Bunge la Tanzania ambalo sio Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la Tanzania ambalo sio Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by King Suleiman, Feb 14, 2011.

 1. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  salaam wana JF,
  nimekaa na kulitafakari bunge letu tukufu la Tanzania na kugundua bunge letu ni bunge kwa jina lakini halifanyi kazi ya bunge haswa ambayo wananchi tunaitarajia na kuona mafanikio yakipatikana kupitia huko. nina sababu chache nitazieleza kisha mwenye nyongeza anaweza kuongeza.

  Bunge kwa tafsri nyepesi ni chombo cha uwakilishi wa wananchi, kusaidia kutatua kero zao na kutafuta njia ya kuleta maendeleo kwa wananchi, lakini kwa tanzania ni kutetea maslahi ya chama na ya binafsi.

  Bunge letu limekuwa sehemu ya kutetea maslahi binafsi ya chama na si maslahi ya taifa kama amabavyo tulitarajia bunge liwe. utakuta wabunge wa vyama fulani wako tayari kupitisha hoja mbovu au isiyo na manufaa kwa taifa kisa tu ni ya chama chao au kumlinda mtu wa chama chao asiaibike, kwa hakika inasikitisha sana.

  ukiangalia hata chaguzi za hizi kamati, utaifa na utendaji umewekwa pembeni na vyama vimeshika hatamu. Kama wewe sio muumini wa chama fulani au haupo kwenye ndoa yao, basi hata kama ni mtendaji na mfanisi kiasi gani tarajia kuanguka.

  bunge la sasa ndio limeleta ladha mpyakabisa, sasa mipasho, majungu kuzomeana na kukejeliana wazi kabisa ndio fasheni huku spika akiacha kukemea, huku akionekana dhahiri kuelemewa na shughuli iliyomuweka hapo mjengoni.

  Ndg zangu kwa mimi Bunge la Tanzania sio Bunge tena ila Vyama na Maslahi binafsi vimeshika hatamu na ile dhana ya uwakilishi wa wananchi haipo tena limebaki bunge jina tu.
  nawakilisha
   
 2. l

  limited JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  naunga mkono, nimekuwa nikifuatilia hasa kipindi cha jioni hakuna cha maana sana kwa mfano leo spika alikuwa akiwaambia wabunge wasipige makofi lakiini wanaendelea tuuu!!! amewakemea wabunge more than 4 times !!!! Sasa sijui hii semina walioyokaa more than a week walikuwa wanafanya nini kama hata hawana nidhamu ya kumsikiliza spika?
  yaani hata vikao vya harusi baa vina afadhali
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Spikaa?!!!!!!!!!!
   
 4. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  ndg yangu Bunge letu limepoteza muelekeo, kwa sasa ni porojo tu ndio hujadiliwa na ushabiki usio na maana, naogopa siku za usoni litapoteza kabisa mvuto na jamii itakuw haitegemei tena bunge zaidi ya kutegemea njia nyingine....
   
Loading...