Bukoba ya leo (2)

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,958
7,512
Ni mwendelezo wa nilichokiona na katika hatua hii ya mwisho ntajaribu kuongea juu ya mambo yafuatayo

Huduma za jamii,shule za kata ni nyingi matatzo ya shule hzi ni yaleyale ya siku zote ila kuna haja ya kuanzisha vyuo vikuu pale ili kuinua elimu na kurahisha mambo mengine yanayotokana na uwepo wa vyuo vikuu,maji ya bomba kuna upatikanaji wa kuridhisha kdogo japokuwa sehemu nyingi bado wanategemea maji ya asili kutoka mitoni,umeme kdogo naona umeendelea kupatikana japo kuna sehemu kubwa pia bado wanakosa huduma hii muhimu,kuna udhibiti wa sheria za barabarani na katika hili matrafiki wa kule wanaendelea kukamata sana na kuchukua pesa,nawapongeza kwani tofauti na sehemu zingine abiria wa pikipiki sharti nae anakuwa na kofia yake ya kuvaa kichwani,vyakula viko chini sana na bidhaa za dukani kama sukari zinapatikana japo kwa bei ya juu kama kwingineko

Mazingira na usafi,mjini bukoba mji ni msafi kiasi na hii nimeishuhudia askari wakisimamia usafi na kila mtu aliposimama hata mpita njia sharti uokote takataka pembeni mwako,majengo mengi ni ya zamani ambayo panahitajika mengine ya kisasa kama ghorofa,kwa kilimo na kuishi pako sana ukizingatia hata ile mito ya zamani mingi bado inatiririka

Usafiri,kuna usafiri kuanzia baiskeli,pikpk na daladala ambazo zinatoa huduma walau kwa kiwango flani fresh,kuna mabus ya mikoani na mazuri kiasi chake na hata nchi jirani

My take;Niseme wazi kwamba kuna miaka kama 5 imepita mkoa ukiwa immovable kitu ambacho kimeleta uchumi wa mkoa kushuka,hii inatokana na ukweli kuwa mkoa wetu unakosa viongozi dhabiti wenye kutambua maana ya uongozi kwamba badala ya kuwaleta wanamkoa wote kuongelea maendeleo ya mkoa wao wao wamekuwa makuhadi wa unyambo,uyoza,unyayangilo,uangaza n.k,hapa tulipo hatuhtaji viongozi wa hv wanaoshindwa kuonesha njia na dira kwani kila mmoja anafanya kwake tu kama nilvyoona mbunge mmoja kaanzisha shule yake,sawa lakni kwanini usipiganie kuwepo kwa shule za umma nyingi na kutafuta jinsi ya kuzihudumia,wananchi wanahtaji vya kwao sio vya kwako...kazi kwetu
 
Rweyemamu ensenene ozisigile otai

Mkuu i salute you!senene kusema kweli ni wengi bukoba mjini ambako kuna taa zinazowavuta wale senene kwa wingi tofauti na vijijini ambako wao wanaishia kuokoteza tu kama si kuzisikia maeneo na maeneo

ila pia nilishangaa ile asubuhi kwenye mabasi badala ya kuona vitu kama chai,vocha,maji n.k kwa ajiri ya kuweka breakfast wananchi wakawa busy na kuuza mifuko ya senene,kila mtu anauza senene
 
Polisi wa usalama barabarani wanaongoza kwa kupokea rushwa.Vipi mkuu kuhusu viwanda vya BUKOP,TANICA NA TTA MARUKU ,maana viwanda hivi vinatoa ajira ndogo sana kuliko zamani.
Wabunge wengi wa CCM mkoani Kagera wana mashule zaidi ya moja nalakushangaza mfano Rweikiza Jason Mb Bk vijijini iliwaada wananchi kuwa shule yake itapokea wanafunzi ata ambao wanatoka kwenye familia au kaya zisizo nauwezo basi wakampa kula lakini hadi leo hakuna kaya maskini ambayo ina mtoto anayesoma pale.
 
Bukoba tatizo lao ni ubaguzi,ni wabaguzi sana hawa jamaa,hata wao wenyewe wanabaguana licha ya kuwa asilimia kubwa hawana kitu zaidi ya misifa.Hawataki na wala hawapendi kuona watu wa mikoa mingine wakiwa Bukoba.Miji yote duniani imeendelezwa na wageni sasa kama hawa jamaa wanakataa wageni wataendeleaje aisee?Halafu kilugha kila mahali hadi kanisani na maofisini ni kihaya tu!
 
