Mwene chungu
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 915
- 754
Nimekaa nawaza na kuona matukio haya mawili la clouds tv kuvamiwa kwa bunduki tena zaidi ya moja,na la leo Nape Nnauye kutishiwa bastola ili hali hakukuwa ulazima kabisa wa kutoa bastola hio.
Kifupi linaweza kuonekana tukio la kawaida kwa sababu TU MATUKIO HAYA YOTE MAWILI HAYAJAMWAGA DAMU.
lakini huu ni mwanzo wa dalili sizizokuwa nzuri kabisa,inawezekana tunakoenda maaskari wetu watakuwa wanaua tu watu bila sababu.
Wapo wadau mbalimbali wanaotakiwa kulikemea swala hili kabla halijaanza kuleta madhara...
Najua huwa Watanzania tunasubiri hadi maafa yatokee ndio tuanze kusema...
Lakini binafsi pamoja na kutomkubali Nape,lakini sio kwa kiwango cha kumtishia bunduki,kama nape angejarbu kufanya fujo pia pengine tungekuwa tunaongea mengine sasa.
Askari wetu bila bunduki huwa hawana namna nyingine ya kujitambulisha?.
Rais na wadau wa usalama kama siraha zimekosa kazi nendeni huko somalia mkapambane na AL-SHABAAB sisi Tanzania tumezoea Amani.