Buriani: Watanzania Wengi Hawakumjua Rais Mkapa. Nami Nishuhudie

Kwa hiyo unaposema Jose Morinho ni kocha mzuri ina maana na yeye huwa anaingia uwanjani kucheza? Think critically bwana acheni kutuchosha bila sababu. Kwanza tu kuwachagua hao mawaziri katika serikali yake inaonyesha alikuwa yupo makini.
 
Mkuu, huyu bwana kaandika vizuri sana. Kitu kimoja tu alichokosea ni kwenye exchange rate aliyoikuta Mkapa na aliyoikuta Mwinyi.

Ndugu yangu, sijui kwa nini unaamini kuwa nimekosea kwenye exchange rate. Tazama na hii kumbukumbu ya BOT, labda utaamini kuwa nilichokiandika ni sahihi. Wengi hawajui, wanadhani shilingi ilikuwa dhaifu kukaribia udhaifu uliopo sasa. Kabla ya mwaka 1985, shilingi ilikuwa na nguvu sana.
1967-2002​
1967-1985​
1986-2002​
1986-1992​
1992-2002
Official exchange rate (Tsh/US$1)​
231.2​
8.99​
479.7​
173.8​
693.8​
Source: Computed from annual data from Bank of Tanzania, National Bureau of Statistics.

In ‘Exchange rate regimes and inflation in Tanzania By Longinus Rutasitara, Department of Economics, University of Dar es Salaam – Tanzania, page 8.

Angalia wastani wa exchange rate kati ya 1967 -1985.
 
What I can remember correctly exchange rate ilikuwa kwenye 800 wakati Mkapa anatoka madarakani kwa kuwa nilikuwa na change physically. By Mwinyi anaondoka ilikuwa 1 to around 500 Tshs. Mkapa ameiacha kwenye 800.
 
Mkapa alikuwa mashine sio mchezo. Reforms za kiserikali alizoanzisha au kuzisimamia zitafaidisha wana wa nchi hii vizazi kwa vizazi vingi vijavyo.
Rest In Peace, a true Africanist.
 
ule mdahalo ulifanya mrema aonekane kituko bila vile alikua anachukua nchi mrema ha ha ha ha ha ha wananchi wakafunguka akili kuwa wanataka kumpa nchi kishoka
 
Tunashukuru kwa kututoa tongotongo, lakini ingependeza masuala haya mngeyasema wakati wa uhai wake.
wakati watu wakimshambulia na kumtuhumu mambo mbalimbali pasipo kuujua ukweli,
Watu wangeelewa na ingekua njia nzuri sana ya kumsafisha.
haya yanayoandikwa na kusemwa sasa hayaoni Wala hayasikii pengine ameondoka na sononeko kwa watanzania wengi kutotambua mchango wake mkubwa aliofanya kwa nchi.
Tuwape sifa zao mapema wakiondoka wawe na amani nafsini mwao.
 
What I can remember correctly exchange rate ilikuwa kwenye 800 wakati Mkapa anatoka madarakani kwa kuwa nilikuwa na change physically. By Mwinyi anaondoka ilikuwa 1 to around 500 Tshs. Mkapa ameiacha kwenye 800.
Upo sahihi. Mwaka 1982 ndipo shilingi ilianza kupoteza thamani. Wakati huo Serikali ilikuwa imefix exchange rate kwenye $1=sh5. Kisa cha mabasi ya mzunguko Dar kuitwa daladala (doladola), na sh 5 ile yenye kona kuitwa dalla (dollar) ni kwa sababu ilikuwa sawa na dola 1. Na noti ya sh 20 ilikuwa ikiitwa paundi kwa sababu sh 20 ilikuwa sawa na £1.

Baada ya Mwalimu kuridhia masharti ya IMF ndipo shilingi ilianza kupukutika kwa kasi. Ilitoka kuwa sawa na sh 5, ikaenda sawa na sh 20, ikaenda ikawa sawa na sh 60, kisha 90, hatimaye ikafika 390. Ndio wakati Mwinyi alipoingia madarakani. Hapo ndipo kidogo ikawa inaendelea kupoteza thamani angalao siyo kwa spidi ya mwanzo. Ilifika dola 1 sawa na sh 700, kisha ikashuka mpaka sh 500. Kisha ilipanda kwa kasi tena. Mwinyi akaondoka dola 1 ikiwa sawa na sh 1,200.

Mahali nilipkosea ni kufikiria Mwinyi alichukua uongozi mwaka 1980.

Usahihi ni kuwa shilingi ilianza kupoteza thamani kipindi cha mwisho cha Mwalimu, Mtei akiwa Waziri wa fedha. Mwinyi aliichukua nchi mwaka 1985, dola 1 ikiwa sawa na sh 390. Akaipeleka mpaka ikafikia dola 1 sawa na sh 1,200. Mkapa alipoingia shilingi ilianza kupanda thamani mpaka kuifanya dola 1 kuwa sawa na sh 800.

Nashukuru kwa kunifanya nirudi kupekua kumbukumbu zangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi. Nahisi hatukumtendea haki Mzee huyo. Ni wakati sahihi sasa kuyanena yaliyo mema kwa hawa wastaafu wetu walio hai ili wajue na wajisikie fahari kuona tunathamini michango yao kwa Taifa letu.

Binafsi najisikia vibaya sana, hasa kwenye awamu hii, wanavyotaka kuonesha Rais Kikwete hakuganya la maana zaidi ya Serikali yake kuendekeza ufisadi. Nina hakika Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa sana. Na mengi mabaya yanayosemwa dhidi yake kwa kiasi kikubwa yanatengenezwa.

Kuna siku tutayaweka yote makubwa ambayo ameyafanya na tutayaenzi. Ayafahamu akiwa hai kuliko kumsifia mtu wakati hayupo.

Kuwasema vibaya hawa wastaafu wakiwa hai halafu kuwasifu sana wakiwa hawapo Duniani, ni unafiki wa hali ya juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tawire.
 
Mkapa nilipenda zile hotuba zake vibaya yaani anafanya tathmini ya mambo yote yaliyofanyika mwezi mzima na anatoa majawabu yote kuanzia malalamiko ya kila wizara halafu anatoa mwongozo wa namna tutakavyokuwa kwa mwezi mwingine.
 
Mkapa nilipenda zile hotuba zake vibaya yaani anafanya tathmini ya mambo yote yaliyofanyika mwezi mzima na anatoa majawabu yote kuanzia malalamiko ya kila wizara halafu anatoa mwongozo wa namna tutakavyokuwa kwa mwezi mwingine.
Na alikuwa consistent, kama kuna mwezi aliacha basi ilikuwa dharura.
 
double R uzalendo wangu wa nchi uliiisha baada ya kuingia kikwete,halafu magufuli nimeichukia hii nchi ,watu ambao wamezaliwa 1995 ,2000,2005 pia wako humu Jf hawataweza kulinganisha yupi alikuwa na ukweli na yupi alikuwa mwongo hadi sasa kwa umri wangu nimegundua unaweza ukawa na PHD lakini kichwani hamna kitu Mkapa alinifanya nikimbie haraka kwenye safari zangu niwahi kwenda kumsikiliza aisee Raha ya milele umpe eebwana na mwanga wa milele umwangazie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…