Bungeni Dodoma: Wabunge wataka Bunge liahirishwe ili wajadili mafuriko yaliyoikumba nchi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Wabunge wametaka shughuli za Bunge za leo ziliahirishwe ili wabunge wajadili tatizo la mafuriko liloyakumba maeneo mbalimbali nchini ambayo yameacha watu bila makazi na kusababisha vifo.

Wabunge hao walisimama na kuomba miongozo hiyo leo asubuhi muda mfupi baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni.

Walioomba miongozo ni Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani, James Mbatia (NCCR Mageuzi) na Rashid Shangazi (Mlalo-CCM).

Ngonyani maarufu kama Majimarefu ametumia kanuni ya 68(7) alisema kuwa kuna matatizo makubwa ya mafuriko nchini.

“Haswa kwenye mkoa wangu wa Tanga, kumekuwa na maafa, leo hii tunavyoongea kuna watu 1000 hawana chakula, mahali pakuishi na hawana msaada wowote lakini itawasaidiaje hawa watu wakati kamati za afya zikiendelea na utaratibu,”amesema.

Amesema watu wanaadhirika na wanaweza kufa wakati wote.

Shangazi amesema anasimama kwa kanuni 47 (1) akitaka shughuli za Bunge ziahirishwe ili wabunge wajadili kuhuau mafuriko hayo.

“Sasa hivi katika mkoa wa Tanga kuna mafuriko makubwa sana. Na jana yametokea maporomoko katika milima ya usambara, eneo la barabara Lushoto- Arusha- Mombo, Pangani kwenda Tanga, Mombo kwenda Lushoto na Kilindi kwenda Morogoro shoto zilifungwa,”amesema Shangazi.

Chanzo:
Mwananchi
 
Hata tetemeko la kagera miongozo ilikuwepo. Serikali haileti mafuriko waathirika wahame maeneo husika chapeni kazi acheni maneno. Naota tu majibu ya awali.
 
Kweli kiswahili kigumu!.

Mi naona kama hapo ni kwamba wanataka shughuli za kibunge zilizopo kwenye ratiba ndio ziahirishwe ili mijadala ihamie kwenye hilo swala la mafuriko. Na siyo Bunge liahirishwe!
 
Wajadili mafuriko?, kwani yameletwa na Serikali ya ccm, mkuu waambie wachape kazi, nasema tena wachape kaziiiii in koromije sound
 
Ni busara wawakilishi wa wananchi kuonyesha kuguswa na maafa yanayowakumba wananchi. Wafanye hivyo itawapa faraja waliowachagua
 
Ni jambo jema ila wajadili Wao, likifika kwa baba hakuna msaada.
1. Mafuriko hayajaletwa na serikali
2. Njaa, haijaletwa na serikali
3. Tetemeko, hali kadhalika
4. Labda, wanaweza kufikiriwa.
Eeh Mungu tunusuru Watanzania.
 
Wabunge wametaka shughuli za Bunge za leo ziliahirishwe ili wabunge wajadili tatizo la mafuriko liloyakumba maeneo mbalimbali nchini ambayo yameacha watu bila makazi na kusababisha vifo.

Wabunge hao walisimama na kuomba miongozo hiyo leo asubuhi muda mfupi baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni.

Walioomba miongozo ni Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani, James Mbatia (NCCR Mageuzi) na Rashid Shangazi (Mlalo-CCM).

Ngonyani maarufu kama Majimarefu ametumia kanuni ya 68(7) alisema kuwa kuna matatizo makubwa ya mafuriko nchini.

“Haswa kwenye mkoa wangu wa Tanga, kumekuwa na maafa, leo hii tunavyoongea kuna watu 1000 hawana chakula, mahali pakuishi na hawana msaada wowote lakini itawasaidiaje hawa watu wakati kamati za afya zikiendelea na utaratibu,”amesema.

Amesema watu wanaadhirika na wanaweza kufa wakati wote.

Shangazi amesema anasimama kwa kanuni 47 (1) akitaka shughuli za Bunge ziahirishwe ili wabunge wajadili kuhuau mafuriko hayo.

“Sasa hivi katika mkoa wa Tanga kuna mafuriko makubwa sana. Na jana yametokea maporomoko katika milima ya usambara, eneo la barabara Lushoto- Arusha- Mombo, Pangani kwenda Tanga, Mombo kwenda Lushoto na Kilindi kwenda Morogoro shoto zilifungwa,”amesema Shangazi.

Chanzo:
Mwananchi
Wanafiki Tu, mbona hawakuwahi kujadiri tetemeko?
 
Back
Top Bottom