Utawala usiojali ELIMU haufai kupewa ridhaa ya kuongoza. Elimu ndiyo chanzo cha uthabiti wa Taifa kwa kujenga rasilimali watu watakao weza kulisimamia Taifa na kuzitumia rasilimali zake kwa uwiano mzuri wenye manufaa kwa Taifa. Kosa hili halitaweza kuvumilika. Tumeshuhudia walimu wakinyanyaswa na kunyimwa stahiki zao, tumekuwa tukilalamika kuwa elimu yetu inashuka mwaka hadi mwaka huku watawala wakilazimisha waliofeli kufaulu na kuendelea na ngazi za juu za elimu. Jinsi viongozi wa bunge kutoka chama tawala wanavyotetea uzembe huu, inatufanya tuamini kuwa mtaji wa CCM ni katika kudhoofisha elimu. Yapo mengi yameniumiza, ila hili limeniumiza na kunitisha zaidi.