Buriani Pendo, Buriani mpenzi yangu

Buriani Pendo, Buriani mpenzi yangu

KING ASSENGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2016
Posts
929
Reaction score
1,494
Ni juzi tulikuwako, kwa karamu yakufana
Ikiwa bathdei yako, Da! Pati ya kuagana
Ukanita Niko, niko, Ati hatuta achana
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Siamini umeenda, hatutaonana tena
Yote tuliyoyatenda, hayatarudia tena
Popote tulipo kwenda, hatuwezi fika tena
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Siamini hutofika, kawaida kusalimu
Kwa utani tukicheka, Dah! Hilo tabasamu
Malengo yakipangika, mbeleni ndoa muhimu
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Ukapanga lake jina, la mtoto tukijaliwa
Kwa wakike Rihanna, wa kiume majaliwa
Ni mipango mingi sana, tulopanga maridhawa
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Umeniacha na kidonda, kutwa kucha ninakonda
Giza nene limetanda, moyo wangu ulipenda
Pendo leo umeenda, Najua sio kwa kupenda
Ni seme si langu fungu, haujakubali mtima

Moyo wajawa uchungu, hauijui hatima
Kwaheri', Mapenzi yangu, yamebakia yatima
Nisamehe sana Mungu, nizitoapo lawama
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Ukaandika wosia, nifikie mazikoni
Eti niache kulia, siwezi huo mtihani
We ukiniandikia, pendo ulilia nini?
Mama yote kanitonya, kweli tulipendana

Nenda salama pendo, sisahau abadani
Ulinifunza upendo, uliozidi uzani
Umeacha pengo, pendo, Mpaka nije kwa manani
Kwaheri' mpenzi, Tutaonana baadae
 
Kwa hiyo Pendo amekufa akiwa katika status ya "uasherati".

Maana yake, kutokana na maelezo yako mwenyewe, wewe na marehemu mlikuwa hamjafunga ndoa, ila mlikuwa mnafanya "uasherati".

Kumbuka imeandikwa, "wazinzi na waasherati hawatauona Ufalme wa MUNGU kamwe".

Hakuna ajuaye siku ya kufa, hivyo basi ni vema sana kila aliye hai sasa hivi akajitahidi sana kuishi maisha ya usafi.

Usiogope kufa, bali, ogopa sana kufa ukiwa na DHAMBI!!!!!

Mwenye masikio na asikie.
 
Kuna sehemu umeona uasherati? Je kuwa wapenzi ni kufanya ngono , ni lugha sawa na alikuwa mchumba wangu tukiwa kabisa kwenye hatua ya kuingia kwenye ndoa, saratani ikakatisha safari yetu
 
Kwa hiyo Pendo amekufa akiwa katika status ya "uasherati".

Maana yake, kutokana na maelezo yako mwenyewe, wewe na marehemu mlikuwa hamjafunga ndoa, ila mlikuwa mnafanya "uasherati"...
Usihukumu usije ukahumiwa. Mpaka Pendo anaaga dunia hukuwa nae.... Swala la dhambi au mema ni lake na Mungu wake..... Sote hatuna ukamilifu mbele za Mungu
 
Ulale salama Pendo, mwenzio akulilia,
Tungo zilojaa nondo, nyuma umemuachia,
Dhahiri kwa huu mwendo, machungu yamemjaa,
Mkafurahi pamoja, mbinguni mkutanapo.
 
Ulale salama Pendo,Mashauri wako akulilia
Umelala na wako upendo,Ni ngumu kuvumilia
Hakika umemaliza mwendo,mwenzio haachi kulia
Hakika atakalo Mola,binadamu hawezi zuia

Mpendwa Kaka mfiwa,jikaze wako mtima
Namjua wako ukiwa,kupoteza wake uzima,
Kuonana majaliwa,kumuombea simama
Hakika atakalo Mola,binadamu hawezi zuia

R.I.P .
 
Ni juzi tulikuwako, kwa karamu yakufana
Ikiwa bathdei yako, Da! Pati ya kuagana
Ukanita Niko ,Niko, Ati hatuta achana
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Siamini umeenda, hatutaonana tena
Yote tuliyoyatenda, hayatarudia tena
Popote tulipo kwenda, hatuwezi fika tena
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Siamini hutofika, kawaida kusalimu
Kwa utani tukicheka, Dah! Hilo tabasamu
Malengo yakipangika, mbeleni ndoa muhimu
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Ukapanga lake jina, la mtoto tukijaliwa
Kwa wakike Rihanna, wa kiume majaliwa
Ni mipango mingi sana, tulopanga maridhawa
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Umeniacha na kidonda, kutwa kucha ninakonda
Giza nene limetanda, moyo wangu ulipenda
Pendo leo umeenda, Najua sio kwa kupenda
Ni seme si langu fungu, haujakubali mtima

Moyo wajawa uchungu, hauijui hatima
Kwaheri', Mapenzi yangu, yamebakia yatima
Nisamehe sana Mungu, nizitoapo lawama
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima

Ukaandika wosia, nifikie mazikoni
Eti niache kulia, siwezi huo mtihani
We ukiniandikia, pendo ulilia nini?
Mama yote kanitonya, kweli tulipendana

Nenda salama pendo, sisahau abadani
Ulinifunza upendo, uliozidi uzani
Umeacha pengo, pendo, Mpaka nije kwa manani
Kwaheri' mpenzi, Tutaonana baadae
Ni shairi ?? Au
 
Shairi zuri sana hili, umelikatia copyright lakini?
 
Back
Top Bottom