Mkuu kuhusu shule hizi za mabwana wakubwa kusema kweli zinaninyima maana halisi ya shule,kwann?hivi mie nikifungua shule nikaipa registration ile shule inakuwa mali ya nani?na hyo ni biashara ambayo mwisho wa siku ni faida yangu...kuna ugumu gani ukaweka shule alafu ikamilikiwa na umma hata kama baadae ukifa ile shule ikabaki ni shule ya umma?hawa ndo viongozi wa Kagera ambao kimsingi ni mkosi na kikwazo katika maendeleo,hivi imagine huyu ataconcentrate wapi na atadeconcentrate wapi katika kuhudumia za kwake ama za umma?

Tunahitaji kureview siasa zetu na kuchallenge idea za hivi,maendeleo asifanye yeye,yeye anatakiwa awaoneshe watu njia yao,wajenge shule zao kwa nguvu zao kwa ajiri ya watoto wao,haya sasa hyo ya Rwegasira ni nani wa kuiongelea,ni mtoto gani ambaye mzazi wake ni maskini anasoma pale?
 
si nilisikia wale wamiliki wa AMAN shule ya msingi na peace secondary wanataka kuanzisha chuo? Alafu trafic wa huko ni wala rushwa ile mbaya..alafu ata daladala hailiruhusiwi watu kusimama kama miji mingine.
 
Bukoba tatizo lao ni ubaguzi,ni wabaguzi sana hawa jamaa,hata wao wenyewe wanabaguana licha ya kuwa asilimia kubwa hawana kitu zaidi ya misifa.Hawataki na wala hawapendi kuona watu wa mikoa mingine wakiwa Bukoba.Miji yote duniani imeendelezwa na wageni sasa kama hawa jamaa wanakataa wageni wataendeleaje aisee?Halafu kilugha kila mahali hadi kanisani na maofisini ni kihaya tu!

Mkuu unaongelea watu wakati mie naongelea vitu,umeona wapi nafanya descriptions na behaviours za watu ama ndo unataka tuamini kwamba unafikiria too emotionally?

Hawa watu kuongea kihaya hadi ofisini ni jambo la kihistoria ambalo ukitaka utapatiwa kwanini make huko haikuwepo wala kiswahili ila ilikuwa kihaya mpaka makanisani,mpaka vitabu,mpaka kalenda n.k hata leo vpo, kwanini?uliza utaambiwa pia

Jaribu kutafiti ama huliza kwanini mpaka leo waganda wanatumia kiganda sana kuliko kiswahili na kizungu?soma historia kuliko kuja hapa unalaumu..alafu ni wapi ulikaa ukafukuzwa?mbona hausemi? ila wale watu wako conscious sana na ardhi sasa kama ulienda ukachezea ardhi yao watch out kaka,wanalinda vitu vyao sana tofauti na kwingine unakoona mtu anajenga tu,analima tu anapopapenda,kule hicho kitu hakuna,soma sana historia itakusaidia kujua vizuri mambo ya dunia hii
 
mkuu i salute you!senene kusema kweli ni wengi bukoba mjini ambako kuna taa zinazowavuta wale senene kwa wingi tofauti na vijijini ambako wao wanaishia kuokoteza tu kama si kuzisikia maeneo na maeneo

ila pia nilishangaa ile asubuhi kwenye mabasi badala ya kuona vitu kama chai,vocha,maji n.k kwa ajiri ya kuweka breakfast wananchi wakawa busy na kuuza mifuko ya senene,kila mtu anauza senene

2 points of collection.

1. Bakubaza omukihaya oholole omukihaya.
2. Aha bihandiko ebi kutukutula olekele ebishuba, ogambe amazima, buli muntu naguza ensenene????????! Watujangula rugamu.
 
Bukoba tatizo lao ni ubaguzi,ni wabaguzi sana hawa jamaa,hata wao wenyewe wanabaguana licha ya kuwa asilimia kubwa hawana kitu zaidi ya misifa.Hawataki na wala hawapendi kuona watu wa mikoa mingine wakiwa Bukoba.Miji yote duniani imeendelezwa na wageni sasa kama hawa jamaa wanakataa wageni wataendeleaje aisee?Halafu kilugha kila mahali hadi kanisani na maofisini ni kihaya tu!

