Busara itumike ziara za kushitukiza sekta binafsi

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2011
Posts
497
Reaction score
236
Jana katika vyombo vya habari imeripotiwa kwamba mmiliki wa Fore Plan clinik amekimbia kituo chake kutokana na ziara ya Kushitukiza ilivyofanywa na naibu Waziri Dr. Hamis Kigwangala.

Habari hii ya Dr. Mwaka waandishi wameiripoti kishabiki sana. Hakuna aliyemuona Dr. Mwaka akimkimbia naibu Waziri bali ni hisia za naibu Waziri na team yake.

Unapofanya ziara ya kushitukiza kwenye sekta binafsi ni tofauti na serikalini, sekta binafsi nao wanamipango yao. Ningeona logic ya habari ile kama ingebainisha makosa kadhaa waliyoyaona kituoni hapo kwani kituo hakikuondoka na wagonjwa walikuwepo wangeweza kutoa maoni yao kuhusu ubora au uchakavu wa huduma wanazozipata.

Kigwangala kutumia muda mwingi kuzungumzia watu badala ya kuzungumzia masuala ya msingi aliyoyaona katika ziara hiyo ni ujenzi wa Nidhamu ya woga kwa sekta binafsi na kutafuta sifa kupitia kwa waandishi wa habari.

Ni wazi kwamba bila jitihada za Dr. Mwaka kujijenga kihuduma na kujitangaza sana kupitia vyombo vya habari naibu Waziri asingekifahamu kituo hicho mtu anayafanya maovu hawezi kujitangaza hivyo ni muhimu kudhamini jitihada za kila mmoja wetu na kumpongeza anapofanya vizuri au kukosoa kwa staha anapokosea ili kumuwezesha kujenga zaidi.

Ni vema kabla ya kumshambulia na kuchafua haiba za watu na taasisi zao tujiridhishe na udhaifu wao tujulishwe mapungufu yao na utetezi wao dhidi ya mapungufu hayo ili tupate fursa ya kupembua pumba na mchele. Tukumbuke kwamba sifa ya mtu au taasisi inaweza kujengwa kwa miaka mingi lakini ikabomolewa ndani ya dakika chache tu hivyo ni vema tukajiridhisha kabla ya kubomoa watu.

Kwa mwenendo huu wa kuendeshwa na hisia na kujaribu kubomoa sifa aliyojijengea mtu kwa miaka mingi bila HOJA za msingi tutawakatisha tamaa na kuchafua haiba za watanzania wengi walioamua kuthubutu kuwa wajasiriamali hapa nchini.

Na hali hii ndio imepelekea watanzania kukosa Role Models katika biashara kwani watu wamekuwa wakipambana kuwashusha na kuwachafua watu waliofanikiwa hata kama watafanya makosa madogo madogo ya kibinadamu. Tujifunze kurekebushana kwa lengo la kujenga.
 
Umeongea vizuri sana sana tena bila emotions! Mtu anahangaika kivyake kwa jasho na damu yake, leo serikali inataka kumshusha wakati haikumpa msaada wowote alipokuwa anapigana. Ni mbaya sana sana.
 
Nimekua nikibishana na baadhi ya watu wanaofanya judgment subjectively dhidi ya hili suala kwenye mitandao leo,wengi wao wanaendeshwa na mihemko,bila kuangalia uhalisi wa jambo lenyewe,no principle of Natural justice applied to Dr Mwaka concern,siasa inapoingia kwenye mambo kama haya huleta shida sana,naibu Waziri anaongea majestically as if kweli Dr Mwaka alimkimbia,Dr Mwaka ni public figure now,anajulikana mpaka uvungu wa kitanda anacholala,sasa akimbie eti kisa Waziri anakuja?,watanzania huwa tunapenda kutojiongeza hata kidogo!
 
Back
Top Bottom