Bunge la Zanzibar liko LIVE. Zanzibar sio Tanzania?

Shukrani A. Ngonyani

JF-Expert Member
Feb 23, 2014
1,182
2,015
Nape alituambia hawatoonesha LIVE bunge kwa ajili ya kupisha watu waende na kufanya kazi nyakati za mchana, kukwepa gharama ya kurusha matangazo ya moja kwa moja kupitia TBC.

Ila ajabu nimeona ZBC wanarusha LIVE vikao vya baraza la wawakilishi.

1. Je Zanzibar sio sehemu ya Tanzania?

2. Je wazanzibar hawaendi kazini?

3. Je ZBC hawatumii kodi za WATANZANIA?
 
Kama issue ni kufanya kazi basi TV zote zizimwe mpaka saa kumi, hizo TV watu wanapoteza muda kulingana na serikali ya awamu hii
 
1. Tofautisha kati ya Zanzibar Broadcasting Corporation na Tanganyika Brodcasting Corporation.
2. Bunge la Zanzibar ni la wanaCCM watupu wanaongea kile walichokubaliana na wanakubaliana kile wanachoongea kwa hiyo hakuna wanachohofia kuonyesha bunge live.
 
Nape alituambia hawatoonesha LIVE bunge kwa ajili ya kupisha watu waende na kufanya kazi nyakati za mchana, kukwepa gharama ya kurusha matangazo ya moja kwa moja kupitia TBC.

Ila ajabu nimeona ZBC wanarusha LIVE vikao vya baraza la wawakilishi.

1. Je Zanzibar sio sehemu ya Tanzania?

2. Je wazanzibar hawaendi kazini?

3. Je ZBC hawatumii kodi za WATANZANIA?
Hili swali ni vema akalijibu nape
 
1. Tofautisha kati ya Zanzibar Broadcasting Corporation na Tanganyika Brodcasting Corporation.
2. Bunge la Zanzibar ni la wanaCCM watupu wanaongea kile walichokubaliana na wanakubaliana kile wanachoongea.
Kumbe kushindwa kurusha live bunge ni kwa sababu bunge letu lina wabunge wa upinzani ambao wanaisumbua serikali kwa kuhoji mambo ya msingi
 
Wapinzan wakitoka bungen linakuwa live...wakiwepo wanazima...wanawaogopa sabab hoja zao n vgum kuzijib...
 
Bahati mbaya wewe hukumbuki mambo yaliyopita. Hukumbuki walisema hawana mamlaka na zenj japo walipeleka majeshi yetu kule?
 
Njia ya Muongo fup sana!! Naiyona serikali inakwenda kuumbuka vibaya sana...
 
Nape alituambia hawatoonesha LIVE bunge kwa ajili ya kupisha watu waende na kufanya kazi nyakati za mchana, kukwepa gharama ya kurusha matangazo ya moja kwa moja kupitia TBC.

Ila ajabu nimeona ZBC wanarusha LIVE vikao vya baraza la wawakilishi.

1. Je Zanzibar sio sehemu ya Tanzania?

2. Je wazanzibar hawaendi kazini?

3. Je ZBC hawatumii kodi za WATANZANIA?
Yaani mtu anayedai bunge kurushwa papo mpaka sasa lazima awe anamtindikio wa ubongo tu si bure.
 
Sababu ni rahisi sana, zanzibar bungeni hamna wapinzani hivyo hakuna wa kuwahaibisha mafisiem.
 
Leo bunge lilikua live TBC asubuhi. Nafikiri limerudi kimya kimya.
Kwasababu wapinzani hawapo so lazima waoneshe watu hamna kupingana goodluck yupo,agnes marwa,nape nauye,majaliwa kassim makatoon wote ni kucheza tu na vituko this is the time yakuonesha ngoja simba warudi uone bunge litarudi saa saba usiku tena edited
 
Back
Top Bottom