Bunge lazishauri serikali kuhusu suala la mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge lazishauri serikali kuhusu suala la mafuta

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Jul 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, imeishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kulifanyia kazi suala la mafuta kuwa la Muungano ama la ili kulitolea maelezo endelevu yatakayodumisha Muungano.

  Mwenyekiti wa Kamati hiyo, William Shelukindo, aliyasema hayo bungeni wakati akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu bajeti ya Wizara ya Nishati ya Madini kwa mwaka 2010/2011.

  "Kuhusu suala la mafuta kuwa la Muungano au la, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilifanyie kazi kwa pamoja na kulitolea maelezo endelevu yatakayodumisha Muungano," alisema Shellukindo, ambaye ni Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga.

  Hoja ya mafuta kuwa ya Muungano ama la imekuwa ikizuka mara kwa mara bungeni.

  Hivi karibuni, hoja hiyo iliibuliwa na Mbunge wa Dimani (CCM), Hafidh Ali Tahir, ambaye alihoji serikali inatoa majibu gani juu ya mafuta na gesi asilia kuwa ya Muungano ama la.

  Pia alihoji serikali inatoa tamko gani juu ya maneno makali na kashfa yaliyotumiwa na baadhi ya viongozi wa Muungano wakati wa kupitisha muswada huo ndani ya Baraza la Wawakilishi.

  Aidha, alihoji nini kifanyike ili matakwa ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wananchi wa Tanzania Zanzibar yaweze kufanikiwa.

  Wakati akiuliza swali hilo, Tahir alisema ingawa Bunge liliridhia kuwa mafuta ya petroli na gesi asilia kuwa ya Muungano kikatiba pindi yatakapogundulika katika ardhi ya Tanzania, Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika moja ya vikao vyake lilipitisha muswada na kuutangazia umma juu ya kukubaliana mafuta ya petroli kutokuwa katika orodha ya mambo ya Muungano.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Muhammed Seif Khatib, alisema serikali haina taarifa za baadhi ya viongozi wa Muungano kutoa maneno makali na ya kashfa wakati wa kuupitisha muswaada wa mafuta ya petroli ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

  Aidha, alisema mafuta na petroli yaliingizwa katika orodha ya mambo ya Muungano mwaka 1968 katika kikao cha Bunge na lilipigiwa kura na wabunge wa pande mbili zote za Muungano.

  Alisema serikali inalitambua suala hilo ni la Muungano hadi litakapoamuliwa vinginevyo.

  Akizungumzia kuhusiana na nini kifanyike kuliondoa jambo hilo katika mambo ya Muungano, Waziri Khatib alisema kwa kuwa Muungano ni ubia wa hiari, linalotakiwa kufanyika ni Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuiandikia Serikali ya Muungano rasmi kuonyesha dhamira ya kuliondoa jambo hilo katika orodha ya mambo ya Muungano.

  Alisema Serikali ya Muungano ikiafiki, itabidi jambo hilo lipelekwe bungeni ili wabunge watoe baraka zao kwa kura kwa mujibu wa taratibu na kwamba endapo theluthi mbili ya pande zote za wabunge watakubali, suala hilo litaondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano.


  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...