Hawa nshomile wanajidai tu hamna lolote bukoba.sikuamini macho yangu nilipofika bukoba na kujionea.mjini bkb ovyo ovyo.pamoja na yote hawana customer care nzuri.jengo ni moja tu la nssf.bkb ovyooo waone hivyo hivyo na makeke yao huku mjini.wenzao wachaga wamekamata kila mji hapa tz na kwao usiseme wako juu mbaya.nawafagilia sana chagas.bigup sana.kama skul wamo,bizinez namba moja.haya mapompus kibao mjini
do not judge a book by its cover mkuu.Mkoa wa Kagera una matatizo lukuki sasa wewe umeongelea mjini tu lakini hata mjini mtatatizo mengi.
Mf.sokoni kuchafu saana kwani takataka zinamaliza siku kibao bila kuondolewa.
Mji wa Bk hauna barabara ata moja yenye miti na maua,nyumba nyingi ni za zamani hazifanyiwi ukarabati ata kupaka rangi hamna,bei ya vitu hiko juu kuliko sehemu nyingine mfano mafuta,sukari etc
Rushwa nikama halali hasa maaskari polisi na traffic,vijana wengi hawana kazi maarum,elimu ndo usiseme shule za kata nyingi hazina walimu na vyumba vya maadarasa mf.wanafunzi wakidato cha kwanza wengi wataenda shule mwezi wa nne baada ya january.
Mkuu hii kasumba ya kujisifia hakina nshomire haina nafasi tena wakati matatizo ni chungu nzima.
Nimejifunza hivi: ukomavu wa fikra ni kukubali kukosolewa na kutojikweza. Nimezaliwa Bukoba na kukulia hapo, nimeishi nje ya Bukoba tangu sept 11(nakumbuka sana siku hiyo kutokana na kulipuliwa kwa WTC).
Dini(baadhi ya vijiji vimegeuka Jaralabad au Kano) Siasa za majitaka na visasi,wizi,n.k vimeiharibu kila kitu Bukoba....watu wamechagua kuwa wavivu,ebu jiulize gari dogo toyota cololla linabeba abiria kwenda Izimbya,tena trip moja kwa siku,huo ndio ubunifu tuliobakiza.
Katikati ya mji mdogo wa Bukoba mfanya biashara wa duka anauza kreti moja ya soda kwa wiki moja!Mji mchafuu,wenyeji wavivu kila siku Kagasheki,Lwakatale,sisi waziba wao wanyaihangiro,ptuuu! Nakumbuka wimbo wa Kakau Band...Kagera yaitu yagera...ebya nshomile byatweshara!
kaka ulibahatika kulala kwenye lodge moja imetulia sana kwa magentle me inaitwa CMK LODGE karibu na walkguarg ya hapa linas?
seriously, kwa wale wanaoujua mji wa BKB vizuri wangetujulisha on business opportunities zilizopo huko. Maana nasikia opportunities bado ni nyingi sana uko, ila wengine hatuzijui, naimagine hata kwenye kilimo maana ardhi kule ina rutuba sana.
also vipi kuhusu swala la vivutio vya utalii
wekeza kwenye kilimo mkuu,ardhi yenye rutuba,mvua za kutosha,vyanzo vya maji vya uhakika n.k
TAHADHARI:
Nguvu kazi hakuna:vijana wengi wenye nguvu wamekimbilia mjini(waendesha pikipiki),wengi wa wahaya tuna nature ya 'vandalism'..katoto ka std II kanaweza kuvuna mananasi mabichi kwenye shamba la mtu na wazazi wasiseme kitu,hata watu wazima nao ni hivyo hivyo. Jitahidi kuwa na mwanasheria wako, kule hata bibi kizee anataka kesi ya kugombea cm 150 za ardhi ifike mahakama kuu.
yeye kaandika alipoona yeye sasa kama na wewe una yako si useme bila kulaumu mtu
eeehhhh umetokea wapi weye unakuja andika point zako na kumsema kwani kakosea nini kaongea alivyoona yeye wewe sema ulivyoona wewe kwa umekataliwa?
sasa mambo ya kumkosoa mtu ndio ujinga kwa kweli andika point zako songa mbele
kumbuka vidole cyote sio sawa, yaani mizunguko yake sio sawa na weye. OK?