Mimi ingawa ni mtu wa Kyerwa lakini nimewahi kufanya kazi serikalini hapo Bukoba na najua siasa za hapo Bukoba ....kwanza kwa location ya Bukoba ina advantage nyingi kuliko Mwanza ....Kagera ndio mkoa unaopakana kwa ukaribu na nchi nyingi tena nchi hizo miji yao mikuu ikiwa mbali kulinganisha na distance ya kufika Bukoba ......lakini Bukoba imeshindwa kuvutia wafanyabiashara wengi kutoka nchi jirani kutokana na vitu vingi ....nikipata wasaa nitaviainisha hapa ili serikali isaidie kuimarisha miji mikubwa ya mipakani inayoweza kuvutia biashara nyingi ...
Mheshimiwa mimi siyo mkazi wa Bukoba lakini nafika mara kwa mara hapo mjini kwa shughuli zangu binafsi nikitokea mkoani kwangu. Nashauri kama mtanzania mpenda maendeleo mjaribu kujadiliana kuhusu suala la kuihamisha stendi ya mabasi iliyopo hapo katikati ya mji maana ni ndogo sana na imezidiwa na wingi wa magari. Hii pia itasaidia kuutanua mji na kuongeza fursa. Nakutakia shughuli njema katika kuwalete maendeleo wananchi wako.
Mzee tatzo sio sherehe, nisome vzuri! Ulipaswa kuweka mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi km mbunge. Sijaongelea sherehe hzo. Hata madiwani wengi baada ya kushnda walifanya sherehe lakn hilo halikuwazuia kupita kwa wananchi kuwashukuru.
Mbunge wangu usipokuwa mtu wa kupokea maoni ya watu wako mbeleni kuna tabu. Kagasheki kilichomuangusha ni hayo hayo ya kuamini kila anachofanya yy ni sahihi na hakuna mtu wa kumshauri.
Ebu kwanza changamkenı wabunge wote wa Bukoba ipatıkane dawa ya ugonjwa wa MNYAUKO kwa migomba.Matatizo kama haya yakitokea Kilimanjaro haichukui round yanatatuliwa,BK sasa miaka karibia 10,migomba imeisha na ndızi hakuna.Alafu ya Bukoba nı ndızı na Kahawa.Achana mambo ya ubishıbishi,kuwenı wajanja,dawa lazima serikali inunue dawa!
Ni kweli mkuu, mie niliyegemea kwa vile alipokuwa anaomba kura aliweza kufanya mikutano mingi basi nikatarajia alivyopewa hizo kura angerudi kuandaa mkutano wa kuwashukuru wananchi. Luna tatizo moja, hawa viongozi bado wanahisi mnawawazia sana, wanalinga na wao w?nachukulia kila kitu ni watanikima, mimi ndiye, n.k. Kusema ukweli mtu wa hivi hatambui hata kwanini yuko pale, ni kukosa maadiri pia, unawafundisha nini wenzio? Lakini niliwahi kusikia, kwamba huyu na yule wa CCM wao ni watu wa show tu, anataka tu amshinde mwenzie basi ( prestige). Kwake akishamshinda mwenzie na akaweka mikogo basi mambo ya jimbo ni mengineyo, kama hilo lina ukweli basi wananchi kazi mmejipa wenyewe ( ekibi okizara ).
Ebu kwanza changamkenı wabunge wote wa Bukoba ipatıkane dawa ya ugonjwa wa MNYAUKO kwa migomba.Matatizo kama haya yakitokea Kilimanjaro haichukui round yanatatuliwa,BK sasa miaka karibia 10,migomba imeisha na ndızi hakuna.Alafu ya Bukoba nı ndızı na Kahawa.Achana mambo ya ubishıbishi,kuwenı wajanja,dawa lazima serikali inunue dawa!
Nadhani ushauri kaupata. Km hatasikilza atajuta labda km atajitoq ktk siasa. Watu wanamchora tu. Ss tuliokuwa mashabiki wake ndo tuko tunapondwa. Swala la kuandaa mkutano wa hadhara kuwashukuru wananchi lilikuwa jambo la msngi xana ila yy baada ya kupata ubunge kasepa Dar. Swez kuandka mengi kwa heshima yake na ya Chama chetu.
Tushirikiane kuijenga Bukoba yetu. Aache "kwebona" ili tuondoe makundi ya uchama. Bukoba ni yetu sote. Nina imani manispaa itapga hatua kubwa kimaendeleo maana meya na mbunge ni kutoka Ukawa. Tusije kuleta vsngzio baada ya manispaa kudorora.
Tuanze na stendi ya Bukoba maana ni aibu.
Elimu imedorora xana.
Tuna imani mbunge atafanya kazi kubwa na kwa weledi na kushirikiana na wananchi kuleta maendeleo Bukoba.
Wapendwa Ndugu, Wadau na Wazawa wa Bukoba,Kagera..
Nichukue fursa hii kuwakaribisha katika Bukoba Municipal Developmental Conference (BUMUDECO) Kongamano litakalowapa fursa ya kuijadili na kuijenga Bukoba Mjini Tuitakayo.
Kongamano hili limeandaliwa na Mbunge & Baraza la Madiwani kutegemea kufanyika 27 Disemba 2015 saa tisa Jioni. (tutawajulisha juu ya ukumbi hivi karibuni).
JUKWAA HILI LITAAMBATANA NA YAFUATAYO:
-Mbunge na Baraza la Madiwani kuwasilisha mpango kazi wetu wa miaka mitano 2016-2020.
-Mwakilishi wa Halmashauri kuwasilisha Fursa za uwekezaji zilizoko Bukoba Mjini.
-Kuzijadili changamoto za wananchi na wazawa wa Bukoba Mjini ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
-Kuona ni namna gani wazawa wa Bukoba, Kagera walioko mbali wanaweza kushiriki katika maendeleo ya Bukoba Mjini.
BUKOBA MPYA TUTAIJENGA KWA KUWA NA UONGOZI SHIRIKISHI UTAKAOWAPA WANANCHI, WAZAWA NA WADAU FURSA YA KUSHIRIKI.
Kongamano hili haliko katika misingi ya uvyama,udini wala ukabila. Yeyote mwenye kutaka kuiona Bukoba Mjini ikisonga mbele kwa kasi anakaribishwa sana.
Tuendelee kuwasiliana kupitia ukurasa wangu wa Facebook: Wilfred Lwakatare na email: mbungebukoba2016@gmail.com au wilfredlwakatare@gmail.com
kufika kwenu ndiyo mafanikio yetu.
Wenu katika ujenzi wa Bukoba Mpya;
Wilfred M. Lwakatare
Mbunge Bukoba Mjini 2015-2020.