Bunge Kuendelea Mafichoni, Uwongo wa Magufuli/CCM

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Miezi Michache iliyopita Waziri wa habari alilitaarifu Bunge Kuwa Serikali imesitisha Mataangazo ya Moja kwa Moja ya Bunge kwa ajili ya Kubana Matumizi, Huu nilijua ni Uwongo, Uwongo wa Serikali ya CCM, Kwani waliamini Kuwa Njia pekee iliyowapa Upinzani Kukubalika na Wananchi ni Matangazo ya moja kwa moja ya Bunge. Pia walifedheheka sana siku ile ambayo Rais alihutubia Bunge na, "Aliyekuwa Rais wa Zanzibar" Mohamed Shein Akazomewa!

Kwa Mtazamo Makini Ni kuwa Kuzuiwa Matangazo ya Bunge Hakukuwa na Nia Nzuri na Kutaruhusu Bunge Kuendeshwa Vibaya, Kutaendelea Kulea Rushwa na Mikataba ya Vificho. Na Pia kutawezesha Ukandamizaji wa Wabunge wa pande zote ambao wanataka Kufanya kazi yao Kizalendo Kusimamia Serikali na Kupinga Utawala mbovu.

Ushauri wangu Ni Kuwa, Kunapokuwa na Kupigwa Vita sio wakati wa Kulia lia bali Ni Muda wa Kutafuta Mbinu mpya ya kufikia malengo yale yale na Zaidi.

Kinachosikitisha Wabunge wa Upinzani na wale wa CCM wanaotaka Kuleta Mabadiliko ya Kweli nchini Ukiwashauri wanapuuza. Mfano, Badala ya Maandamano, Wabunge wote wa Upinzani na wale wa CCM wanaotaka Mabadiliko Halisi na ya Kudumu wanaweza:-

a) Kuvaa Skafu zinazosema, Tunataka Katiba mpya na Huru.
b) Wanaweza Kuanzisha Channel Mpya ya Ya Internet, (eg,Youtube, hata Pope anayo) Na Kurusha Matangazo/Video zote za Vikao vya Bunge. Watarekodi Vipi? Kuna Clear eye glasses zenye Uwezo wa Kuchukua HD Video kwa zaidi ya Dakika 250. Inarekodi Video na Sauti ya Kila Unachoona na Unachosikia. Wanaweza Kufanya Hivi Kwa Kuwa na Miwani Kadhaa kwa Wabunge Kadhaa na Kurekodi kwa Zamu. (Natamani Tusifikie huku, ila kama Serikali inayataka hayo hakuna jinsi)
c) Wanapotaka Support ya Wananchi wanaweza Kuchapisha Kanga, Tshirts, Kofia kwa Mamilioni na Kuwapa Wanachi wanaotaka Mabadiliko ya kweli Bure. (Italeta Nguvu kuliko Maandamano)
Wanaweza Kuwapa Wasanii fedha na Kuwaomba watunge Senema, Michoro, Na Miziki inayohamasisha na Kudai Mabadiliko. (Kwa njia ya Kutangaza Tenda ya Siri na Watakaotunga Senema, au Muziki Mzuri Watakuwa promoted, Hata Hollywood wamekuwa kwa miaka mingi wakilipwa kutunga senema zenye jumbe maalumu!)
d) Wanaweza Kulipia Mabango Kudhamini Jumbe zinazodai Mabadiliko, bila Kumkashifu Kiongozi au Chama Kingine.

Nikimalizia, Niwakumbushe Watanzani, Mnakumbuka harakati za Kukomboa Kusini mwa Afrika, na Kushinikiza Mandela Afunguliwe zilivyohusisha, Nyimbo za Mchakamchaka, Miziki, Senema, Mavazi, Vikwazo vya Uchumi etc?

