Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,901
- 20,410
Wadau, amani iwe kwenu.
Dirisha la usajili kwa Timu ya Umoja ni Ushindi limefungwa rasmi Julai 19. Kama ilivyotabiriwa na kama ilivyotokea kwenye nafasi ya Urais, kumekuwa na wimbi kubwa la watu kujitokeza kuomba nafasi ya ubunge kwa tiketi ya CCM. Napenda kukiri kwamba haijapata kutokea watu wamekuwa huru zaidi kujitokeza kugombea mwaka huu tofauti na chaguzi zilizotangulia.
Pamoja na uhuru huo, wapo watu ambao walikuwa mguu ndani mguu nje kwenye Timu ya Umoja ni Ushindi. Baada ya jimbo la Bunda kugawanywa, na kuwa Bunda Mjini na Bunda vijijini, Stephen Wassira amechukua fomu kugombea jimbo la Bunda Mjini ambako anaamini ataibuka mshindi.
Ikumbukwe kwamba Esther Bulaya ambaye alikuwa mbunge kwa tiketi ya CCM akiwakilisha vijana, alitegemea kugombea jimbo hilo. Ijapokuwa alishauriwa kuwa akagombee jimbo la Bunda vijijini, yeye hakuwa tayari kupokea ushauri huo na badala yake akaamua kususa na kutangaza kuhama chama.
James Lembeli, mbunge wa Kahama Mjini, hakuchukua fomu kutetea jimbo lake na badala yake alitangaza kujitoa CCM na kujiunga na CHADEMA. Kujitoa kwa Lembeli kumetokana na mbunge huyo kupoteza ushawishi ndani ya jimbo lake na hivyo kuibuka washindani wake kama mfanyabiashara maarufu wa Jijini Mwanza, Kishimba ambao kimsingi Lembeli alijikuta hana chake Kahama. Hivyo, kitendo cha kwenda CHADEMA ambako wapo tayari kupokea makapi ya CCM kinatafsiriwa kama kuhuisha ushawishi wake uliopotea.
John Magale Shibuda, Mbunge wa Maswa Magharibi ambaye alikuwa mbunge wa CCM kabla ya kwenda CHADEMA ameamua kugombea tena jimbo lake safari hii si kwa tiketi ya CHADEMA tena ama kurejea CCM kama alivyofanya Said Arfi, bali akiwakilisha chama kidogo sana cha TADEA ambako ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.
Nimetafakari sana hatima ya wanasiasa hawa kwenye uchaguzi ujao hakika naona kuna giza totoro mbele yao. Kwanza kabisa, Lembeli na Bulaya wanatangaza kujiunga na CHADEMA katika kipindi ambacho chama hicho kinaelekea ukingoni kupata wagombea wao ambao wanaenda kushiriki uchaguzi huo kupitia UKAWA. Timing imekuwa tatizo kwao. Nafahamu kuwa yapo makubaliano waliyofikia baina ya wabunge hao na viongozi wa CHADEMA. Ila kimsingi ni kwamba kuna ulaghai umefanyika ambao kwa hakika hautakuwa na manufaa kwa wabunge hao. Nawasikitikia na nawahurumia sana.
Pili, wabunge hao wa kutoka kanda ya Ziwa wanajiunga na upinzani kipindi ambacho wafuasi wengi mamia kwa maelfu wanahama vyama hivyo na kujiunga na CCM. Hakika uteuzi wa CCM kwa John Pombe Magufuli umerejesha ari ya wananchi wa kanda ya Ziwa kuipenda CCM. Wananchi wa Kanda ya Ziwa wamejifunza kwa wenzao wa Kaskazini.
Kwamba kitendo cha wananchi wa Kaskazini wakichoma moto kadi za CCM kutokana na "mtu wao" Lowasa kukatwa mkato mkubwa kimewafanya wajitafskari upya na hivyo wale wa upinzani wa kanda ya ZIWA wameamua kushikamana na Mgombea wa CCM, Magufuli kwani kitendo tu cha kuteuliwa kwake kimewajengea heshima kubwa.
Kutokana na hali hiyo, kipindi cha muda mfupi tu tangu Magufuli ateuliwe kupeperusha bendera ya CCM, Chama hicho kimevuna wanachama wengi wa upinzani na hasa CHADEMA katika mikoa ya Shinyanga, Geita, Simiyu, Mwanza na hata Kagera. Kundi hili ni mbali na lile lililorejea CCM wakati wa ziara za Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana. Hivyo, wakati CHADEMA wakijisifu kumpokea Lembeli na Bulaya, CCM inaendelea kuvuna maelfu na malaki ya wafuasi wa CHADEMA ambao ndio wapiga kura.
Kutokana na hali hii, ni wazi kwamba hata kama CHADEMA itafanya maamuzi ya kuwasimamisha Bulaya na Lembeli kwenye majimbo ya Bunda Mjini na Shinyanga Mjini, naamini kuwa hawatafanikiwa kwa vile Magufuli amekuwa ndiyo habari ya Mujini Kanda ya Ziwa.
Tatu, CHADEMA walitangaza kuwa hawatapokea na kuwasimamisha kugombea makapi ya CCM. Kutokana na kauli hiyo, ni wazi kuwa Lembeli na Bulaya wamekalia kuti kavu.
Nne, vyama vya upinzani kwa sasa vipo kwenye mvurugano mkubwa sana katika mambo kadhaa. Kwanza, mpaka sasa hawajakubaliana namna ya kushirikiana kwenye umoja wao wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi. Hali hii inawafanya waogopane na kushukiana.
Pili ujio wa Lowasa. Lowasa anatakiwa na vyama vyote vya upinzani ambavyo wakati akiwa CCM walisimama kidete kueleza machafu yake kubwa zaidi likiwa ni kashfa za ufisadi. Lowasa yule yule fisadi ndiye huyo huyo anayewindwa na upinzani.
Lowasa amekuwa kama ganda la muwa la jana. Ndani ya CHADEMA, kundi linaloongozwa na Katibu Mkuu halimtaki Lowasa huku kundi la Mwenyekiti likisukumwa na tamaa ya fedha likiona kuwa Lowasa ni mtaji wao kisiasa. Kwa hali hii, wafuasi wengi wa chama hicho wanaochukizwa na ufisadi wamepoteza matumaini na chama hicho ambacho kilikuwa kinajipambanua kuwa ni kiboko ya mafisadi.
Kwa upande wa Shibuda, huyu namhurumia sana. Natambua kuwa yeye anabebwa zaidi na sifa zake na si chama. Hata hivyo ni vyema angesoma alama za nyakati. Kama political analyst, naamini kuwa Shibuda atakuwa kwenye political risk sana kwenye uchaguzi wa mwaka huu kuliko chaguzi zilizopita. Wana Kanda ya Ziwa wana imani na CCM na kwamba wapinzani na hasa CHADEMA hawana cha kuwashawishi wananchi wengi wawapigie kura. Hivyo ijapokuwa Shibuda anabebwa na sifa zake, ila kwa uchaguzi wa mwaka huu sifa hizo hazitamsaidia mbele ya Tingatinga.
Wadau, kutokana na hali hii, ni dhahiri kwamba Shibuda, Lembeli na Bulaya kwa msemo wa sasa ni kwamba wameingia choo cha kike.