Bunge la Iran laazimia kuongeza uzalishaji wa Nyuklia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Bunge la Iran limepitisha sheria ya kuwazuia wachunguzi wa Umoja wa Mataifa katika maeneo yao ya shughuli za kinyuklia na kuongeza uzalishaji wake wa Urani.

Sheria hiyo itaitaka serikali kurejelea urutubishaji wa urani kwa asilimia ishirini.

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema anapinga kupitishwa kwa sheria hiyo ambayo inakiuka makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2015 kati ya Iran na nchi zenye nguvu zaidi ulimwenguni ya kudhibiti mpango wa kinyuklia wa nchi hiyo kutokwenda zaidi ya asilimia 3.67 na kuongeza itahujumu diplomasia.

Bunge la Iran linataka wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wa kudhibiti silaha za kinyuklia kuzuiwa kuchunguza vitu vya kinyuklia na kuongeza uwezo wake wa kuzalisha urani katika kinu cha Natanz na Fordow iwapo vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran havitaondolewa katika kipindi cha miezi miwili ijayo.

Vikwazo hivyo vilivyolenga sekta ya mafuta na fedha ya Iran vilirejeshwa na nchi za magharibi baada ya Marekani kujiondoa kutoka makubaliano hayo ya kihistoria yaliyofikiwa 2015.

Rais Rouhani alisema serikali yake haikubaliani na ongezeko la gharama za shughuli za nuyklia

Hayo yanakuja baada ya mwanasayansi mwandamizi wa masuala ya nyuklia wa Iran Mohesn Fakhrizadeh kuuawa katika mazingira ya kutatanisha nje ya mji mkuu wa nchi hiyo Tehran Ijumaa iliyopita.

Iran inaamini kuwa Israel na kundi la Wairan walioiasi nchi na kukimbilia uhamishoni walitumia silaha inayodhibitiwa kwa remote kumuua mwanasayansi huyo.

Israel haijajibu madai hayo dhidi yake.

Iran yailaumu Israel kwa mauaji ya mwanasayansi wake wa nyuklia
Fakhrizadeh alikuwa na mchango muhimu katika mpango wa kinyuklia wa Iran ambao serikali inasisitiza kuwa shughuli zake za kinyuklia ni kwa ajili ya amani na sio kutengeza silaha za kinyuklia zinazouweka ulimwengu katika hatari.

Rais wa Marekani Donald Trump chini ya utawala wake alirejesha vikwazo vikali vya kiuchumi dhidi ya Iran akikosoa makubaliano yaliyofikiwa kwa kuyataja yenye mapungufu makubwa na yanayoipa Iran nguvu za kutengeza silaha za kinyuklia.

Rais Mteule wa Marekani Joe Biden ameahidi kuirejesha nchi yake kwa makubaliano hayo yaliyofikiwa wakati wa utawala wa Rais Barack Obama.
 
Waache haraka wamsubiri Biden ale kiapo airejeshe Marekani kwenye ule mkataba wa nyuklia.

Huenda huu mswada umepitishwa makusudi ukilenga utawala mpya wa Biden.
 
Hongera zao kwani kuna kosa gani kurutubisha?

Ambao tayari wanamiliki hizo silaha wao sio wa dunia hii?

Hivi tanzania tutaanza lini michakato kama hii? Natamani sana kusikia siku moja kuna kuna kinu kimewekwa hata hapo shinyanga kikirutubisha uranium
 
Hizi siraha kuwa nazo muarabu ni hatari kuliko hatari yenyewe waarabu wakitamka Takbriiii!

Hakuna huruma Ni kata funua twende hakibaki kitu. Ni mungu wao amesema wanaenda peponi. Tulaani kitendo hiki siraha zibaki hukohuko! Shukuruni tu hawa jamaa hawana uwezo na akili. mngeolewa wote
 
Hongera zao kwani kuna kosa gani kurutubisha?

Ambao tayari wanamiliki hizo silaha wao sio wa dunia hii?

Hivi tanzania tutaanza lini michakato kama hii? Natamani sana kusikia siku moja kuna kuna kinu kimewekwa hata hapo shinyanga kikirutubisha uranium
huku tunamradi wa kufyatua makasuku ya kusifu na kuabudu
 
Kwa akili zako za mafunza unafkiri ni Muarabu gani anaemiliki silaha za Nuclear, Huyo mzungu alishawahi kuzitumia na kuuwa maelfu ya watu Japan, acha ukuma dada
hivi broo unandugu huku uarabuni? au na wewe ni muarabu wa buza? maana sio kwa povu hilo
 
  • Thanks
Reactions: PNC
hivi broo unandugu huku uarabuni? au na wewe ni muarabu wa buza? maana sio kwa povu hilo
Naona alipokua akitoka povu huyo malaya apo juu ulinyamaza kimya, kulikoni unanilaumu mm, mm nimemjibu kulingana na alichocoment, kuna wengine wanastahili kujibiwa kulingana na wanavyocoment
 
Kwa akili zako za mafunza unafkiri ni Muarabu gani anaemiliki silaha za Nuclear, Huyo mzungu alishawahi kuzitumia na kuuwa maelfu ya watu Japan, acha ukuma dada
Unadhani ndo watakupenda? Niache ukuma unipe yako hiyo ya nyuma au?
 
Naona alipokua akitoka povu huyo malaya apo juu ulinyamaza kimya, kulikoni unanilaumu mm, mm nimemjibu kulingana na alichocoment, kuna wengine wanastahili kujibiwa kulingana na wanavyocoment
Tuliza mshono uzae weye. Mbona domo limechakaa kwa kuongelea chini tuu. Wamesha kuharibu nini? Hukawii kujilupua
 
Back
Top Bottom