Unachoongea sina uhakika kama ulikifanyia utafiti; na inadhihirisha ni jinsi gani wewe ujatembelea mikoa
mingine zaidi ya Dar: ni wachaga, wahindi, wakurya, na wasukuma wangapi wako Bukoba? au unataka makabila yote tanzania yahamie Bukoba??, nenda sehemu kama Njombe(kwa wakinga na wabena), Shinyanga(kwa wasukuma) uone kiwango cha matumizi ya kilugha chao. Unashauriwa siku nyingine usiwe mwepesi wa kuandika kitu ambacho ujui undani wake , jaribu kuwa unaomba ushauri kwa wanaojua, au kama una visa na watu wa Bukoba sema walichokukosea.
 
2 points of collection.

1. Bakubaza omukihaya oholole omukihaya.
2. Aha bihandiko ebi kutukutula olekele ebishuba, ogambe amazima, buli muntu naguza ensenene????????! Watujangula rugamu.

Bakanyegesa okuhulila waitu mara onganyile eitatzo aba aboikubona mbatujuma aho aluguru mbaleba okosee bagambe bati twaba bakabila,nomanya mbatutamwa mno toubona okwo bazimbisize amatama si?

Omukama abele naiwe!
 
Bukoba tatizo lao ni ubaguzi,ni wabaguzi sana hawa jamaa,hata wao wenyewe wanabaguana licha ya kuwa asilimia kubwa hawana kitu zaidi ya misifa.Hawataki na wala hawapendi kuona watu wa mikoa mingine wakiwa Bukoba.Miji yote duniani imeendelezwa na wageni sasa kama hawa jamaa wanakataa wageni wataendeleaje aisee?Halafu kilugha kila mahali hadi kanisani na maofisini ni kihaya tu!

Mkuu hapo umepotea ni lini umeenda Bukoba ukabaguliwa kwa taarifa yako waahaya ni wakarimu sana, wanaona fahari kutumia lugha yao hawaoni aibu wanapoizungumza iwe kwenye daladala au wapi, kwanza hii lugha ni tamu inapotamkwa omba tukufundishe kihaya ili na wewe uienjoy raha wanayoipata wahaya
 
2 points of collection.

1. Bakubaza omukihaya oholole omukihaya.
2. Aha bihandiko ebi kutukutula olekele ebishuba, ogambe amazima, buli muntu naguza ensenene????????! Watujangula rugamu.

Mbali na nia njema ya kutaka kudhihirisha kuwa unathamini utamaduni wako kwa kuongea/andika lugha ya kabila lako. Ni jambo jema pia kushirikisha wanaJF wengi juu ya kile unachotaka kuandika hapa jukwaani kwa kutafsiri hayo uliyoyaandika kwa lugha ya kiswahili au hata kiingereza kwa wasiojua kiswahili. Kama ulimaanisha kumueleza mwanzisha mada hayo uliyoyaandika kwa siri basi ungem'PM'(ungetumia Private massage tab).

Vinginevyo hata mimi sijakubaliana na 'Rweye' Kubajangula(kuwadhalilisha) Wahaya kuwa wote wanauza senene ingawa sio bihashara haramu .
 
Mkuu hapo umepotea ni lini umeenda Bukoba ukabaguliwa kwa taarifa yako waahaya ni wakarimu sana, wanaona fahari kutumia lugha yao hawaoni aibu wanapoizungumza iwe kwenye daladala au wapi, kwanza hii lugha ni tamu inapotamkwa omba tukufundishe kihaya ili na wewe uienjoy raha wanayoipata wahaya

according to linguistics kweli kabisa kihaya is a pretigious lg.lakini wahaya ni wabaguzi sana sio kama waskuma
 
Infact mada zinazoihusu Bukoba nazipenda sana kuzijadiri lakini pia wahaya wengi ni note ABAYOZA NA ABAZIBA ni wavivu wa kazi sana hivi ni kwa nini?
 
Infact mada zinazoihusu Bukoba nazipenda sana kuzijadiri lakini pia wahaya wengi ni note ABAYOZA NA ABAZIBA ni wavivu wa kazi sana hivi ni kwa nini?

Mkuu unaongea usichomaanisha ww hauna nia ya kuongea juu ya Bukoba bali unapenda kuongea juu ya watu sana na mambo mengine yasiyokuwa na mantiki...sasa hapa nani ameongelea watu ama na ww uko kama viongozi wenu wanaoshinda wanahubiri unyambo,uyoza,ukiziba,uangaza n.k?unalenga nn hapa?
 
Back
Top Bottom