi ntawapa mnifanyie. mna make sense na mnaonekana mnajua mnachoongelea na mnachokifanya. Asanteni.
   
 15. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2011
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Asante na karibu sana. Lakini pia ingewezekana kutupa kazi ukiwa bado uko safarini (Nje), hii itasaidia pande zote mbili (sisi na wewe) kuwa na muda wa kutosha na kucomplete assignment yetu bila pressure. Na utakapokuwa unarudi itakuwa ni kuangalia kama wazo lako limewekwa kisahihi katika maandishi (kwa kulinganisha na mazingira) ikitokea kuwa hukuridhika na uwasilishaji wetu wa concept yako tutaweza kurudia kuandika upya mradi kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza.

  Pia kwa kuwa upo mbali na nyumbani basi tunaweza pia kukufanyia fessibility study kuhusiana na wazo lako la kibiashara na kukupa ushauri unaofaa. Kama utakuwa na mahitaji ya kusajiri kampuni tutakuandalia Memorandum and Article of association na pia kusaidia kusajiri kampuni yako na
  Business Registration and Licensing Agency (BRELA) kama niu kampuni, Registration, Insolvency and Trusteeship Agency (RITA) kama ni trustee n.k pia kukutafutia lesseni za kibiashara toka mamlaka husika kama TRA n.k na utakuwa tayari na documents zote za kuendesha biashara kabla hujafika nchini.

  Kuna usumbufu mkubwa wa watu ambao wamekuwa wakiishi nje ya nchi, hasa kutokana na utofauti wa culture kutoka maeneo wanayotoka na hapa kwetu. Watu wanaotoka nchi za ulaya na Amerika hata nchi za asia kiasi fulani huwachukua muda kuweza kucope na usumbufu na bureaucracy zetu, pamoja na tips na rushwa na utapeli wa hapa nchini. Kwa hiyo ni hisia yetu kuwa wanahitaji msaada wa kuwezesha kufanikisha shughuri zao hasa miezi ya mwanzo ya re-entry zao.
   
Loading...