ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 620
- 1,543
Magazeti ya Mwananchi na The Citizen yamefanya kazi nzuri ya uchunguzi kwamba nini kinaendelea huko MKIRU ( Mkuranga, Kibiti na Rufiji). Siku ya 3 mfululizo Leo nasoma masuala haya na kupata mambo mengi ambayo huyapati kutoka Taarifa za Serikali.
Ni wakati mwafaka Kamati ya Bunge ya Usalama iende MKIRU kuonana na wananchi na askari pia. Kuna haja kubwa Sana Bunge kutoa Taarifa Maalumu kuhusu eneo la MKIRU.
Leo katika Gazeti la Mwananchi kuna Taarifa ya kwamba jeshi la polisi linaua raia wasio na hatia akiwemo kijana Sultani Mpingi ambaye alikutwa anafua nguo nyumbani kwao na kukamatwa na kuteswa mpaka kufa. Baba yake aitwaye Mussa Mpingi aliikuta maiti ya mwanae huko Muhimbili. Hii ni Habari ya kustusha mno na chombo pekee cha kufuatilia na kuchukua hatua ni Bunge.
Nawapongeza Sana Mwananchi na The Citizen Kwa kazi Hii muhimu ya uchunguzi.
@zittokabwe (Mb)
KC [HASHTAG]#ACTWazalendo[/HASHTAG]