Bunge kuchunguza ufisadi wa Sh. 200 bilioni za Meremeta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge kuchunguza ufisadi wa Sh. 200 bilioni za Meremeta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by palalisote, Aug 5, 2011.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  BUNGE, kupitia Kamati yake ya Nishati na Madini litachunguza ufisadi wa zaidi ya Sh205.9 bilioni unaodaiwa kufanywa kupitia Kampuni ya uchimbaji madini ya Meremeta iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

  Kamati Ndogo ya Madini ya Bunge itafanya uchunguzi wa uhalali wa malipo ya Dola za Marekani 132 milioni (sawa na Sh205.9 bilioni kwa viwango vya sasa vya kubadilishia fedha ambacho ni Sh1,560 dhidi ya Dola) ambazo zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenda Ned Bank ya Afrika Kusini ikiwa ni malipo ya mkopo wa Dola 10milioni uliokuwa umechukuliwa na Kampuni ya Meremeta Ltd.

  Hatua hiyo imekuja baada ya mvutano wa muda mrefu, ulisababishwa na hoja zilizokuwa zikitolewa na Serikali kwamba suala la Meremeta lisingeweza kufanyiwa uchunguzi kutokana na "sababu za kiusalama."

  Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na Mwananchi na kuthibitishwa Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel umebaini kwamba Spika wa Bunge, Anne Makinda ameridhia kufanywa kwa uchunguzi huo kupitia Kamati Ndogo ya Nishati na Madini ya Bunge.

  Pendekezo la kuundwa kwa Kamati hiyo ndogo lilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, January Makamba wakati akitoa maoni ya Kamati yake kuhusu Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Julai 15, mwaka huu, wakilenga kuchunguza nafasi ya Kampuni ya Pan African Energy katika mchakato wa uzalishaji wa gesi ya Songosongo.

  Awali, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe alikuwa amewasilisha barua kwa Katibu wa Bunge akitoa taarifa ya hoja ya kuunda Kamati Teule ya Bunge kwa ajili ya kuchunguza tuhuma za ufisadi kupitia kampuni hiyo ya uchimbaji wa dhahabu ya Meremeta.

  "Spika ameona kwamba ni bora suala hilo la Meremeta likafanyiwa kazi na Kamati Ndogo ya Nishati na Madini ambayo itaundwa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake mengine," alisema Joel simu jana.

  Alisema hatua hiyo itaepusha gharama kubwa ambazo zingeweza kutumika kama Bunge lingeamua kuunda kamati teule kama Zitto alivyokuwa amependekeza.

  "Hili linafanyika kwa mujibu wa kanuni na kwa kuwa tayari kamati ilikuwa imependekeza kuundwa kwa kamati ndogo, basi Spika aliona ni vyema jukumu hili likafanyike hukohuko," alisema Joel na kuongeza:

  "Tayari nimezungumza na Mheshimiwa Zitto kuhusu uamuzi huu wa Spika lakini nitamjulisha kwa barua rasmi na pia Mwenyekiti wa Kamati naye atajulishwa maelekezo hayo ya Spika."

  Kwa upande wake, Makamba alisema kamati husika tayari imeishapendekezwa kwa Spika, lakini hakuwa tayari kuwataja wajumbe wa kamati hiyo.
  Hata hivyo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba miongoni mwa wajumbe wa Kamati hiyo ndogo waliopendekezwa ni Mbunge wa Simanjiro (CCM) Christopher Ole Sendeka ambaye amejipambanua kuwa miongoni mwa wanasiasa wanaopiga vita ufisadi nchini.

  "Kamati yetu ina uwezo wa kufanya kazi hizi wala sina wasiwasi hata kidogo, lakini sijapata maelekezo ya Spika hivyo siwezi kuingia kwa undani kuhusu jambo hili hadi hapo nitakapokuwa nimepata maelekezo hayo," alisema Makamba.

