Bunge Senegal kufutwa kuokoa maisha

Tungaraza Jr

Senior Member
Feb 3, 2012
196
48
[h=1]Bunge Senegal kufutwa kuokoa maisha[/h]
120814122729_dakar_floods2009_304x171_afp_nocredit.jpg
Mafuriko Senegal


Rais wa Senegal, Macky Sall ametoa wito wa kufutiliwa mbali bunge la Senate, huku pesa ambazo hutumika kulipia shughuli za bunge hilo zikitumika kwa msaada wa chakula.
Rais huyo alikatiza ziara yake nchini Afrika Kusini kuweza kushughulikia mafuriko makubwa yanayokumba nchi hiyo na ambayo yamesababisha vifo vya watu 13.


Akiongea akiwa katika uwanja wa ndege wa Dakar rais Macky Sall, alisema kuwa ataweza kuwasilisha mswaada wa dharura bungeni ili kufutilia mbali bunge la Senate.
Pesa ambazo hutengewa shughuli za bunge hilo, ambazo ni takriban dola milioni 15, zitaweza kutumika kuzuia mafuriko zaidi katika siku za usoni.
Ingawa maeneo ya nyanda za chini nchini Dakar hukumbwa na mafuriko kila msimu wa mvua, mwaka huu athari zimekuwa kubwa kwa sababu ya mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo mengi ya Afrika Magharibi. .
Inakisiwa maelfu ya watu wameachwa bila makao.
Hapo awali, wananchi walifanya maandamano kutuhumu serikali kwa kukosa kuchukua hatua mwafaka kukabiliana vilivyo na hali hiyo ya mafuriko ingawa walitawanywa na gesi ya kutoa machozi.
Rais Sall alielezea umuhimu wa bunge la Senate katika mfumo wa demokrasia lakini akasema kuwa afueni ya watu wanaoathirika kutokana kwa mafuriko hayo ni muhimu kuliko bunge hilo.
Mwezi Mei mwaka huu, benki ya dunia iliahidi kutoa dola milioni 55.6 kuweza kuimarisha miundo mbinu itakayowezesha nchi hiyo kukabiliana na mafuriko.
Nchi hiyo imekuwa mfano mzuri wa nchi yenye demokrasia barani afrika ikiwa na mfumo mzuri wa siasa za vyama vingi na mfumo wa majimbo.


BBC Swahili - Habari - Bunge Senegal kufutwa kuokoa maisha
 
sijajua nini response ya wabunge hao wa senate but ingekuwa tanzania kuna watu wangezimia au kufa kabisa hasa MAGAMBA ie anna killer ngo, sophia simba, lyatonga mrema,etc
 
Nadhani bunge lao lina chemba mbili kama lile la Uingereza. Nahisi anataka kuua chemba moja mabayo haitokani na uwakilishi wa moja kwa moja kama ilivyo House of Lords ya Uingereza.
 
Angalau ameonyesha uzalendo kwa kuahirisha sarafi yake hiyo ili kujumuika na wananchi wake.....huku kwetu Tanzania kukiwa na janga lolote Rais ndio anajisikia kusafiri zaidi yaani hata kama hana hiyo ratiba.....akisikia meli imezama tu yeye huyooooooo Jamaica kujifunza kilimo cha mihogo!
 
Natamani huyu 'nanga' wetu angekuwa na hata chembe ya uzalendo kama huyu sall...
 
Back
Top Bottom