Bunge Latibuka Kwa Homa ya Uchaguzi, LITAKUWA LA WIKI TANO, KUVUNJWA JULAI 16 !

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Ramadhan Semtawa

UCHAGUZI mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, umegusa ratiba ya shughuli za Bunge, baada ya mkutano wake wa bajeti unaoanza kesho mjini Dodoma, kutarajiwa kufanyika kwa wiki tano badala ya miezi mitatu kama ilivyozoeleka.Habari za kuaminika zilizopatikana mwishoni mwa juma lililopita kutoka ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam ,zilisema Bunge litavunjwa Julai 16, ili kupisha maandalizi ya uchaguzi huo.

Spika wa Bunge Samuel Sitta, jana alithibitisha habari hizo na kwamba ratiba hiyo imezingatia kwa kina, mchakato wa uchaguzi mkuu na namna ya kupata serikali mpya.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa Bunge, kutokana na ratiba ya mchakato wa uchaguzi mkuu, lazima mkutano huo wa Bunge uwe mfupi tofauti na miaka ya nyuma.

"Ndiyo, Bunge litavunjwa Julai 16 kwa sababu lengo ni kuendana na ratiba ya mchakato wa kupata wagombea na kisha majina yao yapelekwe Nec (Tume ya Taifa ya Uchaguzi)," alifafanua.

"Hatuwezi kutumia muda mwingi kwa mijadala mirefu wakati tutahitaji utekelezaji wa bajeti kwa kupata serikali mpya...kwasababu mawaziri watapaswa kupatikana ili waweze kusimamia na kutekeleza bajeti ya serikali," alisisitiza.

Kwa kawaida Bunge la bajeti linafanyika kwa kipindi cha kati ya miezi miwili hadi mitatu, kuanzia Juni.


Kwa habari zaidi soma MWANANCHI.
 
Naona mambo mengi yanabadilika nchini, vyuo vinafungwa hadi Novemba, bunge ndiyiohilo. Kuna kitu watanzania.... tuwe tayari kwa mabadiliko makubwa nchini. Nahisi yapo! Panapofuka moshi....... mimi siyo sheik.. y lakini na....
 
Naona mambo mengi yanabadilika nchini, vyuo vinafungwa hadi Novemba, bunge ndiyiohilo. Kuna kitu watanzania.... tuwe tayari kwa mabadiliko makubwa nchini. Nahisi yapo! Panapofuka moshi....... mimi siyo sheik.. y lakini na....
Inaonekana hali ya kifedha sio shwari!
 
Back
Top Bottom