Mimi Naamini Mh. Magufuli anajitahidi, Na nampenda Kama Nini, Lakini anafanya Kosa Kubwa sana, sana, anaendeleza Tabia ya Kuwalea na Kuwabebabeba CCM, Tabia ambayo Ndiyo Iliyoharibu sana nchi yetu na CCM yenyewe. Watu wazuri na Thabiti walio katika CCM hawahitaji Kubebwa au Kupendelewa na yeyote. Kuendelea Kubeba na Kujenga Mfumo wa Kukipendelea Chama Tawala Kunawanufaisha wale tu, Mafisadi, Magoigoi na "Good for Nothing" Katika CCM, Na Kufanya hivyo Kunawahujumu sana Wale waliosafi na Wachapakazi Katika CCM, akiwepo Rais Mwenyewe! The actions of a good leader should be his own Ladder! and not otherwise.

KWA UPANDE WA SERIKALI, MIMI NINGESHAURI, RAIS AFUNGE MACHO AFANYE UTAKASO HASA KWA CCM, KWA KUJENGA MFUMO UTAKAOKUWA WAZI NA WA HAKI KWA SIASA ZA NCHI YETU NA WOTE WALIOWAZALENDO, CCM NA UKAWA WATANUFAIKA! NA WANANCHI WATAKUWA WASHINDI WA KWELI. MFUMO HUO UWEKE UGUMU WA WACHAFU KUKATIZA, NA UWEZESHE WACHAFU WALIOKO KUBAINIKA NA "WAENDE NA MAJI"
 
Kitendo cha kutunyima matangazo ya moja kwa moja ni ubakaji wa democrasia. Bunge ni chombo
Cha kutusemea sisi wananchi wa hali ya chini tulipaswa tufahamu kinachoendelea ndani ya bunge kama ilivyokuwa.
 
Bora lisirushwe papo kwani hicho ni kikao cha kazi watu wanabungua bongo. Siri ya bungua bongo mchangiaji husema chochote anachoona kinafaa kuwa suluhu. Mengine si mazuri kuja moja kwa moja kwa wananchi.
Pia chadema hutumia muda huo kuuza sura na kuyumbisha uamuzi kwani kwenye kamati wanakubari wakimurikwa kwenye kamera wanapinga michango yao. Sasa njia ni kuondoa kifaa kinachowapa uwendawazimu.
 
Makalio ya mala
 
Unajishushia hadhi wewe watu wanazungmzia kuona live wewe na Chadema kwani Camera zinachagua? Sema hutaki watu waone matusi ya akina kibajaji na mengineyo.
 
Kweli Unasema haya kwa nia nzuri?
 
Hamnaga kazi za kufanya zingine muendelee na maisha kiliko kung'ng'ania kuona live kila siku toka j3 mpaka ijumaa saa 3 asuhi mpka saa7 mchna na saa10 jioni mpka saa 2 usiku mmegeuza ajira hiyo!!
 
Kwamba Watanzania Wanakazi ya Kufanya au La sio Kazi yako Kuwapangia, Hata nchi zilizoendelea Kuna Luninga Maofisini, Waangalie nini ni Policy za Ofisi na sio Serikali iwapangie, Mwishoni Mtawapangia watu wale saa ngapi na walale saa ngapi wavae nini Nk
 
Hivi unadhani kunapokuwa na mjadala mkali kuhusu uharibifu wa mazingira bonde la Rufiji ni Watanzania wote wanaelekeza macho yao kwenye TV? Hapana ni kwa vile hata wengine hawajui hiyo Rufiji iko upande gani lakini wakazi wa Rufiji watafuatilia kwa makini na kujua Mbunge au serikali yao wanalichukuliaje jambo hilo. Vivyo hivyo kwa masuala mengine.
Maana yangu ni kuwa hakuna Mtanzania anayeweza kuangalia kila kitu na kushindwa kufanya kazi, ataangalia kile kinachomuhusu basi na kwa muda mfupi tuu.
 
