Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Umoja wa mataifa umeonesha kushtushwa na video iliyoonesha kikundi cha vijana cha Chama Tawala cha Burundi CNDD-FDD wakiimba kuwa "wanawake wa upinzani wapewe ujauzito au wauawe"
Video hiyo ilionesha vijana kama 100 wa kikundi cha "Imbonerakure" wakiwa ktk mkutano huko Ntega, province ya Kirundo na wakawa wakipiga kelele " Wanawake wa upinzani wapewe ujauzito ili wajifungue Imbonerakure"
Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa mataifa(OHCHR) Zeid Ra'ad Al Hussein imeelezea kuwa tukio hilo linatia wasiwasi.
" Kelele zile za vijana wale zinatia wasiwasi hasa kwa sababu zinaonesha ukweli wa kile tulichokisikia kutoka kwa wale waliokimbia Burundi kuhusu kampeni ya kutandaza hofu inayofanywa na kikundi hicho"
OHCHR imekubali kuwa Chama hiko Tawala kimekemea maneno hayo na kuongeza kuwa kuna ripoti inaonesha ushiriki wa Maofisa wakubwa wa Serikali katika vitendo vinavyoendana na hivyo. Zeid aliongeza kuwa kukemea tu haitoshi bali wanatakiwa waweke 'stop' kwa vitendo hivyo.
Video hiyo pia inaonesha kikundi kingine kikipiga kelele mara 19 kuwa wapinzani " wanatakiwa wafe"
Umoja wa mataifa wanakadiria kuwa zaidi ya 400,000 wamekimbia Burundi ktk miaka 2 iliyopita wakihofia usalama wao.
Video hiyo: