Ninachokiona ni summary executions kwa hawa waliokamatwa lakini in no time, inafuatia assassination ya watu wakuu wanaosimamia uvunjwaji wa makubaliano unaolalamikiwa.
Nkurunzinza amekuwa akiifool dunia kwamba anagombea tena muhula wa tatu kwa kuwa mihula miwili iliyopita, alisimikwa na Parliament lakini kikubwa ni kwamba anagombea kwa sababu wananchi wa Burundi wanamtaka/wanamshawishi agombee ili aendelee kuwaongoza.
Baada ya vurugu kutokea, public ikiwa imegawanyika na watu wanaandamana mitaani kupinga kinachothibitisha ni uwongo wa kushawishiwa na umma, inakuwa vigumu, hao wanaomshawishi aendelee muhula wa tatu ni wapi? Warundi wamekataa!.
Sasa hivi, dunia ina development agenda kubwa moja ya kupunguza na kutokuzalisha wakimbizi wapya. Nkurunzinza, no matter amejishawishi au amejifungia ofisini na wapambe akaamua kuwadharau warundi wote akaamua kuwaburuza kwa lazima watake wasitake atawatawala, anapoona anazalisha maelfu ya wakimbizi tena wakiwa ni wasomi na nguvu kazi ya taifa, inaleta sintofahamu, anachoking'ang'ania kwa gharama kubwa hivyo kina maslahi ya nani hasa? Na atajustify namna gani kwamba utawala wake ni halali hata akubalike na jumuiya ya kimataifa kama si kusababisha vikwazo na mateso zaidi kwa raia atakakobaki nao?
Katika hali ya kawaida, ukishaona raia wamegawanyika, na jeshi likagawanyika kuwasupport raia, na wengine wachache wakatumia mtutu kuwanyamazisha wanaokupinga, inahitaji kuwa na shida kwenye moyo na nafsi ili usimame kwa ujasiri na kusema kwa mbwembwe watu wawe na amani kwa kuwa umerudi kwenye kiti.
INATAKIWA NKURUNZINZA AFAHAMU KWAMBA UWEPO WAKE KWENYE KITI NDIO UNAOSABABISHA MACHAFUKO NA MIGAWANYIKO HIYO. KAMA KWELI YUKO HAPO KWA MASLAHI YA WARUNDI, NA ALIDANGANYWA KWAMBA WATU WANAMPENDA NA WALIMSHAWISHI AONGEZE MUDA WA KUTAWALA, SASA AFAHAMU AMESHAURIWA KIJINGA.
ANATAKIWA HAO WASHAURI WAKE AWAWEKE KANDO MARA MOJA NA ATEUE WENGINE WENYE MRENGO SAHIHI.
ATANGAZE MSAMAHA KWA WAASI WOTE WALIOKAMATWA NA WANAOTAFUTWA KWA UHALIFU UTOKANAO NA VURUGU NA UASI WA JESHI.
AWAOMBE MSAMAHA WARUNDI WOTE KWA KUAMUA VIBAYA KUTOKANA NA USHAURI MBAYA ALIOPEWA NA SIJUI KAMA WATAMSAMEHE HASA WALIOPOTEZA NDUGU ZAO.
AWASIHI WAKIMBIZI WOTE ALIOTENGENEZA WARUDI MARA MOJA BURUNDI ILI KUJENGA NCHI.
ATANGAZE KUONDOA JINA LAKE KWENYE UGOMBEA WA URAISI AMBAO NDIO CHIMBUKO LA UHARIBUFU.
ATANGAZE MCHKAKATO MPYA NASAHIHI WA UCHAGUZI BILA YEYE KUWEMO ILI ASIMAMIE HAKI BILA TAMAA.
Vingineyvo, anamaliza vibaya sana na anatengeneza Burundi yenye resentments kitu ambacho hakijawahi kutengeneza amani zaidi ya unafiki na kuumizana kwa visasi.
It is just a beginning,unakiuka peace agreement & so what next,huyu jamaa raia hawamtaki sijui nn kitatokea huko mbeleni.