Miezi Michache iliyopita Waziri wa habari alilitaarifu Bunge Kuwa Serikali imesitisha Mataangazo ya Moja kwa Moja ya Bunge kwa ajili ya Kubana Matumizi, Huu nilijua ni Uwongo, Uwongo wa Serikali ya CCM, Kwani waliamini Kuwa Njia pekee iliyowapa Upinzani Kukubalika na Wananchi ni Matangazo ya moja kwa moja ya Bunge. Pia walifedheheka sana siku ile ambayo Rais alihutubia Bunge na, "Aliyekuwa Rais wa Zanzibar" Mohamed Shein Akazomewa!

Kwa Mtazamo Makini Ni kuwa Kuzuiwa Matangazo ya Bunge Hakukuwa na Nia Nzuri na Kutaruhusu Bunge Kuendeshwa Vibaya, Kutaendelea Kulea Rushwa na Mikataba ya Vificho. Na Pia kutawezesha Ukandamizaji wa Wabunge wa pande zote ambao wanataka Kufanya kazi yao Kizalendo Kusimamia Serikali na Kupinga Utawala mbovu.

Ushauri wangu Ni Kuwa, Kunapokuwa na Kupigwa Vita sio wakati wa Kulia lia bali Ni Muda wa Kutafuta Mbinu mpya ya kufikia malengo yale yale na Zaidi.

Kinachosikitisha Wabunge wa Upinzani na wale wa CCM wanaotaka Kuleta Mabadiliko ya Kweli nchini Ukiwashauri wanapuuza. Mfano, Badala ya Maandamano, Wabunge wote wa Upinzani na wale wa CCM wanaotaka Mabadiliko Halisi na ya Kudumu wanaweza:-

a) Kuvaa Skafu zinazosema, Tunataka Katiba mpya na Huru.
b) Wanaweza Kuanzisha Channel Mpya ya Ya Internet, (eg,Youtube, hata Pope anayo) Na Kurusha Matangazo/Video zote za Vikao vya Bunge. Watarekodi Vipi? Kuna Clear eye glasses zenye Uwezo wa Kuchukua HD Video kwa zaidi ya Dakika 250. Inarekodi Video na Sauti ya Kila Unachoona na Unachosikia. Wanaweza Kufanya Hivi Kwa Kuwa na Miwani Kadhaa kwa Wabunge Kadhaa na Kurekodi kwa Zamu. (Natamani Tusifikie huku, ila kama Serikali inayataka hayo hakuna jinsi)
c) Wanapotaka Support ya Wananchi wanaweza Kuchapisha Kanga, Tshirts, Kofia kwa Mamilioni na Kuwapa Wanachi wanaotaka Mabadiliko ya kweli Bure. (Italeta Nguvu kuliko Maandamano)
Wanaweza Kuwapa Wasanii fedha na Kuwaomba watunge Senema, Michoro, Na Miziki inayohamasisha na Kudai Mabadiliko. (Kwa njia ya Kutangaza Tenda ya Siri na Watakaotunga Senema, au Muziki Mzuri Watakuwa promoted, Hata Hollywood wamekuwa kwa miaka mingi wakilipwa kutunga senema zenye jumbe maalumu!)
d) Wanaweza Kulipia Mabango Kudhamini Jumbe zinazodai Mabadiliko, bila Kumkashifu Kiongozi au Chama Kingine.

Nikimalizia, Niwakumbushe Watanzani, Mnakumbuka harakati za Kukomboa Kusini mwa Afrika, na Kushinikiza Mandela Afunguliwe zilivyohusisha, Nyimbo za Mchakamchaka, Miziki, Senema, Mavazi, Vikwazo vya Uchumi etc?

Mimi Naamini Mh. Magufuli anajitahidi, Na nampenda Kama Nini, Lakini anafanya Kosa Kubwa sana, sana, anaendeleza Tabia ya Kuwalea na Kuwabebabeba CCM, Tabia ambayo Ndiyo Iliyoharibu sana nchi yetu na CCM yenyewe. Watu wazuri na Thabiti walio katika CCM hawahitaji Kubebwa au Kupendelewa na yeyote. Kuendelea Kubeba na Kujenga Mfumo wa Kukipendelea Chama Tawala Kunawanufaisha wale tu, Mafisadi, Magoigoi na "Good for Nothing" Katika CCM, Na Kufanya hivyo Kunawahujumu sana Wale waliosafi na Wachapakazi Katika CCM, akiwepo Rais Mwenyewe! The actions of a good leader should be his own Ladder! and not otherwise.

KWA UPANDE WA SERIKALI, MIMI NINGESHAURI, RAIS AFUNGE MACHO AFANYE UTAKASO HASA KWA CCM, KWA KUJENGA MFUMO UTAKAOKUWA WAZI NA WA HAKI KWA SIASA ZA NCHI YETU NA WOTE WALIOWAZALENDO, CCM NA UKAWA WATANUFAIKA! NA WANANCHI WATAKUWA WASHINDI WA KWELI. MFUMO HUO UWEKE UGUMU WA WACHAFU KUKATIZA, NA UWEZESHE WACHAFU WALIOKO KUBAINIKA NA "WAENDE NA MAJI"
CCM wanajisumbua tu maana tunapata update za huko mjengon daily kupitia social medias,tena vya kuambiwa bila kuona vina ushawish mkubwa sana tu
 
Kwa kweli kuna haja ya hili jambo kujadiliwa kwa kina na wote tufikie mwafaka wa pamoja.

Vinginevyo kwa kweli umetoa ushauri mzuri sana na unaofaa. Na ni kweli pia kuwa, hata ndani ya serikali na ndani CCM kwenyewe wapo wengi sana wasiokubaliana na maamuzi haya ya ajabu na ya kijinga kuwahi kutolewa!!

Inafika wakati watu wenye akili na utambuzi wanajiuliza ni kwa nini Rais John P. Magufuli na serikali yake pamoja na chama chao CCM wanakuwa too defensive kiasi hiki!?

Wanaogopa nini na wanataka kuficha nini eti kiasi ambacho wanazuia vituo vyote vya matangazo ya Radio na Television kurusha matangazo yote ya bunge yakiwa mabichi "live?"

Mimi na nadhani watu wengine pia walikuwa na matarajio kuwa badala ya kuturudisha nyuma, tungesonga mbele zaidi kwa kuhakikisha kuwa hata vikao vya kamati za kudumu za bunge pamoja na vya mabaraza ya madiwani ya wilaya, miji, manispaa na majiji kwa kutumia local TVs na Radio za maeneo yao yanafanyika kwa uhuru na uwazi kabisa kwa kila mwananchi mwenye nafasi ya kufuatilia wawakilishi wao wanajadili nini juu mipango na maendeleo yao anafuatilia!!

Ni vigumu sana kupata maendeleo ya kweli chini ya watawala wapenda sifa na wenye kufanyia mambo yao gizani.

Mimi TL Marandu nitofautiane na wewe juu ya nia na dhamira ya Rais JPM, kwamba HAPANA si njema kama ulivyomsifia!!

Laiti ingekuwa ni njema na anataka kuleta mabadiliko ya kweli na halisi kama alivyohubiri wakati wa kampeni, hatua ya kwanza ingekuwa na kupingana na maamuzi haya waziwazi dhidi ya hujuma ya demokrasia. Lakini kilichotokea ni kukubaliana. Labda ajirudi na kukubali kuwa hakutafakari kwa makini kabla ya kukubaliana na ushauri wa waziri wake wa habari juu ya hili!!

Vingenevyo, hakuna kitu hapa. Huyu naye ni msanii tu, hana tofauti na JK labda wanatofautiana njia tu za kufanyia usanii wao. JPM usanii wake umechanganyikana na ghiliba za kama kila anachofanya ni KWELI na HAKI tupu hata watu wanapumbaa na kupumbazika hata kuuamini usanii wake!!

