Bunge liombe radhi


Hapa una mengi lakini ukiisoma KATIBA ya Tanzania kwa uzuri sana imeeleza Bayana kuwa MBUNGE anawakilisha Chama na sio Mpigakura. Sasa kwa mantiki hii ndio maana wanawakilisha mawazo au matakwa ya vyama vyao na sio matakwa ya waliowapigia kura yaani wananchi.

Ndio maana tunasisitiza sana kupata katiba mpya ili mamo kama hayo yaondolewe na MBUNGE awe pale kutetea wapiga kura wake na sio chama chake.
 
Mimi nilishangaa ule mkutano wa kwanza/? mbunge wa ccm mtera alitishia kuwa watapigana bungeni! Na spika, vyombo vya habari nk havikupaza sauti kupinga kauli za hivyo. Huwa najiuliza mbunge wa upinzani angetoa kauli ya vile si tungesikia kile kibwagizo cha uvunjifu wa amani hadi tukome. Matokeo yake jana tena imetoka kauli ya aina ile!! Baadhi ya wananchi wa kanda ya ziwa tumeamua kuwa ccm wakianzisha fujo hizo bungeni, sisi tutawatandika wabunge wao huku mitaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…