Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,571
Bajeti hii sio kwa ajili ya watanzania , ila ni kwa ajili ya wenye nchi,
1. Pikipiki zimeongezewa kodi, ile hali huu ni usafiri wa kawaida kwa walalahoi wa nchi hii. Badala yake makampuni ya madini yamesamehewa kulipa ushuru wa mafuta kwa ajili ya migodi yao.
2. Matumizi ya serikali yameongezeka sana ukilinganisha na bajeti ya mwaka jana ambayo imeongezeka kwa 1.8 trilioni.
3.Mazao ya biashara kama pamba, kahawa, katani na chai --yameachwa pembezoni kabisa , ila faraja inaweza ikawa ni kwa wakulima wa korosho.
4.Wavuvi wote hawapo wala vifaa vyao havijapunguziwa ushuru ili walau waweze kutumia nyavu halali badala ya kutumia chandarua , kitu ambacho kinapoteza mazalio ya samaki .
5.Leo imekuwa 11 Trilion, ila ukweli ni kuwa hizo ukilinganisha na kuporomoka kwa shilingi yetu ukiangalia na mwaka jana utaona kuwa hakuna nyongeza kwani mwaka jana ilikuwa 9 trilion ,leo tunasema tumeongeza kwa 18% , ila hali shingi imeanguka ukilinganisha na dola kwa zaidi ya 26% , hivyo hakuna kilichoongezeka.
6.Mfumko wa bei ambao sasa tumeambiwa umeshuka kutoka 12.4% na umefikia 10.2% , hakuna mkakati wowote wa kuhakikisha kuwa mfumko huu unapungua , kwani kati ya vitu vikubwa ambavyo vinasababisha mfumko wa bei ni matumizi ya kaya kwa ajili ya chakula, kila kaya zaidi ya 55% ya kipato ni kwa ajili ya matumizi ya chakula , sasa kama tungetaka kupunguza mfumko wa bei basi tungewekeza kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula.
Hii sio bajeti yetu , ni ya kwao..