Britain under pressure to review £200 million aid for Tanzania after US cuts support

Mi nashangaa watu wanaongelea ya zanzibar tu kuboronga uchaguzi,wakati hata lowassa ameporwa ushindi wake.Lakini bahati nzuri malipo ni hapa hapa duniani,wale viongozi wa sekta mbalimbali waliosaidia kupora uchaguzi ili magufuli ashinde,wameshafukuzwa kazi,au watafukuzwa kazi siku yoyote au mishahara yao imefyekwa.Shukrani ya punda...najua huko waliko wanalia na kusaga meno!Na bado..
Demokrasia gani ya kuweka wezi kuongoza taifa Hata kama Lowassa angeshinda kihalali asingepewa nchi ! Ni mwizi, nchi sio kupiga kura tu na kupewa , tulishajifunza toka kwa wenzetu , Hilter alishinda uchaguzi kwa kura , watu walizungusha mikono kwa ushabiki wakampa nchi , baadae ikawa kilio cha dunia mzima
 
Acha kumchonganisha mzee wa watu,ni lini na wapi Magu alisema Hataki msaada?
Kumbe nimegundua kuna watu humu ni kizazi cha watumwa walioachwa zanzibar maana wengi ni akili ya kupewa misaada , tunavyolia lia na hii misaada tungekuwa tunalia hivyo kwa kufanya kazi mbona tungekuwa mbali , Magu kaisha amua hatuitaji hizo pesa tutazipata wenyewe kwa kufanya kazi , sisi tutatoa misaada kwao
 
Demokrasia gani ya kuweka wezi kuongoza taifa Hata kama Lowassa angeshinda kihalali asingepewa nchi ! Ni mwizi, nchi sio kupiga kura tu na kupewa , tulishajifunza toka kwa wenzetu , Hilter alishinda uchaguzi kwa kura , watu walizungusha mikono kwa ushabiki wakampa nchi , baadae ikawa kilio cha dunia mzima
Mwizi ni huyu aliyenunua meli mbovu na zee ya mwaka 1968 mv Dar es salaam kwa bilioni 6,ambayo kutoka hapo bagamoyo tu mpaka dar inachukua masaa matatu!wakati bakhresa akanunua mv Kilimanjaro mpya kwa bei hiyohiyo na inaenda Zanzibar kwa dakika 45,by the way hiyo meli yenu iliyonunuliwa na huyo fisadi wenu mnaemuabudu iko wapi siku hizi?
 
Mi nashangaa watu wanaongelea ya zanzibar tu kuboronga uchaguzi,wakati hata lowassa ameporwa ushindi wake.Lakini bahati nzuri malipo ni hapa hapa duniani,wale viongozi wa sekta mbalimbali waliosaidia kupora uchaguzi ili magufuli ashinde,wameshafukuzwa kazi,au watafukuzwa kazi siku yoyote au mishahara yao imefyekwa.Shukrani ya punda...najua huko waliko wanalia na kusaga meno!Na bado..
Mkuu,kilichotuponza sisi ni uvumilivu wetu (na Lowassa pia)
Hatukuonesha reaction yoyote ya kutokuridhika na matokeo au kudhulumiwa haki yetu.

Lakini angalia wenzetu Wanzanzibar wakiongozwa na Maalim Seif walivyochachamaa.
Na hata Diasporas wa Zanzibar walioko UK uliona maandamano yao pamoja na jumbe zilizokuwa kwenye mabango yao?
Hili liliwafungua akili nchi wahisani hadi wakafuatilia kwa ukaribu na matokeo yake ndio kama tulivyoona.
 
JokaKuu nadhani unafahamu mzizi wa tatizo la Zanzibar.

Tatizo la Zanzibar siyo itikadi za kisiasa bali ni ubaguzi lakini vile vile kumbuka hatujaboronga katika uchaguzi huu tu, tumeanza kuboronga siku ambayo tulituma wanajeshi zaidi ya 300 ili kutoa ulinzi kwa Amani Karume na hapo hapo tukaamua kuungana na katika maisha yote ya muungano kabla ya vyama vingi, tumeshuhudia matatizo mengi.

Wakati Tanzania Bara wanaongelea Marais watano, Zanzibar imekuwa na Marais saba.

Nchi za Western zinachofanya ni kutumia matatizo haya kama opportunity katika ku-set agenda zao za kiuchumi ili ziwanufaishe.

Kuna mahojiano yalifanywa na Maalim Seif ambayo ukiyachunguza utaona hali halisi ya matatizo ya Zanzibar. Maalim Seif alinukuliwa akisema,“Kabla Kikwete (Rais Mstaafu Jakaya Kikwete) hajaondoka madarakani, aliniambia kuwa Maalim CCM wanakuogopa, wanajua ukishinda utaweza kuvunja Muungano, lakini nilimwambia, CCM ndio wenye jeshi, wenyewe ndio wenye dola mimi nitavunjaje Muungano’’.

