Buriani engadget distro!

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159

​
Mwezi Septemba mwaka 2010 iPad ya kwanza kabisa ilitangazwa na hayati Steve Jobs, huu likuwa ndio mwanzo wa tableti za kisasa, Jobs alitaja mambo matano ambayo yatafanyika kwenye tableti kwa ufanisi mkubwa, miongoni mwa mambo matano hayo ni usomaji wa vitabu na majarida ya elektroniki (e-books na e-magazines) kwa kutumia vifaa hivyo vyenye skrini yenye ukubwa mithili ya kitabu.


Ni kweli kwamba ni rahisi kusoma kitabu kwenye tableti kuliko simu, hii ni kutokana na ukweli kwamba skrini ya simu ni ndogo mno kwa usomaji wa kitabu kamili. Pia ni kweli kwamba ni rahisi kusoma kusoma kitabu kwenye tableti kuliko laptop kwa vile laptop si rahisi kuibeba katika mazingira fulani, unapokuwa safarini kwa mfano kwenye basi au treni, au unapokuwa kitandani tayari kwa kulala.


Pia ubora wa magazeti hayo ni ule uwezo wake wa kuwa na video, audio na pia tasiwra na zinazozunguka ambazo unaweza kuziona kwa nyuzi 360, yaani pande zote za taswira husika, hii hufanya usomaji wa majarida haya kuwa ni kiburudisho cha aina yake.


Lakini kinachoshangaza ni kwamba majarida yameanza kufeli katika soko la tableti, miezi kadhaa iliyopita jarida ambalo lilikuwa ni kivutio kikubwa hasa kwa wanateknolojia, jarida la Tech liifungwa, wiki iliyopita Jarida maarufu kuliko yote katika soko hili kwa upande wa washabiki wa gajeti nalo ni Engadget Distro nalo limefungwa. Baada ya kuchapisha majarida 106 kwenye iPad kuanzia msimu wa kiangazi mwaka 2011 hadi Ijumaa iliyopita. Ni wapi biashara hii imekwenda kombo hadi kufikia hatua hii?



Mhairiri mkuu wa Engadget Distro Christopher Trout ameeleza kwa masikitiko makubwa katika makala unayozungumzia ufungaji wa jarida hilo kwamba “Ni huzuni kubwa kwa mhariri kuzima taa ya uchapishaji wa jarida, lakini kwa bahati mbaya leo ni ya pili ambapo nalazimika kufanya hivyo” Akielezea sababu ya kuanguka kwa Distro, ameeleza kuwa “kuhamia kutoka kwenye blogi kwenda kwenye jarida ilikuwa ni kurudi nyuma kihatua”


Hata hivyo utitiri wa majarida hasa kwenye iPad ndio sababu ya kuanguka kwa baadhi ya vigogo katika biashara hii, takwimu zinaonyesha mwaka 2011 katika mwezi wa Julai wakati Distro inaingia mitamboni kulikuwa na majarida 562 hadi kufikia mwisho mwa mwaka jana idadi ya majarida kwenye iPad ilifikia 1,871.


Ingawa teknolojia ya kuchapisha jarida si kubwa au yenye kugharimu, kazi ya uendeshaji wa jarida inagharama kubwa hasa yale majarida yanayotoa habaria kutoka kwenye vyanzo halisi (primary sources) ambapo wanatakiwa kuwa na waandishi kwenye matukio mbali mbali Ulimwenguni na pia kuwa na nyenzo zao ya kufanyia uandishi, pia huwa ni wenye kununua kajeti mbali mbali ili kuweza kuzifanyia uchambuzi halisi.


​
Hivyo jarida kama Distro ambalo lilikuwa linatolewa bure huku likitegemea kuingiza mapato kupitia matangazo ya biashara limeshindwa kuwa na kipato cha kutosha kuweza kurudisha gharama na kuingiza faida. Sababu ya msingi ni kwamba kwa nini wenye biashara wapeleke matangazo yao kwenye Distro wakati kwenye blogi kuna wasomaji wengi, wasomaji wa Distro ni wamiliki wa iPad tu ambao ni washabiki wa teknolojia na gajeti.


Sisi katika Gajetek tuna huzuni kubwa kwa kuondoka kwa Distro kwa vile lilikuwa ni burudani kubwa kwetu, hata hivyo soko hili bado lina muelekeo wa mafanikio, huu ni mwanzo wa kufeli kwa majarida mengi kisha wachache watakaoweza kubaki wataweza kuendelea na biashara hii, tukizingatia kuwa watumiaji wa tableti wanaongezeka kila leo, itafikia wakati tofauti ya idadi ya wasomaji haitakuwa kubwa baina ya blogi na e-magazine. Kama ulikuwa msomaji wa Distro unaweza kuhamia jaribu bora kuliko Distro nalo ni T3, ingawa hili ni la kulipia. Itakubidi utoe ndururu kidogo ili kuweza kusoma T3.




CHANZO: gajetek habari​

​
 
Reactions: HT
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…