BUKOMBE, GEITA: Mtoto wa miaka 7 ajinyonga kwa kamba

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mtoto George Elias (7) amekutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kamba ya katani katika Kijiji cha Buganzu, Kata ya Uyovu wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita, tukio linalodaiwa kusababishwa na michezo ya kitoto.

Baba wa mtoto huyo, Elias Martin alisema mwanawe alikuwa anasoma darasa la awali katika shule ya msingi ya kijiji hicho na siku ya tukio alikwenda kucheza na watoto wenzake.

Martin alisema akiwa nyumbani kwake akipata chakula cha mchana na wageni waliokwenda kumtembelea, walifika watoto watatu wa jirani yake wakidai mtoto wake ananing’inia juu ya mti.

Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo aliambatana na wageni wake mpaka eneo la tukio na kumkuta mtoto huyo akining’inia kwenye mti uliopo pembeni ya nyumba yake.

Mzazi huyo alisema chanzo cha tukio hilo ni michezo ya watoto na huenda alidanganywa na wenzake kuweka shingo kwenye kamba walipokuwa wakicheza.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Matayo Paschal alisema kuwa alipokea taarifa ya kifo hicho na kulijulisha Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Mpojoli Mwabulambo alisema wamefungua jalada la uchunguzi kuhusu tukio hilo, lengo likiwa kujua chanzo cha kifo hicho.
 
Hii ilitokeaga miaka ya 95 kule mabibo ya Mandela road. Dogo alikuwa anamuiga commando Lambo, lakini bahati mbaya hakufanikiwa
 
Mambo mengine yanafuata mkondo wa damu na matukio yaliyopita tokea kwa vizazi vya nyuma.

Mambo mengine, yanawekwa na binadamu wenzetu, kukomoana na huo ni ushirikina haswa.

Wajuzi wa mambo haya watasaidia sana kutuelewesha hayo juu.

Pole kwa familia fiwa.

Cc Mshana Jr, Jichawi, & Wajuzi wa Dini wengine wote mlio humu.

Ahsante!
 
Kumlinda mtoto ama familia yako, ni maombi thabiti pekee, ndiyo yatafaa. Yaani tuwe Ki-Roho zaidi.

Roho Mtakatifu na siyo yule aitwaye roho mkatakisu.

Ahsante!
 
Kwa hiyo wewe unafikiria Roho Mtakatifu siyo Roho Mtakakisu? Katika Magic Ceremonies,wachawi wananunua kisu,na aina ya kisu lazima iwe 'kisu kizuri ambacho kinaweza kumuondoa mtoto shingo kwa pigo moja',halafu zinafuata sala nyingi sana ambapo Malaika Gabriel na malaika wengine wengi wanaombwa kukibariki kisu 'kitusaidie katika shughuli zetu', 'kitusaidie kujilinda'.
 
Kumbe wachawi nao wanamwomba Malaika Gabriel..sikujua.
 
Kwa hiyo wewe unafikiria Roho Mtakatifu siyo Roho Mtakakisu? Katika Magic Ceremonies,wachawi wananunua kisu,na aina ya kisu lazima iwe 'kisu kizuri ambacho kinaweza kumuondoa mtoto shingo kwa pigo moja',halafu zinafuata sala nyingi sana ambapo Malaika Gabriel na malaika wengine wengi wanaombwa kukibariki kisu 'kitusaidie katika shughuli zetu', 'kitusaidie kujilinda'.
What is this? How dare you post such a thing? Jamani tuache kufuru tusijejikuta mahali ambapi hatukutegemea.
 
Back
Top Bottom