Buriani Pendo, Buriani mpenzi yangu

Buriani Pendo, Buriani mpenzi yangu

Ulale salama Pendo,Mashauri wako akulilia
Umelala na wako upendo,Ni ngumu kuvumilia
Hakika umemaliza mwendo,mwenzio haachi kulia
Hakika atakalo Mola,binadamu hawezi zuia

Mpendwa Kaka mfiwa,jikaze wako mtima
Namjua wako ukiwa,kupoteza wake uzima,
Kuonana majaliwa,kumuombea simama
Hakika atakalo Mola,binadamu hawezi zuia

R.I.P .
Naulazimisha mtima, uikubali hatima,
Mikono nikiachama , isilishikize tama ,
Japo chozi aandama , ujasiri najipima
Niseme si langu fungu , haujakubali mtima
 
Ni juzi tulikuwako, kwa karamu yakufana
Ikiwa bathdei yako, Da! Pati ya kuagana
Ukanita Niko ,Niko, Ati hatuta achana
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Siamini umeenda, hatutaonana tena
Yote tuliyoyatenda, hayatarudia tena
Popote tulipo kwenda, hatuwezi fika tena
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Siamini hutofika, kawaida kusalimu
Kwa utani tukicheka, Dah! Hilo tabasamu
Malengo yakipangika, mbeleni ndoa muhimu
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Ukapanga lake jina, la mtoto tukijaliwa
Kwa wakike Rihanna, wa kiume majaliwa
Ni mipango mingi sana, tulopanga maridhawa
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Umeniacha na kidonda, kutwa kucha ninakonda
Giza nene limetanda, moyo wangu ulipenda
Pendo leo umeenda, Najua sio kwa kupenda
Ni seme si langu fungu, haujakubali mtima

Moyo wajawa uchungu, hauijui hatima
Kwaheri', Mapenzi yangu, yamebakia yatima
Nisamehe sana Mungu, nizitoapo lawama
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Ukaandika wosia, nifikie mazikoni
Eti niache kulia, siwezi huo mtihani
We ukiniandikia, pendo ulilia nini?
Mama yote kanitonya, kweli tulipendana

Nenda salama pendo, sisahau abadani
Ulinifunza upendo, uliozidi uzani
Umeacha pengo, pendo, Mpaka nije kwa manani
Kwaheri' mpenzi, Tutaonana baadae

Pole sana Mungu Wa mbinguni ampe pumziko la milele pendo wako
 
Pole sana mkuu...! Apumzike kwa amani Bi Pendo.
 
Kuna sehemu umeona uasherati? Je kuwa wapenzi ni kufanya ngono , ni lugha sawa na alikuwa mchumba wangu tukiwa kabisa kwenye hatua ya kuingia kwenye ndoa, saratani ikakatisha safari yetu
Sijui nikwambieje mkuu? Mimi bado napata maruweruwe tu, saratani ni shetani kamili, eti Leo nimebaki kama yatima!!

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo Pendo amekufa akiwa katika status ya "uasherati".

Maana yake, kutokana na maelezo yako mwenyewe, wewe na marehemu mlikuwa hamjafunga ndoa, ila mlikuwa mnafanya "uasherati".

Kumbuka imeandikwa, "wazinzi na waasherati hawatauona Ufalme wa MUNGU kamwe".

Hakuna ajuaye siku ya kufa, hivyo basi ni vema sana kila aliye hai sasa hivi akajitahidi sana kuishi maisha ya usafi.

Usiogope kufa, bali, ogopa sana kufa ukiwa na DHAMBI!!!!!

Mwenye masikio na asikie.
Acha uboya wa kujihesabia haki, kwani ndoa ndio tiketi ya kwenda huko peponi unakokuamini wewe?
 
Pole mkuu saratani ni janga lingine la kutisha duniani. Siku hz unakuta vijana wtt wanakufa kwa hili jinamizi. Jipe moyo
 
Pole mkuu saratani ni janga lingine la kutisha duniani. Siku hz unakuta vijana wtt wanakufa kwa hili jinamizi. Jipe moyo
Unakufa ukijijua utakufa , nilijitahidi kumtia moyo lakini wapi aliamini mda umeisha , siku mbili tu naondoka kutoka karibu na kwao anaandika wosia , na anaaga dunia
 
Ulale salama Pendo,Mashauri wako akulilia
Umelala na wako upendo,Ni ngumu kuvumilia
Hakika umemaliza mwendo,mwenzio haachi kulia
Hakika atakalo Mola,binadamu hawezi zuia

Mpendwa Kaka mfiwa,jikaze wako mtima
Namjua wako ukiwa,kupoteza wake uzima,
Kuonana majaliwa,kumuombea simama
Hakika atakalo Mola,binadamu hawezi zuia

R.I.P .
Dah mko vzr kwenye mashahiri umelipatia haswa
 
Kumanyooko kifo kwann hutoi taarifa pendo angejiandaa akatwambia tumdai nani mwenye Deni

Kifo ooh kifo huna huruma nimeenda kununua mboga narudi kifo umemchukua pendo wangu

Kifooo huna huruma twambie mapema nasi tuage
 
Nawaza sijui Pendo alikuwepo pale ziwa Victoria au ni kifo kingine tu?......
Ila pole sana mkuu Mashaurijr
 
Ur mourning or you are writing a poem?

If ur mourning let wish ur soulmate Rest in Peace and if ur writing a poem you a good upcoming poet
Sasa wewe mwenzio anaandkika kiswaz wewe una muandikia kidhungu mtaelewana kwel
 
Back
Top Bottom