Kama haya maelezo ni kweli basi yanatoa picha kuwa Rais wa Tanzania/Mwenyekiti wa CCM Taifa hana nguvu lilopokuja suala la Zanzibar. Kuna nguvu zaidi ya Rais ambazo zinafanya maamuzi kuhusu hatima ya Zanzibar.

Suala la kujiuliza, kina nani zaidi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania ndani ya CCM ambao wanaogopa Maalim Seif kuwa Rais wa Zanzibar kwa sababu atavunja Muungano? Au chenye nguvu ni ''Kitengo'' kilichokuwa kinasemwa na Mzee Kingunge ambacho tunaambiwa ndicho kinachofanya hata maamuzi kuhusu mgombea Urais wa CCM.

Kumbuka kwa kiwango kikubwa CCM bado ni chama dola kama ilivyokuwa kwenye siasa za chama kimoja!
Makubaliano ya mwafaka ya Zanzibar yaliyozaa Serikali ya umoja, huko nyuma niliyaona yalikuwa na matatizo na kuwa hayataleta suluhu ya kudumu. Pamoja na kuwa kwa sasa yanaonekana kufa, lakininkwa kweli nafikiri Rais mstaagu Kikwete anatakiwa kupongezwa kwa kubuni na kusimamia makubaliano hayo. Ilifanya utawala wake uwe wa amani hasa kwa upande wa Zanzibar. Zanzibar haikumsumbua kipinfi vhote cha utawala wake na wala hakulazimika kupeleka vikosi vya jeshi au polisi wa ziada huko. Zanzibar iliweza kufanya miradi mikubwa ya maendeleo kwa uelewano tofauti kabisa na tawala zilizomtangulia! Ninachokiona sasa haya yatakuwa kinyume.
 
Kumbuka kuwa USA wanajua na walihusika kwa kiasi kikubwa kuasisi muungano wa Tanganyika na Zanzibar. USA wanajua kwa nini ni vigumu kwa Tanzania bara kutawala kila kinachoendelea Zanzibar. Rejea tamko la msemaji wa ubalozi wa Marekani kuhusu MCC kwamba linazungumzika hivi majuzi.
 
wakati mwingine ni bora viongozi wetu wawe makini sana na haya mataifa ya magharibi maana inaonekana kabisa JPM halikuwa chaguo lao hivyo wanajitahidi kumbana JPM ili afuate matakwa yao
 
Demokrasia gani ya kuweka wezi kuongoza taifa Hata kama Lowassa angeshinda kihalali asingepewa nchi ! Ni mwizi, nchi sio kupiga kura tu na kupewa , tulishajifunza toka kwa wenzetu , Hilter alishinda uchaguzi kwa kura , watu walizungusha mikono kwa ushabiki wakampa nchi , baadae ikawa kilio cha dunia mzima
Mkuu ni kilio chako unajuwa Hitler ndio shujaa wa ujerumani? Nguvu za uchumi za ujerumani chanzo ni Adof
 
Makubaliano ya mwafaka ya Zanzibar yaliyozaa Serikali ya umoja, huko nyuma niliyaona yalikuwa na matatizo na kuwa hayataleta suluhu ya kudumu. Pamoja na kuwa kwa sasa yanaonekana kufa, lakininkwa kweli nafikiri Rais mstaagu Kikwete anatakiwa kupongezwa kwa kubuni na kusimamia makubaliano hayo. Ilifanya utawala wake uwe wa amani hasa kwa upande wa Zanzibar. Zanzibar haikumsumbua kipinfi vhote cha utawala wake na wala hakulazimika kupeleka vikosi vya jeshi au polisi wa ziada huko. Zanzibar iliweza kufanya miradi mikubwa ya maendeleo kwa uelewano tofauti kabisa na tawala zilizomtangulia! Ninachokiona sasa haya yatakuwa kinyume.
Mkuu, hufahamu kama Maalim Seif hakutambua matokeo ya Uchaguzi wa mwaka 2005 baada ya kupata kura asilimia 46.1 ambapo Amani Karume alipata asilimia 53.2 ambao pia uchaguzi wa Tanzania ulimwingiza Rais Kikwete kwa mara ya kwanza madarakani?

Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliopita angalau bila mikwaruzo mikubwa ni ule wa 2010.
 
Hehehe kiukweli naona bado watu wana lizungusha jambo moja
Ngoja tuone
 
Hakuna uamuzi kama huo labda uwe umefanyika leo!

