Burkina Faso: Wanajeshi 12 wauawa katika shambulio dhidi ya Wapiganaji wanaodhaniwa kuwa Magaidi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
"Makundi ya magaidi" yaliojihami kwa bunduki yameshambulia vikosi vya jeshi la Burkina Faso na kuua baadhi ya askari na wengine wengi kujeruhiwa, kwa mujibu wa byanzo kadhaa vya usalama nchini humo.

Shambulio hilo lilitokea mapema Jumatatu asubuhi, Kaskazini mwa nchi.

Uongozi wa jeshi la Burkina Faso umeandika kwenye taarifa kwamba kambi ya jeshi ya Koutougou katika Mkoa wa Soum imelengwa kwa "shambulio kubwa" na "makundi ya kigaidi yaliyojihami kwa bunduki".

Watu waliojihami kwa bunduki ambao walikuwa kwenye pikipiki na magari walifika kwenye eneo la mpakani na Mali, kulingana na chanzo cha usalama.

Shambulio hili, kwa uhakika, limeua askari wasiozidi kumi na mbili kulingana na taarifa iliyotolewa na uongozi wa jeshi. Lakini vyanzo kadhaa vya usalama vinaeleza kwamba askari ishirini ndio waliuawa katika shambulio hilo. Wanajeshi kadhaa pia wamejeruhiwa na wengine wengi wamekosekana. Vifaa vya jeshi vilichomwa moto na silaha kadhaa zilibebwa na washambuliaji.

Kwa mujibu wa uongozi wa vikosi vya jeshi vya Burkina Faso, operesheni kubwa ya jeshi iliendeshwa kujibu shambulio hilo. Washambuliaji wengi waliouawa na wengine wengi kukamatwa, taarifa ya jeshi imeeleza.

Kwa kuelezea mshikamano wake na vikosi vya ulinzi na usalama, serikali ya Burkina Faso, kupitia msemaji wake, imethibitisha azimio lake la kuhakikisha usalama wa watu na mali unapatikana kote nchini.
 
hiyo nchi ina waislam 70%+...ila tangu uhuru hapajawahi kuwa na rais muislam..wataipata fresh
 
Kama hawajaenda shule bado itakuwa ngumu kuongoza. Rais lazima awe ana Elimu na siyo Ilimu. Elimu ipo madarasani na Ilimu ipo Madrasa. Wataendelea kuua kwa sababubya wivu na siyo vinginevyo
wana ujinga kama wako..na wataendelea kuumia,elimu imetoholewa kwenye ilmu,ni neno la kiarabu,unaamini hakuna waislam walioelimika bukinafaso!?..funzo la mjinga ni tabu
 
hiyo nchi ina waislam 70%+...ila tangu uhuru hapajawahi kuwa na rais muislam..wataipata fresh
Senegal nayo 90% ni waislamu lkn tangu uhuru 1960 wameongozwa na marais wakristo kwa miaka mingi zaidi.

Kufikiria kuwa dini fulani wakiwa wengi basi ni wao ndio sharti wawe uongozini ni wazo mfu linaloweza kutolewa na mpumbavu tu, hivyo basi Senegal na Burkina Faso wana bahati kutokuwa na hao wapumbavu.
 
Senegal nayo 90% ni waislamu lkn tangu uhuru 1960 wameongozwa na marais wakristo kwa miaka mingi zaidi.

Kufikiria kuwa dini fulani wakiwa wengi basi ni wao ndio sharti wawe uongozini ni wazo mfu linaloweza kutolewa na mpumbavu tu, hivyo basi Senegal na Burkina Faso wana bahati kutokuwa na hao wapumbavu.
unaongea ujinga,hayo ndiyo ya watutsi na wahutu,nadhani matokeo yake unayajua..sasa subiri hao burkinafaso waulambe upumbavu
 
Back
Top Bottom