Bundi kulia usiku ina maana gani?

Bundi kulia usiku ina maana gani?

Rocky City

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2017
Posts
982
Reaction score
749
Jamani eti Bundi kulia usiku mlio fulani hivi nini kinaashilia? Maana nimeambiwa eti ni mikosi, lakini kambi hapa ninapokaa kuna miti miti mingi sana na Bundi wapo wengi sana

Lakini usiku wanapokuwa wanaluka wanatoa sauti fulani hivi ambayo nimesikia ni uchuro.

mshana jr saidia hili..
 
Ni ushirikina tu hakuna ushahidi wowote wa kwamba kuna uhusiano wa bundi kulia na mikosi.

Ila kama unaamua kuishi kwa woga, unaruhusiwa kuogopa hata kivuli chako mwenyewe.
 
Mkuu ni hatal sana mana ukisikia story za mtaa unaweza kukimbia kambi
Story za mtaa haziishi, mtu anaweza kukujaza ujinga ukimbie kambi ili akae yeye.

Za kuambiwa changanya na zako.

Kuna vibabu vilikuwa vime specialize katika saikolojia hiyo kuitoa maishani kwa kutisha watu tangu enzi za kabla ya ukoloni, unafikiri uongo mrefu kamahuo unaweza kuisha mara moja?
 
Hiyo ni democrasia yao
Kama nyie mnavyoamka asubuhi na kuongea siku nzima ,
Na wao wanaamka jioni na kuongea usiku mzima.

Waacheni bundi na maisha yao.
 
Mkuu hakuna kitu kama hicho. Bundi ni kiumbe kama tulivyo sisi, atalia, ataimba nk, Mapokeo yasiyo ya kitafiti toka kwa mababu yamelazimisha kutukaririsha ujinga. Na hii ni kwakuwa mwafrika anakiogopa sana kifo. Vinginevyo Bundi yuko poa, hasa kama wewe umemfuata kwenye makazi yako porini.
e1284f1b33d1707c522550274ed461da.jpg
 
1. Bundi ni "NOCTURNAL ANIMAL" yaani wanyama wanaofanya shughuli zao usiku. Haimanishi kuwa wanaona usiku ila wanatumia sense nyingine kama sauti na harufu

2.Lengo la kuwa active wakati wa usiku na kupumzika wakati wa mchana ni kwa ajili ya kuepuka mapambano ya kugombania chakula na huduma nyingine ambazo kuna baadhi ya wanyama wanakula hivyo hivyo sasa wanapotoka usiku wale wapinzani wao huwa wamelala na kupata chakula kiurahisi.

3. Kama ilivyo kwa wanyama wengine katika mihangaiko yao ya kawaida hutoa sauti kama ishara ya mawasiliano baina yao, kama kumuita mwenzake, kumfukuza, kutongoza, kuogopa ama kumgombeza adui au mwenzake

4. Hivyo sauti unazoziskia usiku za bundi ni sauti za kawaida zenye malengo kama niliyoeleza hapo juu na hazilengi kwa vyovyote kumtisha binaadamu na wala hawana shida yoyote na binaadamu na wanawapenda sana binaadamu ndio maana hupenda kuishi walipo karibu binaadamu ili awalinde
 
Bundi ni ndege kama kuku na njiwa sisi huku kijijini kwetu tunawala sana tu!
 
Jamani eti Bundi kulia usiku mlio fulani hivi nini kinaashilia? Maana nimeambiwa eti ni mikosi, lakini kambi hapa ninapokaa kuna miti miti mingi sana na Bundi wapo wengi sana

Lakini usiku wanapokuwa wanaluka wanatoa sauti fulani hivi ambayo nimesikia ni uchuro.

mshana jr saidia hili..
Ukweli ni kwamba, kuna bundi wa aina mbili. Wapo wa Kichawi na wapo wa kawaida (ambao siyo wa kichawi).

Hawa wakawaida huwaga wanataga mayai mengi kama kuku na kwamba wao ni kama ndege wengine kwani hawana shida yoyote ingawa Sauti yao ni sawa tu na wale wanaotumika na wachawi.

In a nutshell ni hivo Mkuu...

Wale wa kichawi, kwanza ukimwona live anasura kama ya binadamu (anatisha na kuogofya pia). Wao hutaga mayai 2 tu. Inasemekana kwamba mayai, kiota na mamyoya yake ni baadhi ya Mali ghafi zinazotumika na wanachawi ktk mambo mbalimbali.
 
Hapa ndipo kabosa nazidi kuogopa..mana hapa tunapokaa kuna bundi wengi sna ni kambini..na hao bundi hata viota vyao tumeviuwa sna mayai yao mawili tu tumeyatupa sna na ni kweli ni ma 2 tu..na mm nimewauwa sana..sasa hapo mkuu ndio vp tena..mwaka wa 4 sasa na bado tunaendelea kuwauwa tu wakionekana mana mazingira ya hapa kuna miti mingi na magofu mengi pia..
 
1. Bundi ni "NOCTURNAL ANIMAL" yaani wanyama wanaofanya shughuli zao usiku. Haimanishi kuwa wanaona usiku ila wanatumia sense nyingine kama sauti na harufu

2.Lengo la kuwa active wakati wa usiku na kupumzika wakati wa mchana ni kwa ajili ya kuepuka mapambano ya kugombania chakula na huduma nyingine ambazo kuna baadhi ya wanyama wanakula hivyo hivyo sasa wanapotoka usiku wale wapinzani wao huwa wamelala na kupata chakula kiurahisi.

3. Kama ilivyo kwa wanyama wengine katika mihangaiko yao ya kawaida hutoa sauti kama ishara ya mawasiliano baina yao, kama kumuita mwenzake, kumfukuza, kutongoza, kuogopa ama kumgombeza adui au mwenzake

4. Hivyo sauti unazoziskia usiku za bundi ni sauti za kawaida zenye malengo kama niliyoeleza hapo juu na hazilengi kwa vyovyote kumtisha binaadamu na wala hawana shida yoyote na binaadamu na wanawapenda sana binaadamu ndio maana hupenda kuishi walipo karibu binaadamu ili awalinde
Sawa mkuu..
 
Back
Top Bottom