Bunduki ya kivita yakamatwa Tabora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunduki ya kivita yakamatwa Tabora

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 21, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  JESHI la Polisi mkoani hapa, limekamata bunduki ya kivita katika mji mdogo wa Kaliua iliyokuwa ikitumiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow, amesema, silaha hiyo ya kivita ilikamatwa Kaliua, wilayani Urambo.

  Amesema, Polisi wa doria, walikuta vijana tisa, wakijiandaa kufanya uhalifu Kaliua.

  Polisi walipofika eneo la uwanja wa michezo wa Kaliua, walikuta vijana hao tisa waliokuwa wamevalia makoti marefu, wamepumzika wakijiandaa kufanya uvamizi na uporaji.

  Hata hivyo, baada ya kuona askari, vijana hao walikimbia na hivyo kuacha bunduki aina ya SMG na risasi 30 kwenye magazini yake, ambapo askari Polisi waliwakimbiza na kupiga risasi angani lakini hakuna aliyekamatwa.

  Amesema, hata hivyo usiku huo askari hawakuiona ila waliporudi kukagua eneo la tukio asubuhi wakaikuta imetelekezwa kwenye majani.

  Amesema, bunduki hiyo namba CT 18731998 licha ya kuonekana ni chakavu, lakini imekuwa ikitunzwa na inafanya vizuri katika utendaji wake, kwa kuwa ipo salama kiufundi.

  Amesema, eneo la Kaliua, limekuwa likisumbua kwa matukio ya ujambazi kutokana na kuwa na misitu mingi na katika baadhi ya maeneo hakuna mtandao wa simu, kitu ambacho kimewafanya majambazi kujichimbia zaidi katika maeneo kama hayo.

  Hata hivyo, amesema Polisi imekuwa ikitegemea sana dhana ya Polisi Jamii ambayo imesaidia kupunguza uhalifu na kwamba Jeshi hilo litaendelea kutumia mbinu mbali mbali hadi litakapofanikiwa kukomesha ujambazi.

  HabariLeo | Bunduki ya kivita yakamatwa Tabora
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  walishindwa kufanya kama arusha
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ujambazi sijui utaisha lini bongo maana kila kukicha unaongezeka tena wa siraha
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Du ! siku ikikamatwa bunduki ya amani sijui itakuwaje?
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hiyo kitu haitakuja tokea tena sababu siku zinaenda na amani inapotea!
   
 6. c

  chetuntu R I P

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mmh, Tabora! Watakuwa wa nchi jirani tu wanazo kama njugu.
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Publicity hungry police officers, SMG moja iliyookotwa unaipamba hoo bunduki ya kivita.

  Naona kukamata bunduki moja ni kitu kigodo sana hakukuwa na haja ya kuita press conference kuelezea kuokota bunduki.
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  man mafanikio hayo kama wezi walikimbia!!!nadhani ni busara kwa polisi kuutangazia umma kwa kila mara waonapo ugumu wa kazi na mafanikio kinachotuboha ni kuonea raia wasio na hatia hapo ndipo tunapoona jeshi linapotoka kabisa!so penye mazuri tupongeze!
   
Loading...