Bunge kutuongezea Tozo, je tulihukumu?

Bunge kutuongezea Tozo, je tulihukumu?

Kazwala mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2016
Posts
1,034
Reaction score
2,250
Salaam

Kawaida ya watu wanaoamini ushirikina wanapogundua kuwa fulani ndiye aliyempiga zongo mwanawe, huwa hawana furaha nae tena hata akijichekesha.

Katika maofisi, watu wanapogundua kuwa fulani ndiye anaeleta fitina ili wenzake waharibikiwe katika shughuli zao, huyu hutengwa mazima kama si kunyooshwa.

Leo hii sisi Watanzania ambao asilimia kubwa tunaishi maisha ya kuunga unga na huku tukikatwa makodi chungu nzima kiasi kwamba ili uendelee inahitaji mkono wa Mungu kwa kweli, tumegundua tunasalitiwa na Bunge ambalo ni kikundi cha watu wachache wenye kuishi kwenye neema ya hali ya juu! Kila mwisho wa mwezi wanakunja mamilioni achilia mbali mikopo ya magari, lita za mafuta maelfu bure na viinua mgongo vizito wasivyovilipia kodi, leo hii wanatukandamiza sisi Wananchi kwa kigezo cha uzalendo!!!

Kama wana uzalendo si wangekata makato yao wao yajenge nchi?

Hawa ndio wanaojigamba kuwa wanawakilisha Wananchi?

Ni wazi hawa ndiyo mchawi mkubwa katika Taifa na lengo lao ni kutuchonganisha na Mh. Rais.

Kwa kukurupuka kwao kujipendekeza kwa Mh. na kutuumiza sisi, je ikitokea tukipata Rais asiyesikiliza Wananchi, je unafikiri atarudi nyuma kusikiliza malalamiko yetu kama hivi?

Ndugu zangu, karibuni tujadili bunge letu tukufu.
 
achana na bunge la ndugai na wabunge wake. Waache waendeleze ujinga wao...wakumbuke makonda aliwaambia kitu gani huko
 
A25100E1-3B9D-4EA8-AC3B-AA67011DCF70.jpeg


4548666B-F0D0-4F77-99A9-C322C9601DE9.jpeg
 
Back
Top Bottom