Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,587
- 28,749
Kuna kitu bado sijaelewa hapo alipodai kuwa kuna vigezo vitakavyotolewa na mamlaka hiyo vya kuzingatia.Watakuwa wanakata matangazo kuficha madudu ya serikali tu hao.
Kuna kamchezo bunge linataka kucheza hapo, kuficha baadhi ya mijadala na kukata matangazoSasa ndo wanakwepa gharama? Yote ni kuficha tu udhaifu wa Bunge
Aisee hio profile pic yako ni mbeya city au ni chama cha zitto kabwe?inatafutwa njia ya kupiga deal tena
Nape kajisahau.Anaota kuwa bado ni Mwenezi wa ITIKADI za ccm..Kwani yeye ni waziri wa bunge? Mwanini alisemee bunge na wizara anayoihudumu?
Kapewa cheo kikubwa kinamzidi.Nape kajisahau.Anaota kuwa bado ni Mwenezi za ITIKADI wa ccm..
..Kweli kabisa. Hasidi haachi asili...Kapewa cheo kikubwa kinamzidi.
Angerudi chamani tu kule apambane na kina Mnyika
Sijaelewa, kwa hiyo Bunge litakuwa linapata wapi pesa za kugharamia hayo matangazo? Pesa hazitatoka kwenye mfuko wa Serikali?
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina mpango wa kuanzisha kituo chake cha televisheni kurusha matangazo ambapo kitakuwa kikurusha matangazo ya mijadala yake yote LIVE.
Hali hii itaviwezesha vituo vingine kuchukua matangazo kutokea katika kituo hicho ambacho bado hakijafahamika jina lake, tofauti na zamani ambapo walikuwa wakichukua matangazo TBC.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, amesema hayo jijini Mbeya, wakati akizungumza na wadau wa habari, michezo, utamaduni na watendaji wa serikali mikoa ya Mbeya na Songwe.
Amesema kutokana na hatua hiyo Bunge lenyewe ndio limechukua dhamana ya kuanzisha studio yake hivyo kutoa fursa kwa televisheni nyingine kurusha matangazo ya moja kwa moja lakini kulingana na vigezo na masharti yatakayohalalishwa na mamlaka hiyo.
Amesema shirika la utangazaji la Taifa, TBC, lilikuwa linaagizwa kurusha matangazo ya Bunge bila ya malipo ambapo kwa mwaka shirika lilikuwa likitumia bilioni 4 kwa mapato yake ya ndani na kulifanya kushindwa kukarabati mitambo pamoja na mslahi ya watumishi hivyo, uamuzi huo ulikuwa sahihi licha ya wananchi wengi kuonesha kutoridhishwa.
Source: Bunge laanzisha studio kuzipa Tv zote fursa ya kurusha "LIVE" vikao vya mikutano - wavuti
Mzee Kimmbunga, uko Dodoma?......Sijaelewa, kwa hiyo Bunge litakuwa linapata wapi pesa za kugharamia hayo matangazo? Pesa hazitatoka kwenye mfuko wa Serikali?
Kuna nini tena huko Dodoma mkuu? Mimi nipo kisiwani Lyakanyasi najitafutia riziki ndani ya Ziwa Nyanza/Victoria.Mzee Kimmbunga, uko Dodoma?......
....Ok. Dodoma kuna Studio mpya za Bunge zinajengwa. Nilikuwa natania tu ndugu yangu. Yaani, inabidi tuelekee huko kunako studio za Bunge...Nakutakia Uvuvi mwema. Nikipita kuelekea Rubondo huenda nikapita Nyakanyasi kukusabakhi..Kuna nini tena huko Dodoma mkuu? Mimi nipo kisiwani Lyakanyasi najitafutia riziki ndani ya Ziwa Nyanza/Victoria.