  Hoja ya Zitto

  Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) alikuwa ametoa hoja ya kutaka iundwe kamati teule ya Bunge kwa ajili ya kuchunguza ufisadi huo.

  Zitto alitoa taarifa ya mdomo bungeni Julai 13, mwaka huu kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge Namba 117 (2)-(a) inayomruhusu kutoa taarifa ya kusudio lake la kuwasilisha hoja ya kutaka Bunge liunde kamati teule. Julai 15, mbunge huyo alimwandikia Spika Makinda barua kutoa taarifa ya hoja husika.

  "Kuna haja ya kujua uhalali wa ongezeko la Dola milioni 122 zilizoongezeka katika malipo hayo," alisema Zitto katika barua yake kwenda kwa Spika.Alisema kitendo cha kurejesha mkopo huo pamoja na faida ya zaidi ya asilimia 1,000 kinaashiria kuwepo kwa ufisadi wa fedha za umma na ni jambo ambalo haliwezi kuvumilika lipite bila kuwekwa wazi.

  Zitto alielezea kushangazwa kwake na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi kutolifafanua suala hilo kwenye majumuisho ya bajeti yake kwa mwaka 2011/12, hivyo kusema kuwa upo umuhimu wa Bunge kuliweka wazi suala hilo kwa wananchi.

  Fedha hizo zilichukuliwa kupitia kampuni ya Meremeta ambayo iliundwa na Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Afrika Kusini ya Triennex PTY, hivyo kuchukua mkopo huo wa Dola 10 milioni, lakini kiasi kilichorejeshwa baadaye ndicho kinachotia shaka.Zitto alisema katika kurejesha fedha hizo, Serikali iliamuru BoT iilipe Nedbank na ilitekeleza agizo hilo mwaka 2004.

  Meremeta ilikotokea
  Suala la Meremeta ni la muda mrefu na mara nyingi Serikali imekuwa haiko tayari kulizungumzia kwa maelezo kwamba ni suala ambalo lina maslahi ya kiusalama kwa taifa.

  Awali, Serikali ilisema kwamba Meremeta Ltd ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na JWTZ kwa ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Mkoa wa Pwani. Taarifa za usajili zilizotolewa na Msajili wa Makampuni wa Uingereza na Wales zinabainisha kuwa kampuni hiyo iliandikishwa nchini humo mwaka 1997 na baadaye ilifilisiwa huko huko Uingereza mwaka 2006.

  Taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ya Mei 31, 2005 inabainisha kwamba Meremeta Ltd ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania, Oktoba 3, 1997 na kwamba hisa 50 za kampuni hiyo zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini, wakati hisa 50 zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania.

  Utata mkubwa kuhusu umiliki wa Meremeta Ltd unatokana na taarifa ya Brela ambayo pia inazitambua kampuni mbili za Kiingereza ambazo ni London Law Services Ltd na London Law Secretarial Ltd kuwa wamiliki wa hisa moja kila moja ndani ya Meremeta.

  Licha ya Serikali kutokuwa mmiliki pekee wa kampuni hiyo, BoT ililipa madeni yote ya Meremeta badala ya kusaidiana na washirika wake ambao kisheria wanaonekana kuwa walikuwa wakimiliki hisa katika kampuni hiyo.

  Serikali Tanzania ilikuwa ikimiliki asilimia 50 ya hisa na kwa mujibu wa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), uhalali wa malipo hayo ulikuwa na walakini kwani kiutaratibu Nedbank Ltd ilitakiwa iachwe idai fedha zake kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo kama ilivyo kwa wadeni wengine.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,924
  Likes Received: 12,124
  Trophy Points: 280
  BUNGE, kupitia Kamati yake ya Nishati na Madini litachunguza ufisadi wa zaidi ya Sh205.9 bilioni unaodaiwa kufanywa kupitia Kampuni ya uchimbaji madini ya Meremeta iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).Kamati Ndogo ya Madini ya Bunge itafanya uchunguzi wa uhalali wa malipo ya Dola za Marekani 132 milioni ambazo zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenda Ned Bank ya Afrika Kusini ikiwa ni malipo ya mkopo wa Dola 10milioni uliokuwa umechukuliwa na Kampuni ya Meremeta Ltd.

