kijana mwenye jinsia mbili alipata shida ya kibofu cha mkojo na kufanyiwa surgery
Lakini hali yake haikutengamaa bali ndio ikazidi kuwa mbaya sana sana .
Sasa jana kanitumia meseji watsap.
Kaka asante kwa kuwa rafiki bora zaidi ya rafiki , ndugu zaidi ya ndugu
Nilifurahia sana kampani yako kwenye maisha yangu kwa muda tuliofahamiana . Ulinipa tabasamu na kidogo kupata mwanga wa kuishi bila kujutia nilivyoumbika na pia kupata faraja na matumaini makubwa kiroho . Japo kuwa ulinifanya nipende kuishi
Ila kwa sasa sina jinsi naondoka ninahuzuni . ila nikikumbuka tumaini la maisha ya uzima wa milele ulilonihubiria basi sina sababu ya kuhuzunika sana nimeshateseka sana na nikiwaza dunia isiyokubali nilivyoumbwa acha tu nipumzike kaka acha nipumzike . Kwaheri bro tutaonana kwenye uzima wa milele jitahidi uishi maisha uliyonihubiria tukutane huko siku moja.
Asante sana bro .
Hayo ndio maneno ya mwisho ya rafiki yangu kijana mwenye jinsia mbili.
Nilipiga simu haikupokelewa leo napigiwa simu naambiwa kijana hatunae tena , sijaweza kumuuliza hata yeye ni nani ila nisauti ya mwanamke mtu mzima alikuwa analia sana.
Nina huzuni sana , nitamisi sana meseji zake na ukaribu wake na mimi utani wa kutosha
Hakuna siku iliyopita bila kuongea na kuchat
R.i.p
View attachment 2574372