Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Serikali ya Burundi inatarajia kuiburuza mahakamani Rwanda kwa madai ya kuwaunga mkono waasi na kusababisha mauaji ya raia wake wasiokuwa na hatia kutokana na machafuko yanayoendelea kutokea nchini humo.
Akizungumza na Shirika la DW la Ujerumani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Alain-Aime Nyamitwe amesema kila nchi ina haki ya kwenda mahakamani iwapo itaona uhuru wake unakiukwa.
Amesema Burundi ina ushahidi unaoonyesha kuwa Rwanda imekiuka uhuru na utu wa raia wake na hivyo lazima wawaburuze mahakamani.
Katika taarifa ambayo shirika la habari la Ufaransa AFP liliipata hapo jana, mkuu wa chama cha CNDD-FDD amesema awali Kagame alifanya jaribio la mauwaji ya kimbari katika maabara na katika maandiko yake hayo rais wa CNDD-FDD Pascal Nyabenda amesema maabara ya mauwaji ya halaiki yapo Rwanda mpaka sasa na bado rais Kagame amekuwa na majaribio huko na kutaka kuyaingiza Burundi akifanya ubeberu mdogo.
Source: DW