Elections 2010 Bunge letu!

Mutekanga

Member
Aug 26, 2007
34
3
Leo Bajeti ya Ofisi ya Rais, imepita! Hata hivyo ilikuwa wazi kwamba ingepita. Ni kupoteza fedha za walipakodi kujadili "Ndiyo". Mnyika,Lisu na wengine wamejitahidi kuondoa Shilingi, kwa hoja nzito ambazo ni za kulisaidia Taifa letu, lakini Wabunge wa CCM ni wengi na kazi yao ni kuimba "Ndiyo". Inavyoelekea hata Hoja ya kuruhusu madawa ya kulevya ikiletwa Bungeni, itapitishwa! Wabunge wetu vijana wa CHADEMA na wale NCCR, wasikate tamaa. Historia inaandikwa na vizazi vijavyo vitaona nani alikuwa mkweli na ni nani alikuwa akitekeleza ya tumbo lake. Bunge letu ni la chama Kimoja, na haliwezi kuleta maendeleo kwa kushangilia "Ndiyo" hata kama ni kuliangamiza taifa. Tafakari!
 
lisu&mnyika live longer tuko pamoja, sikujutia usingizi wangu nilipokua nasubiria matokeo ya mnyika pale loyola
 
Mnyika, Lissu na wenzao wasikate tamaa. Shooting bado inaendelea, DVD zitasambazwa kila kona 2015. Kila mtu atavuna alichopanda, waache waendelee kusifiana.
 
Hii inaonyesha ni kiasi gani wabunge wa CCM walivyo mamluki. CCM's motto now is: "act on interest, to hell with principles". Wameelekezwa kwenye simina zao elekezi kuwa hoja yeyote wapinzani watakayotoa bungeni hata ikiwa nzuri kiasi gani kwa taifa letu, zomeeni na piga meza kwa kwenda mbele! Poor Tanzanians, we have dug our own grave by putting them in power. The brighter side is that we have a chance of reversing the situation. Let us help Chadema with their good cause on all fronts and come 2015 we will definitely get rid of the mamlukis and build our beautiful Tanzania to prosperity. Ambaye hapandi hilo naye atakuwa ni mamluki! Oh cherished democracy, we miss you!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom