Bunge kuamua kubambana?

Liberal

Member
Jan 29, 2012
35
5
Kwa mwenendo wa utendaji wa serikali sasa unavyondelea hasa kwenye sekta ya fedha, haki za binadamu na demokrasia, ni wazi baada ya miaka michache pengine watanzania walio wengi watakuwa wamerudi miaka 50 nyuma za maendeleo kwenye sekta tajwa. Ni bunge letu ndio lenye meno ya kutukwambua.

Kwa bajeti inayoisha 2016/17, fedha ya amendeleo iliyotoka pengine inaweza kuwa chini ya 40% kwa takwimu na hii imepelekea ugumu wa maisha na kuvunjika kwa mitaji ya wafanyabishara wengi. Bunge letu lina kila sababu ya kuiwajibisha serikali.

Itakumbukwa kuwa, hivi majuzi kuna kauli kutoka kwa kiongozi mkubwa akilionya bunge endapo litaamua kuchuka hatua ya kumwajibisha PM juu ya serikali kushindwa kuwakwamua wananchi kwenye umaskini uliokithiri, Je, wabunge wataamua kuendana na maonyo hayo au wataamua kuanza kujifunza kuamua?

Dalili za wazi kabisa zinaonesha kuwa, wabunge wengi, hasa wa CCM hawatakubali kuzibwa midomo. Composition ya Bunge la sasa ni ngumu kwa spika endapo ataamua kuendeleza status quo.

Migogoro ya kisiasa ndani CCM itakuwa chachu kubwa ya kila mbunge kujitetea na pengine kupambana na CCM ya Polepole "kwa hoja"

Tunategemea kupata bunge zuri sio lile lililonyimwa meno tangu awali, kwa sababu tayari kwa mambo jinsi yanavyokwenda, bunge hilo hilo limepewa meno automatically!
 
Acha iwe hivyo kwa sasa. Rais huyu wa sasa ndo atakayeirahisishia CCM kuondoka madarakani na kwenda kuwa chama cha upinzani. Tatizo la huyu kinara ni kutozingatia utawala wa sheria. Bunge limeidhinisha kiasi cha fedha ziende kwenye miradi ya kilimo cha mpunga wilayani Kilombero, yeye anaamuru kiasi hicho kisipelekwe huko Kilombero na badala yake kipelekwe kwenye ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato. Tutafika?
 
Back
Top Bottom