Tatizo la usanii wa namna hii ni kuwa, pengine ukaanza kumrudi yeye mwenyewe si muda mrefu. Na siku hawahawa wanaokenua meno na kumshangilia leo watakapokuja kugundua kuwa ilikuwa ni usanii tu, watakata tamaa hadi mwisho na kumdharau moja kwa moja!!

Let's wait, time itself will tell.
 
Kwamba Watanzania Wanakazi ya Kufanya au La sio Kazi yako Kuwapangia, Hata nchi zilizoendelea Kuna Luninga Maofisini, Waangalie nini ni Policy za Ofisi na sio Serikali iwapangie, Mwishoni Mtawapangia watu wale saa ngapi na walale saa ngapi wavae nini Nk

Wanaofanya kazi maofisini ni kiasi kidogo saana ktkt nchi ya watu 45 million wengi wakulima na wajasiliamali ambao wanahangaika nje sio mdani ya maofisi hiyo kulazimisha kuangali ni ukosefu wa kazi za kufanya hata ofisin mtu kafuata huduma unaona huyu ananiharibia unamlipulia tu ajiondokee ubaki na kuangalia bunge time ya kazi lazima tukubaliane mambo mengine yasiyo muhimu kuna vipindi
 
Umeleta hoja ya msingi ambayo mimi binafsi niliwahi ileta hapa JF japo zinatofautiana kidogo na pia kuna member mwingine nae aliwahi leta wazo linalofanana na hili hapa JF ila bahati mbaya sana ni kuwa hoja kama hizi sio hoja mpaka zitolewe na watu maarufu ndio zitakubalika na kupewa uzito.
 
Taarifa za bunge zimekuwa bidhaa sana.Wananchi tunanyimwa fursa ya kufatilia mijadala kuhusu maendeleo ya nchi yetu.
 
Umeleta hoja ya msingi ambayo mimi binafsi niliwahi ileta hapa JF japo zinatofautiana kidogo na pia kuna member mwingine nae aliwahi leta wazo linalofanana na hili hapa JF ila bahati mbaya sana ni kuwa hoja kama hizi sio hoja mpaka zitolewe na watu maarufu ndio zitakubalika na kupewa uzito.

Nimejaribu sana Kutoa Ushauri na Maoni, Lakini mengine wanapuuza. Au niseme labda hawafuatilii Watanzania wanawaza Nini, Wangeweka Mtu maalumu wa kuyatambua Mawazo ya Watanzania Kupitia Kila Media na Platform ili kuweza kuwa na Ufanisi zaidi Kama Wanasiasa.
 
Mkuu, kuna jambo moja kuhusu wapinzania ambalo naomba leo nilisema hapa na kwa nitakaowakwza watanisamehe.

Uchaguzi umepita hivyo nao wamepunguza sana harakati zao za kisiasa na ndio maana hata hili swala la Bunge kutokurushwa live hawaonekani kuliwekea mikakati madhubutu kukabiliana nalo.Hata maswala ya Tume Huru ya Uchaguzi,mgombea binafsi,matokeo ya uraisi kuhojiwa mahakamani nayo kwa sasa kimya kwasababu wanaona uchaguzi bado uko mbali.

Ninachowaambia wapinzani,acheni kujisahau anzeni harakati hizi sasa kwani hakuna aijue kesho zaidi ya mungu ingawa hatuombei mabaya lakini binadamu hata akiwa raisi alieko madarakani bado ni binadamu tu kama wengine.
 
Ma
Unajishushia hadhi wewe watu wanazungmzia kuona live wewe na Chadema kwani Camera zinachagua? Sema hutaki watu waone matusi ya akina kibajaji na mengineyo.
Matusi ni matusi atoe Kibajaji, Sugu, Msigwa au Mdee ni matusi tu hatutaki kuyaona papo. Kumbe tupo pamoja
 
Unavyosema, "Hatutaki" Unajisemea kwa binafsi yako na Nani? Unajua wazi unachosema hapa ni Unafiki mtupu!
 
Back
Top Bottom