Burudi yatishia kuwaondoa wanajeshi wake Somalia

Burudi yatishia kuwaondoa wanajeshi wake Somalia

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,273
Reaction score
25,303
_92245041_46282e67-b60e-4002-a568-432422c8952e.jpg


Serikali ya Burundi imetishia kuondoa askari wake wa kulinda amani nchini Somalia katika kikosi cha Umoja wa Afrika AMISOM iwapo umoja wa ulaya, mfadhili mkuu wa kikosi hicho, hauto rejelea uamuzi wake wa kutopitisha mishahara ya askari hao mikononi mwa serikali.

Burundi ina wanajeshi zaidi ya elfu tano mia tano nchini Somalia, ikiwa kwenye nafasi ya pili baada ya Uganda , kwa nchi zilizo tuma vikosi vya kulinda amani katika nchi hiyo iliopo upembezoni mwa Afrika.

Waziri wa ulinzi Emmanuel Ntahomvukiye aliliambia bunge kuwa wanajeshi hawajapata mishahara yao ya kila mwezi ya dola 800 kutoka kwa muungano wa ulya kwa muda wa miezi kumi.

Burundi ndiyo nchi ya pili inayochangia wanajeshi wengi zaidi katika kikosi cha AU kinachopigana na al-Shabab nchini Somalia.


Chanzo: BBC
 
Wanataka ipite kwao ili wapitishe mapanga shaa kabla ya kuwalipa.
 
Serikali za Afrika ni shida kabisa.
 
Back
Top Bottom