Burudani za mtaani zilizopotea

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Back in the days, miaka ya 80 na 90 mtaani kulikuwa kuna noga sana kwa burudani mbalimbali tulizokuwa tunazipata kama vile kuona:

1. Ngongoti
2. Joyce Wowowo
3. Kibisa kucheza na Nyoka
4. Mazingaombwe
5. Power akivuta vitu mbalimbali
6. Video za Kibatali (mwanasesere)
7. Magari ya Bati na Udongo
8. Magari ya Cinema
9. Kuwinda Ndege
10. Kuogelea
11. Upinzani wa Mpira timu za mtaani

Mimi kwetu Kwa MTONI Kwa Aziz, timu zetu za kitaa zilikuwa nyingi sana, kama vile:

1. Small Tiger
2. Chama Mneli
3. Double Seven
4. Parma
5. Panama
6. Farudume
7. Banyamulenge
Na zinginezo. Tukumbushane kwa wenyeji wa huko.

Kwa upande wa misimu ya matunda, dah, ilikuwa inanoga sana. Ni kuning'inia tu juu ya miti, maana kipindi kile kila nyumba ilikuwa na mti wa matunda ya kipekee, na ilikuwa wakati wa watu kuvaa ma P.O.P. Matunda kama vile:

1. Zambarau
2. Maembe
3. Stafeli
4. Topetope
5. Fenesi
6. Mabibo
7. Makungu
8. Bungo
9. Peasi
10. Komamamga
11. Shelisheli

Hivi vitu vilileta burudani na hamasa kitaa kipindi kile, sijui vimepotelea wapi. Hivi mkoa gani hizi burudani bado zipo mpaka leo?

Je, tukio gani unalikumbuka wakati mko kwenye harakati za makuzi kuusiana na vitu nilivyovitaja hapo juu?
 
Ngongoti walikua wanafaa magongo miguuni na kua warefu,walikua wakiambatana na mzee Jangala kwenye burudani zake za maigizo.
 
Miaka hiyo watot wa 2000 hawawez elewa,. Mabanda ya sinema za Lufufu
Kutoroka shule
Kuchimba udongo wa mfinyanzi
Mchezo wa goroli
Karata za viberiti
Nk
 
kukodisha baiskeli 🤣
na kuvua na kufuga samaki
-double kisoda
-tambara
-kinyuzi
 
Back in the days miaka ya 80 na 90 mtaani kulikuwa kuna noga Sana Kwa burudani mbalimbali tulizokuwa tunazipata kama vile kuona
1.Ngongoti
2.Joyce wowo
3.kibisa kucheza na Nyoka
4.mazingaombwe
5.power akivuta vitu mbalimbali
6.video za kibatali(mwanasesere)
7.magari ya Bati na udongo
8.magari ya cinema
9.kuwinda ndege
10.kuogelea
11.upinzani wa Mpira timu za mtaani
Mimi kwetu Kwa MTONI Kwa aziz timu zetu za kitaa zilikuwa nyingi Sana yaani kama vile
1.small Tiger
2.chama mneli
3.double seven
4.parma
5.panama
6.farudume
7.banyamulenge
Na zinginezo tukumbushane Kwa wenyeji wa huko
Kwa upande wa misimu ya matunda dah ilikuwa inanoga Sana ni kuning'inia Tu juu ya miti maana kipindi kile kila nyumba INA mti wa matunda ya kipekee na ilikuwa Wakati wa watu kuvaa ma p.o.p,
Matunda kama vile
1.zambarau
2.maembe
3.stafeli
4.topetope
5.fenesi
6.mabibo
7.makungu
8.bungo
9.peasi
10.komamamga
11.shelisheli


Hivi vitu vilileta burudani na hamasa kitaa kipindi kile siju vimepotelea wapi
Hivi mkoa gani hizi burudani bado zipo mpaka Leo?
Je tukio gani unalikumbuka Wakati mko kwenye harakati za makuzi kuusiana na vitu nilivyovitaja hapo juu
Umesahau mdundiko na vanga siku ya kumtoa mwali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom