Britain under pressure to review £200 million aid for Tanzania after US cuts support

JokaKuu nadhani unafahamu mzizi wa tatizo la Zanzibar.

Tatizo la Zanzibar siyo itikadi za kisiasa bali ni ubaguzi lakini vile vile kumbuka hatujaboronga katika uchaguzi huu tu, tumeanza kuboronga siku ambayo tulituma wanajeshi zaidi ya 300 ili kutoa ulinzi kwa Amani Karume na hapo hapo tukaamua kuungana na katika maisha yote ya muungano kabla ya vyama vingi, tumeshuhudia matatizo mengi.

Wakati Tanzania Bara wanaongelea Marais watano, Zanzibar imekuwa na Marais saba.

Nchi za Western zinachofanya ni kutumia matatizo haya kama opportunity katika ku-set agenda zao za kiuchumi ili ziwanufaishe.

Kuna mahojiano yalifanywa na Maalim Seif ambayo ukiyachunguza utaona hali halisi ya matatizo ya Zanzibar. Maalim Seif alinukuliwa akisema,“Kabla Kikwete (Rais Mstaafu Jakaya Kikwete) hajaondoka madarakani, aliniambia kuwa Maalim CCM wanakuogopa, wanajua ukishinda utaweza kuvunja Muungano, lakini nilimwambia, CCM ndio wenye jeshi, wenyewe ndio wenye dola mimi nitavunjaje Muungano’’.

Kama haya maelezo ni kweli basi yanatoa picha kuwa Rais wa Tanzania/Mwenyekiti wa CCM Taifa hana nguvu lilopokuja suala la Zanzibar. Kuna nguvu zaidi ya Rais ambazo zinafanya maamuzi kuhusu hatima ya Zanzibar.

Suala la kujiuliza, kina nani zaidi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania ndani ya CCM ambao wanaogopa Maalim Seif kuwa Rais wa Zanzibar kwa sababu atavunja Muungano? Au chenye nguvu ni ''Kitengo'' kilichokuwa kinasemwa na Mzee Kingunge ambacho tunaambiwa ndicho kinachofanya hata maamuzi kuhusu mgombea Urais wa CCM.

Kumbuka kwa kiwango kikubwa CCM bado ni chama dola kama ilivyokuwa kwenye siasa za chama kimoja!
Aisee!
 
Mkuu,kilichotuponza sisi ni uvumilivu wetu (na Lowassa pia)
Hatukuonesha reaction yoyote ya kutokuridhika na matokeo au kudhulumiwa haki yetu.

Lakini angalia wenzetu Wanzanzibar wakiongozwa na Maalim Seif walivyochachamaa.
Na hata Diasporas wa Zanzibar walioko UK uliona maandamano yao pamoja na jumbe zilizokuwa kwenye mabango yao?
Hili liliwafungua akili nchi wahisani hadi wakafuatilia kwa ukaribu na matokeo yake ndio kama tulivyoona.
Tuliwaambia Chadema/Ukawa mpya chini ya Lowassa, Mwalimu Sumaye na Kingunge ni janga na litawacost lakini tukapuuzwa.
Basi tena. Opportunity ile imepita.
 
Kwani lengo la wewe kuileta hii post ni nini kama si kutaka kuwaumbua wale waliosema kwamba UK pia wamefuta misaada yao kwa Tanzania? Ni kama unashangilia misaada kimoyo moyo huku ukiendelea kujifanya umekunja uso kutotaka hiyo misaada.
Tunapenda misaada na nani? Hii ni hoja yangu na mtazamo wangu pekee.

Ni wapi nimesema ninapenda misaada?

Umetumia kigezo gani kinachotambulika ukafahamu kama sina bongo za kujitegemea?
 
Hivi nyie watu wazima na wasomi mnapokaa chini na kuanza kujadili misaada kwa urefu na umakini kwa kiasi hiki hamuoni kama mnapoteza muda kwenye ujinga?
 
Kina kitu ambacho hakijaeleweka vizuri hapa. Msaada uliositishwa ni ule ambao UK inachangia kwenye bajeti ya Tz kwa kushirikiana na nchi zingine wafadhili (kwa utaratibu wa multilateral agreements). Misaada inaotolewa moja kwa moja na kusimamiawa na serikali ya UK kwa ajili ya kufadhili miradi (hasa ya kijamii) ndio inayozungumziwa kwenye hii story ya gazeti la Telegraph. Kadhalika, misaada inayotolewa na serikali ya Marekani nje ya utaratibu wa MCC kama inayofadhili miradi ya afya/ukimwi haiyaguswa. Hii inahusisha pia misaada ya moja kwa moja kutoka kwa wafadhili wengine (kwa utaratibu wa bilateral agreements).
Huu mwaka tutaona na kusikia mengi.
 
Mimi nadhani siyo vibaya kujadili hizi hoja kwa uwazi na ukweli. Inasaidia kujua hatma ya kiuchumi ya taifa letu.
Hivi nyie watu wazima na wasomi mnapokaa chini na kuanza kujadili misaada kwa urefu na umakini kwa kiasi hiki hamuoni kama mnapoteza muda kwenye ujinga?
 
Marekani na jumuiya ya ulaya wote ni wanafiki hawana lolote ndio maana Korea na washirika wengine hawa patani kabisa.
Wamekuwa wakilinda maslahi yao na pale wanapoona maslahi yao yanaingiliwa wanajidai kutoa vitisho .

Mimi ninauliza kwanini wanashupalia uchaguzi wa Zanzibar Je huu wa Tanzania bara ulikuwa wa haki kama ndio basi uchaguzi wa marudio Zanzibar ulikuwa wa haki waache unafiki.
 
Nadhani "kunyimwa msaada" na wafadhili inaweza kuwa baraka katika kificho "blessing in disguise". Hii iwe chachu kwa viongozi wa mchi yetu na watanzania wote kwa ujumla kuona umuhimu wa kujenga uchumi au taifa linalojitegemea. Isiwepo sababu ya serikali kushindwa kukusanya mapato yake nakufanya matumizi yanayofaa.... Hii itaaidia kuepuka kulamba viatu vya wafadhili pindi wanapotishia "kutunyima misaada"

Period!!
 
KWA UJUMLA TANZANIA HAKUNA DEMORACY NI USANII TUPU AFRICA NZIMA ISIPOKUWA NCHI CHACHE KAMA AFRICA KUSINI,KWINGINE KOTE NI MATATA.NOT YET UHURU AFRICA I CRY !
 
The western Countries Always believe they are right 100%
and After The Almighty God what follow are Themselves.

What Others are doing especially Africans without their permits
are not permitted,and if so, something must be given to them
as gift ,offer and they may accept with conditions (POLITICS).

That is Neo-Colonialism,and as Africans we can not accept it directly or indirectly.

They decided themselves to give us independence long time ago,how come
they are questioning about our livings/internal affairs.

If Great Britain is decided to withdraw its Aid for Tanzania,we are going to praise
a lot since they teach us how to develop without depending their Aid.

The time is now for us to survive without getting any Aid from our former
Colonial Masters.

Aids for us may be good,but they give us for their own benefit or
benefit our fellow few Africans and left more people in great
poverty while emphasis on exploitation of large mass of raw materials
without targeting to build big industry to employ our people.
 
Tanzania itakuwa nchi ya viwanda Na uchumi wa kati sasa mnababaika kwa nn
Nani anababaika huoni kodi zikikusanywa kwa kasi? Mianya ya ufisadi inazibwa? Rais hataki kusafiri ovyo ipongeze serikali mkuuu.
 
Natumaini tujaribu kuangalia western country siasa zao kwa nchi za Africa. Siku zote wao siasa zao kwetu ni unafiki WA masilai hawa ukweli na nchi zetu ila kutafuta namna gani watapenyeza agenda ya kupata biashara kwetu hakuna kubana misaada wala nini. Agenda hapa ni masilahi tu.
 
Kwani lengo la wewe kuileta hii post ni nini kama si kutaka kuwaumbua wale waliosema kwamba UK pia wamefuta misaada yao kwa Tanzania? Ni kama unashangilia misaada kimoyo moyo huku ukiendelea kujifanya umekunja uso kutotaka hiyo misaada.
Mimi nilichofanya ni kusema ukweli.

Kwa hisia na mtazamo wako unadhani kusema ukweli ni kushangilia.

Tanzania haikuwalazimisha kutupa misaada na pia haitawalazimia kukata misaada.

Ni uamuzi wao kusuka au kunyoa.
 
The UK Government was under pressure on Saturday to review British aid worth £200 million after an African country staged a widely condemned election.

A former cabinet minister warned against “spraying money around” simply to ensure that Britain kept the United Nations target of spending 0.7 per cent of national income on overseas aid.

The row focuses on Tanzania where the government has been accused of rigging elections on the island of Zanzibar, leading the opposition to boycott the latest poll.

This week, America accused Tanzania’s government of a “pattern of actions” that undermined democracy and cancelled aid worth $472 million (£331 million).

This placed pressure on Britain to do the same, especially in the wake of widespread concern over the use of the aid budget for controversial projects.

But the Foreign Office told the Telegraph there was no decision to reduce Britain’s support for Tanzania even though Zanzibar’s election had not reflected the “will of the people”.

Owen Paterson, the senior Conservative backbencher and former environment secretary, said that DFID should reduce its aid to Tanzania in line with the US decision.

“The Foreign Office says the election is not valid and we’re carrying on spending the money anyway. This cannot be right,” said Mr Paterson.

“The Americans have acknowledged that this cannot be right and have acted – and we should act accordingly.” said Paterson


Source: The Telegraph
Ni Wakati humefika kuachana na misaada ya nje hasa western country zinakuwa na masharti kwa ajili ya faida zao wenyewe
Wafrica mnatakiwa Kuwa na umoja kama vile nchi za Ulaya ,magharibi .Mpaka hapo wafrica WAKIWA na umoja wenye nguvu
Siyo kama sasa.Hapo mtaweza hatuitaji misaada yenye masharti.Zanzibar hinaserikali yake ,bunge lake ,mawaziri wake,
Tanzania bara walichofanya kuwe na usalama Zanzibar na pemba,lakini mahamuzi ya kurudia kupiga kura ni mahamuzi ya serikali ya Zanzibar siyo Bara
 
Zanzibar hinaserikali yake na mahamuzi yake,Kuna bunge la Zanzibar,mawaziri wake,wabunge wake.
SErikali ya Tanzania bara walichofanya ktk uchaguzi Zanzibar ni kuhakikisha kunakuwa na usalama wakati wakirudia uchaguzi.
Kwanza nchi za Ulaya ya magharabi Zina shida na economic kwa sasa ,watu wengi hawana kazi,Kwa hiyo kukata hiyo misaada
ni kisingiziyo tu,Wamekwisha hamua hakuna misaada kwa nchi za Kiafrica hasa Tanzania Bila Zanzibar au Zanzibar kurudia kupiga kura.
Ni Wakati humefika nchi za Kiafrica kujitegemea 100% badala kutegemea nchi za western
 
Back
Top Bottom