Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,827
Kaimu mkurugenzi wa Vodacom, Hilda Bujiku amesema tozo za miamala ya simu ilivyoanza walipoteza asilimia 30 ya mapato ya kampuni ila wanategemea miamala itarudi.
Hilda amesema kuna watu wameacha kutumia huduma ya kutuma pesa kupitia mitandao ya simu na wapo waliopunguza idadi ya miamala.
Bujiku amesema miamala haijarudi na wanaendelea kuomba Serikali lakini wanafurahi tozo kupunguzwa na wanaamini miamala itarejea ikiwa ni tayari mwezi mmoja umepita nafuu hiyo itangazwe.
=========
MAONI
Kwako waziri Mwigulu; Tozo zinadumaza sekta ambazo watu walitumia uwekezaji wa maarifa, fedha na nyinginezo kuzibuni. Hata vifurushi vya simu mitandao itakuwa imepandisha ili kufidia faida iliyopungua kutoka kwenye miamala.
Pia nikukumbushe mchumi mwenzangu, moja ya kanuni ya msingi ya kodi ni kuepuka 'Double Taxation'. Kipato kilekile kukitoza kodi zaidi ya mara moja sio afya kiuchumi.
Hii itarudisha miamala ya mkononi ambayo si njema pia hasa kwa BOT kuupima uchumi wa nchi lakini pia itaongeza uchakavu wa pesa. Pia inadumaza biashara zilizokuwa zinafanikishwa kwa hizi huduma kwasababu wafanyabiashara wako sensitive kwenye gharama wanazotumia kufanya biashara.