Php
Member
- Nov 27, 2015
- 46
- 12
BAADA YA KUTOA USHAURI KWA BINTIE, BABA HAKUMUACHA NYUMA KIJANA WAKE WA KIUME ALIMPA BUSARA ZIFUATAZO KATIKA KUTAFUTA MKE
Mwanangu kwa unyenyekevu mkubwa napenda niwe mkweli kwako. Usiweke kipaumbele kuoa mwanamke kwa kuangalia size ya makalio yake au size ya maziwa yake ila jali sana size ya moyo wake na akili yake. Makalio hupukutika, maziwa hushuka lakini akili na busara hukua kila uchwao! Jali sana size ya upendo wake kwako na ustahimilivu. Kwasababu baada ya miaka mitano au kumi haitakuwa tena habari ya makalio au maziwa.
Kama unavomuona mama yako, sasa hivi kifua chake kipo flat, na makalio yako tambalale lakini bado tunaishi pamoja. Bado nampenda sana na yeye ananipenda sana. Nadhani umeshaziona picha zake enzi akiwa kijana jinsi alivyokuwa amejaliwa kwa kila kitu. Hivyo mwanangu zingatia hilo.
Mwanangu kuwa makini sana na mwanamke anaependa pesa. Namaanisha mwanamke ambae yeye kila muda anaongelea kubadilisha mitindo ya nywele, kucha, handbags, make-ups na viatu. Maisha ya ndoa si kwa ajili ya hivyo vitu. Bila hvyo vitu ndoa yenye afya inaweza ikasimama ila bila ya mapenzi na ustahimilivu ndoa itakuwa kichekesho na ni ndoano.
Nilipomuoa mama yako, sikuwa na gari wala nyumba. Hata sikuwa nimesoma. Lakini nilikuwa na ndoto za kufanikiwa na mama yako aliishi katika ndoto zangu na kunisupport. Ndio maana unaona haya mafanikio tuliyonayo mpaka leo. Mwanamke yeyote ambae hatoi support katika ndoto zako hafai kama ukoma. Kuna wanawake wataona ndoto na malengo yako ni mazuri kuzidi yao. Utakua na bahati kama ukimpata mmojawapo.
My Son, fungua masikio yako vizuri, kuna aina ya Wanawake unaotakiwa kuwaepuka. Usifanye makosa ukaoa aina hiyo ya mwanamke. Utajuta!! Namaanisha mwanamke ambaye yeye siku zote ni kuwasemea watu mabaya hata wafanye lipi. Ukikutana na mwanamke wa namna hii kimbia mbio na usitazame nyuma tena! Huo ni ukoma!
Kijana wangu, moja ya aina mbaya ya mwanamke utakaeoa ni yule ambae haishi kulalamika kwa kila kitu unachofanya. Kama ukinunua hiki yeye anasema ungenunua kile, kama ukifanya hiki yeye anasema ungefanya hivi. Tafadhali sana kaa nae mbali mwanamke wa namna hiyo.
Najua wanawake wengi wanapenda kuongea, kwani ndivyo jinsi walivyoumbwa na mwenyezi Mungu lakini yule anae ongea kwa masaa mawili na kusikiliza kwa dakika mbili huyo ni bomu. Muda wowote linaweza likalipuka. Kuwa na busara na hekima na kuwa mwangalifu na wale wanaojifanyisha (pretenders). Mwanamke pretender ni vigumu mno kumgundua.
Yeye atajua kila kitu, huwa anakuwa mwangalifu sana. Katika hili mwanangu funga macho na fungua moyo wako! Na utamuona tu kama anajifanyisha.
Hakuna mtu aliyekamilika, kama utamwona mwanamke anae amini ndoto zako, anae kuheshimu, ambae amejikita vilivyo katika mahusiano yenu na ambae sio mbinafsi huyo usimwache aende zake.
Lakini kumbuka usikurupuke! Nimekufunza vilivyo tokea ukiwa mdogo! Kama utapata mwanamke mzuri lakini wewe binafsi una tabia zilizo mbaya kabisa. Hautakuwa na ndoa yenye afya hata kidogo. Endelea kuwa kijana mzuri hata pale utakapoanzisha familia yako. Katika hilo najua hutaniangusha!
Mwanangu usiwe kama yule bwana ambae nimepata kumsikia kupitia mwanamuziki wa muziki wenu wa kizazi kipya aitwae sijui Nikki wa namba mbili, kibao kinaitwa Baba Swalehe.
Sitakuchagulia mke, ila nimekupa ushauri wa aina ya mwanamke utakaetaka kumuoa. Kama utampata, basi mlete nyumbani kwa ajili ya baraka zetu.
Kila ka kheri my son.
from somewhere