  Hatua hiyo imekuja baada ya mvutano wa muda mrefu, ulisababishwa na hoja zilizokuwa zikitolewa na Serikali kwamba suala la Meremeta lisingeweza kufanyiwa uchunguzi kutokana na “sababu za kiusalama.”

  Source: Mwananchi
   
 3. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Are they really serious! Another Episode.
   
 4. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ze Komedi au Futuhi? Huko nyuma Serikali ilishakataa kuzungumzia suala la Meremeta, leo kamati inaundwa ili iweje? Ama ushahidi utakuwa umeshapotezwa au wanaunda kamati kama kiini macho cha kulipotezea mbali suala hilo.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  It needs a character to touch the unknowns
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi kuna tamko lolote kubwa ambalo Waziri Mkuu Pinda ametoa likaachwa bila kugeuzwa? Aliwahi kusema Meremeta ni 'untouchable' sasa hii kamati ya bunge itaenda kuchunguza Meremeta ya Ureno ya Tanzania? Where does this leave our PM in terms of credibility?
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  deleted!
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ok guys stop there!!!! kwa kuletwa hii ni proof kwamba"THE SHIMBO STORY IS ABSOLUTELY TRUE" if you can read btn the letters!!!!!!!!!!!!!!! Cry my beloved country!!!!!!!
   
 9. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  naunga mkono hoja... ingekuwa ni story ya uongo jinsi magamba walivyo na usongo na Jf wangeshaizika mpk muda huu....
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Achilia hiyo, hii ishu hata Pinda alishasema haiwezi kuzungumzika maana inahusu jeshi na vyombo vya usalama, the guy was ready to be crucified just for ths meremeta thing, ghafla from nowhere, speaker tena Anna Makinda eti anaitisha uchunguzi gademu!!!!!!
   
 11. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umeona mkuu eeh? Twende kazi SHIMBO lazima aanikwe ili arudishe matrilion yetu bana..
   
 12. V

  Vonix JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Pinda alitakataa kuzungumzia meremeta hilo lipo wazi kabisa yaelekea ushahidi umeishapotezwa wanasiasa vigeugeu,ikulu vigeugeu,bungeni vigeugeu,spika kigeugeu,magamba vigeugeu nadhani huu wimbo unaopigwa sana siku hizi unawafaa viongozi waliopo madarakani.
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Bunge kuchunguza ufisadi wa Sh200 bilioni za Meremeta
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 05 August 2011 21:01 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Bunge likiendelea mjini Dodoma

  Waandishi Wetu
  BUNGE, kupitia Kamati yake ya Nishati na Madini litachunguza ufisadi wa zaidi ya Sh205.9 bilioni unaodaiwa kufanywa kupitia Kampuni ya uchimbaji madini ya Meremeta iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).Kamati Ndogo ya Madini ya Bunge itafanya uchunguzi wa uhalali wa malipo ya Dola za Marekani 132 milioni (sawa na Sh205.9 bilioni kwa viwango vya sasa vya kubadilishia fedha ambacho ni Sh1,560 dhidi ya Dola) ambazo zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenda Ned Bank ya Afrika Kusini ikiwa ni malipo ya mkopo wa Dola 10milioni uliokuwa umechukuliwa na Kampuni ya Meremeta Ltd.

  Hatua hiyo imekuja baada ya mvutano wa muda mrefu, ulisababishwa na hoja zilizokuwa zikitolewa na Serikali kwamba suala la Meremeta lisingeweza kufanyiwa uchunguzi kutokana na “sababu za kiusalama.”

  Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na Mwananchi na kuthibitishwa Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel umebaini kwamba Spika wa Bunge, Anne Makinda ameridhia kufanywa kwa uchunguzi huo kupitia Kamati Ndogo ya Nishati na Madini ya Bunge.Pendekezo la kuundwa kwa Kamati hiyo ndogo lilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, January Makamba wakati akitoa maoni ya Kamati yake kuhusu Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Julai 15, mwaka huu, wakilenga kuchunguza nafasi ya Kampuni ya Pan African Energy katika mchakato wa uzalishaji wa gesi ya Songosongo.

  Awali, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe alikuwa amewasilisha barua kwa Katibu wa Bunge akitoa taarifa ya hoja ya kuunda Kamati Teule ya Bunge kwa ajili ya kuchunguza tuhuma za ufisadi kupitia kampuni hiyo ya uchimbaji wa dhahabu ya Meremeta.
  “Spika ameona kwamba ni bora suala hilo la Meremeta likafanyiwa kazi na Kamati Ndogo ya Nishati na Madini ambayo itaundwa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake mengine,” alisema Joel simu jana.

  Alisema hatua hiyo itaepusha gharama kubwa ambazo zingeweza kutumika kama Bunge lingeamua kuunda kamati teule kama Zitto alivyokuwa amependekeza.
  “Hili linafanyika kwa mujibu wa kanuni na kwa kuwa tayari kamati ilikuwa imependekeza kuundwa kwa kamati ndogo, basi Spika aliona ni vyema jukumu hili likafanyike hukohuko,” alisema Joel na kuongeza:
  “Tayari nimezungumza na Mheshimiwa Zitto kuhusu uamuzi huu wa Spika lakini nitamjulisha kwa barua rasmi na pia Mwenyekiti wa Kamati naye atajulishwa maelekezo hayo ya Spika.”

  Kwa upande wake, Makamba alisema kamati husika tayari imeishapendekezwa kwa Spika, lakini hakuwa tayari kuwataja wajumbe wa kamati hiyo.
  Hata hivyo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba miongoni mwa wajumbe wa Kamati hiyo ndogo waliopendekezwa ni Mbunge wa Simanjiro (CCM) Christopher Ole Sendeka ambaye amejipambanua kuwa miongoni mwa wanasiasa wanaopiga vita ufisadi nchini.
  “Kamati yetu ina uwezo wa kufanya kazi hizi wala sina wasiwasi hata kidogo, lakini sijapata maelekezo ya Spika hivyo siwezi kuingia kwa undani kuhusu jambo hili hadi hapo nitakapokuwa nimepata maelekezo hayo,” alisema Makamba.

  Hoja ya Zitto

  Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) alikuwa ametoa hoja ya kutaka iundwe kamati teule ya Bunge kwa ajili ya kuchunguza ufisadi huo.

  Zitto alitoa taarifa ya mdomo bungeni Julai 13, mwaka huu kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge Namba 117 (2)-(a) inayomruhusu kutoa taarifa ya kusudio lake la kuwasilisha hoja ya kutaka Bunge liunde kamati teule. Julai 15, mbunge huyo alimwandikia Spika Makinda barua kutoa taarifa ya hoja husika.
  “Kuna haja ya kujua uhalali wa ongezeko la Dola milioni 122 zilizoongezeka katika malipo hayo," alisema Zitto katika barua yake kwenda kwa Spika.Alisema kitendo cha kurejesha mkopo huo pamoja na faida ya zaidi ya asilimia 1,000 kinaashiria kuwepo kwa ufisadi wa fedha za umma na ni jambo ambalo haliwezi kuvumilika lipite bila kuwekwa wazi.

  Zitto alielezea kushangazwa kwake na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi kutolifafanua suala hilo kwenye majumuisho ya bajeti yake kwa mwaka 2011/12, hivyo kusema kuwa upo umuhimu wa Bunge kuliweka wazi suala hilo kwa wananchi.

