Bunge la 11 kuandika historia

ila mbele ya Magufuri hakuna kitakacho haribika.
 

Hicho kisiwa hakihusiki na uchaguzi wa wabunge wa JMT, hakina jeshi, ila ina rais......
 

Jamani kuweni waelewa basi,mlishaambiwa hakuna uchaguzi wa wabunge Zanzibar uliofutwa,umefutwa ni uchaguzi wa ZEC Zanzibar na sio wa NEC,na mtambue kuwa sanduku huwa tafauti na wasimamizi tafauti kila tume inaajiri wasimamizi wake,tuulizeni sisi jamani msiropoke,na ndio maana majimbo yote ya Zanzibar ya ubunge wamewatangaza lkn ya uwakilishi na udiwani Zanzibar umefutwa.
 
Unamdanganya nani na kwa faida ya nani, eti wasimamizi tofauti wakati aliyekuwa anatiki ni yuleyule ndani ya daftari lilelile.
 

Kwa hiyo majina na vituo vya kupigia kura huwa ni tofauti na utangazaji matokeo huwa tofauti eeeh?
 

Mkuu ulipigia Kura Zanzibar na unajua uchaguzi ulivyokuwa au unatumia maneno ya Lubuva?
 
Ukifika katika kituo unapewa kura Tano hauruhusiwi kupigia wachache wengine uache labda uiharibu mwenyewe
Si hakika kama wanatumia daftari moja ila si kila anaweza kupiga kura za Rais wa SMZ na Baraza la wawakilishi na Mashekha anaweza kupiga za JMT
 

Samaritan;
Siku hizi wamekificha kile kitufe cha "Like" ila mimi nakupa like yangu. Naomba nitohoe kasehemu kaliko nitia wazimu; "kama serikali imekubali kwamba uchaguzi ulikua na kasoro, chujio gani limetumika kujua na kujiridhisha kwamba huo uvunjwaji wa taratibu uliathiri tu SMZ?"
Nawaombeni jamani, hatupingi uamuzi wenyu viongozi ila, penye kasoro muwe wazi tu. Mpiga hizo kura ni yule yule anayeingia ndani. Hawezi acha kupiga ile ya JMT kwani kitendo cha kuiacha kitaleta hayo maneno kuwa kura zimezidi walio andikwa.
Mlitumia chujio gani kuonesha kuwa kura hizo si maruhani?? Wa kuchaguliwa kishachaguliwa na NEC sawa ila next tyme hebu kuweni makini. Tujifunze tu kwa hili.
 
Mkuu Samaritan,

nimeingia kituoni wananipa karatasi za kupigia kura moja ya rais wa JMT nyingine ya rais wa SMZ, baada ya kupiga naambiwa kulikuwa na kasoro kosa wasimamizi walivua mashati kupigana, hata hivyo tunafuta kura yako moja nyingine inabaki,

inaingia akilini kweli?
 
Last edited by a moderator:
ZEC walisema haukuwa huru na haki idadi ya majina ilizidi, kwani kulikuwa na daftari mbili tofauti na wasimamizi tofauti na vituo tofauti?
Daftari ni moja lakini kuna wapiga kura ambao hawana vigezo kupiga kura kwa Raisi na wawakilishi wa Zanzibar bali wanaweza kupiga kura kwa wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano!
 
NEC haiko Zanzibar bali ni ZEC inasimamia chaguzi zote, wa muungano wakifanya hivyo kiwakala. Pili hakuna Mashekha wanaochaguliwa katika chaguzi hizi bali ni madiwani. Mashekha uteuliwa ndiyo maana wanalalamikiwa san na vyama vya upinzani.
 
Wabunge wa Bunge la Muungano kutoka Zanzibar wamepatikana na watakuwepo. Wabunge watakaokosekana kati ya kiwango juu kabisa cha wabunge 394 wa bunge la 11 ni wale 8 wa majimbo aambayo uchaguzi haujafanyika, wabunge 10 wateuliwa wa Rais ambao bado hawajateuliwa, watano kutoka baraza la wawakilishi la Zanzibar ambalo bado halipo na wabunge watatu wa viti maalum wanawake ambao watateuliwa baada ya uchaguzi wa majimbo 8 kufanyika.
 
na vp weny vigezo vyote?au ilikua ukpga moja unapunga upepo then unarud kupga ya JMT kwa usahih baada ya kuharibu ya SMZ
 
Mtoa post unaonekana makala zako unatoaga kwasabab hisia zinakutuma,hutumii udadavuzi huzichambui hufanyi research napata wasiwasi kama ww ni msomi hata kama umesoma basi ulishindia madesa tu,,,,No research no right to speak ,sikudharau lkni huo ndo ukwel
 
Tatizo ni watu kutojua sheria someni kwanza katiba ndio utoe hoja na kama huna ufahamu wa sheria uliza
 
Nipe link ya mada zako zilizodadavuliwa na mimi niongeze ujuzi,
nevertheless si kila anayengia humu ni msomi wa level yako tuvumiliane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…