Budget ya UK ya mwaka 2007/08 ukifananisha ya yetu

nenda angalia ya Japan, US na German pia. ndo utaelewa kuwa bajeti yetu ni bajeti ambayo wazungu wanaiweka kwaajili ya kulisha mbwa kwa mwezii au hata mwaka...kwa wale walofika ulaya, wanajua namna mbwa walivyo wengi hapa, na jinsi wanavyothaminiwa kwa garama...
 
Mbona siwaelewi mnafananisha sungura na tembo???? hawawezi wakashabihiana hata kidogo. kama mnataka kufanya comparative analysis tafuteni nchi ya kiafrika yenye uchumi kama wetu
 
Mbona siwaelewi mnafananisha sungura na tembo???? hawawezi wakashabihiana hata kidogo. kama mnataka kufanya comparative analysis tafuteni nchi ya kiafrika yenye uchumi kama wetu

Lengo la hapa ni kuonesha tu njisi tulivyo nyuma na kazi iliyopo mbele yetu!
 
Kama tunataka kujua kazi iliyo mbele yetu ninadhani kuna mifano nchi kama malaysia ambao walikuwa maskini kama sisi na sasa wako mbali, Vietnam vile vile ni mfano mwingine wa nchi ambayo siyo tu ilikuwa maskini kama sisi lakini wao walipata matatizo zaidi ya kisiasa na hivi sasa wako mbele . Mifano iko mingi ambayo inalandana na TZ. Kuihusisha TZ na UK jamani ni mbali kama vile mwezi na dunia
 
Back
Top Bottom