  Fedha hizo zilichukuliwa kupitia kampuni ya Meremeta ambayo iliundwa na Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Afrika Kusini ya Triennex PTY, hivyo kuchukua mkopo huo wa Dola 10 milioni, lakini kiasi kilichorejeshwa baadaye ndicho kinachotia shaka.Zitto alisema katika kurejesha fedha hizo, Serikali iliamuru BoT iilipe Nedbank na ilitekeleza agizo hilo mwaka 2004.

  Meremeta ilikotokea
  Suala la Meremeta ni la muda mrefu na mara nyingi Serikali imekuwa haiko tayari kulizungumzia kwa maelezo kwamba ni suala ambalo lina maslahi ya kiusalama kwa taifa.

  Awali, Serikali ilisema kwamba Meremeta Ltd ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na JWTZ kwa ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Mkoa wa Pwani. Taarifa za usajili zilizotolewa na Msajili wa Makampuni wa Uingereza na Wales zinabainisha kuwa kampuni hiyo iliandikishwa nchini humo mwaka 1997 na baadaye ilifilisiwa huko huko Uingereza mwaka 2006.

  Taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ya Mei 31, 2005 inabainisha kwamba Meremeta Ltd ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania, Oktoba 3, 1997 na kwamba hisa 50 za kampuni hiyo zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini, wakati hisa 50 zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania.

  Utata mkubwa kuhusu umiliki wa Meremeta Ltd unatokana na taarifa ya Brela ambayo pia inazitambua kampuni mbili za Kiingereza ambazo ni London Law Services Ltd na London Law Secretarial Ltd kuwa wamiliki wa hisa moja kila moja ndani ya Meremeta.
  Licha ya Serikali kutokuwa mmiliki pekee wa kampuni hiyo, BoT ililipa madeni yote ya Meremeta badala ya kusaidiana na washirika wake ambao kisheria wanaonekana kuwa walikuwa wakimiliki hisa katika kampuni hiyo.

  Serikali Tanzania ilikuwa ikimiliki asilimia 50 ya hisa na kwa mujibu wa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), uhalali wa malipo hayo ulikuwa na walakini kwani kiutaratibu Nedbank Ltd ilitakiwa iachwe idai fedha zake kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo kama ilivyo kwa wadeni wengine.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Nchi yetu hii bana,ufisadi kila mahali mpaka kwenye familia!
   
 15. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Hii ipo jukwaa la siasa mkuu!!
   
 16. D

  Dudu Baya Member

  #16
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 5
  Ama kweli siku za Magamba zinakaribia ukingoni. "You can fool some people some times, but you can't fool all the people all the time."
   
 17. HT

  HT JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hivi hizi sarakasi mpaka nimechoka kuhesabu. Hii nchi tajiri sana, ila umaskini wa watu wake ni issue tata sana!
  Mungu wetu, tupe macho tuone na kutenda yatupasayo tuokoe ka nchi ketu kazuri ulikotupa.
  Machozi huwa yananilengalenga sometimes.....bah!
   
 18. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Inamaana nchi haina usalama tena, maana ilishawahi kuzungumzwa na Waziri Mkuu Pinda kwamba hawezi kupekenyua issue ya Meremeta kwa sababu za kiusalama. Sasa huo usalama umeisha lini?
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Aug 6, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,494
  Likes Received: 5,724
  Trophy Points: 280
  jammani mnataka kumfunga nini ndugu yangu mboma mbona hivyo sasa hili lifence kubwa na gorofa atamwachia nani..anyway najua porojo hizo wanaishia mahakamani..wakati wanawapeleka watuhumiwa wa ufsadi mahakamani
  ndugu mmoja serikalini akasema akuna kesi nakuhakikishia mpaka kikwete anatoka kesi zinaendelea'...na sasa hili la meremeta naona hadithi za mama na mwana
   
 20. j

  jonasadam Member

  #20
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Swala la meremeta ni jeshi na usalama wa taifa, msituletee balaa! hawa jamaa wakiamua kutoka kama wanaotoka na kunadamana tutaipata! waacheni wenye nchi hayo ni ya kwao!
   
Loading...