Bunge na Mahakama Imara ni nguzo za taifa lolote

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,428
13,936
Hata kama taifa litakumbwa na bahati mbaya ya kumpata Rais asiyeeleweka kama Trump, lakini kama nchi ina bunge na mahakama huru na imara madhara ya kiongozi huyo yatakuwa madogo sana. Tuzidi kuomba ili bunge letu na mahakama zetu ziendelee kuwa huru na imara wakati wote bila kujali ni mwanasiasa gani na waaina gani yuko madarakani. Mwanga tumeanza kuuona
 
Mkono wa mtawala umefika kila mahala. Tuombe Uhuru utawale.
Tuombe tuwe na katiba inayoendeleza uhuru wa bunge na mahakama, maana hatujui taifa litapata viongozi wa aina gani huko mbeleni. Tunaweza kuja kulia watu wote bila kujali chama, dini au kabila. Katiba iliyoko sasa inamruhusu mtawala kumchagua mkewe kuwa Waziri Mkuu, mkwe wake kuwa waziri wa fedha, mtoto wake kuwa mkuu wa majeshi, hawala yake kuwa gavana wa benki kuu na rafiki yake kuwa jaji mkuu bila kuhojiwa sana
 
Back
Top Bottom