Kama huo uamuzi upo, naomba official statement ya Development Partners Group (DPG) Tanzania kwa sababu ni kawaida yao kutoa official statement kila wanapofanya uamuzi unaoligusa taifa kama walivyofanya kwenye kadhia ya Tegeta Escrow Account.

Hizo zilikuwa ni story tu ambazo baadhi ya watu waliamua kuzitunga na kuziweka kwenye media.
Mkuu unahangaika sana kutetea na kukanusha kama vile wewe ndie msemaji wa serikali.

Ile taarifa ya wafadhili kujitoa ilikaririwa na vyombo mbali mbali vya habari vya ndani na nje vingine vikimkariri katibu mkuu wizara ya fedha.

Kama ingejua ni ya uongo serikali au wizara ya fedha inekanusha hiyo taarifa kua sio ya kweli lakini hawajafanya hivyo wewe ndio umekomaa kukanusha, wewe ndie msemaji wa serikali au wizara?

Hili jambo linawaumiza sana,kila siku hapa unatetea kujitegemea hapo hapo unatafta vyanzo mbali mbali vya habari kuonyesha hatujaondolewa misaada, msimamo wenu ni upi,misaada au kujitegemea?
 
Mkuu, hufahamu kama Maalim Seif hakutambua matokeo ya Uchaguzi wa mwaka 2005 baada ya kupata kura asilimia 46.1 ambapo Amani Karume alipata asilimia 53.2 ambao pia uchaguzi wa Tanzania ulimwingiza Rais Kikwete kwa mara ya kwanza madarakani?

Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliopita angalau bila mikwaruzo mikubwa ni ule wa 2010.
Sizungumzii uvhaguzi tu. Matatizo ya Zanzibar ingWa huanza kwa chaguzi lakini hudumu kipindi chote. Ni kweli 2005 hayo yalitokea (kama yanavyotokea kila uchaguzi baada ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi) ambayo yalimfanya Rais mstaafu na mwenzake wa Zanzibar kuyatumia kutafuta suluhu ambayo ilipatikana na kuwafanya kuongoza kwa amani Zanzibar.
 
..u r 100% correct.

..Marekani na Uingereza wanaweza kuwa wanakupiga vita lakini bado makampuni yao yakaendelea kuwekeza nchini kwako.

..kwa mfano, wakati vita vya Angola[mpla vs unita], serikali ya Marekani ilikuwa inasaidia unita[waasi], wakati exxon mobil wanachimba mafuta cabinda na uwekezaji wao ndiyo una-finance war chest ya mpla[serikali]. wakati huo huo majeshi ya cuba ndiyo yalikuwa yanalinda visima vya mafuta vya serikali ya angola.

..jambo lingine nadhani tunafanya makosa kwa kujikita kuona ni nchi gani zitatuwekea vikwazo, na athari za vikwazo hivyo. hali hiyo ni sawa na kuangalia tulipoanguka badala ya wapi tumejikwaa.

..tukubali kwamba tumeboronga ktk uchaguzi marudio wa znz. tunachotakiwa kufanya ni kuchukua hatua ambazo zitashawishi nchi wahisani kuona kwamba tunatafuta suluhisho la kudumu la mgogoro wa znz.

As long as ccm itaendelea kuwa madarakani huku tanganyika hakuna kitakachobadilika zanzibar kamwe; you bet!
 
Mkuu unahangaika sana kutetea na kukanusha kama vile wewe ndie msemaji wa serikali.

Ile taarifa ya wafadhili kujitoa ilikaririwa na vyombo mbali mbali vya habari vya ndani na nje vingine vikimkariri katibu mkuu wizara ya fedha.

Kama ingejua ni ya uongo serikali au wizara ya fedha inekanusha hiyo taarifa kua sio ya kweli lakini hawajafanya hivyo wewe ndio umekomaa kukanusha, wewe ndie msemaji wa serikali au wizara?

Hili jambo linawaumiza sana,kila siku hapa unatetea kujitegemea hapo hapo unatafta vyanzo mbali mbali vya habari kuonyesha hatujaondolewa misaada, msimamo wenu ni upi,misaada au kujitegemea?
Mkuu, Kwanza unaposema msimamo wetu ni upi una maana mimi na nani? Kwani wewe msimamo wenu ni upi?

Pili, Huwezi kuniuliza mimi ni serikali labda kama hufahamu taratibu za serikali katika mawasiliano na umma. Kama unafahamu taratibu za serikali katika mawasiliano na umma halafu unauliza swali kama hili utakuwa unachofanya ni kama upumbavu! sorry!

Hivi unadhani serikali itakanusha suala ambalo haina uwezo nalo? serikali anatoa tamko kwa suala ambalo linahusu serikali.

Sikulazimishi kukubali ninachokiandika kama usivyoweza kunilazimisha kile unachokifikiri.

Kinachosomeka hapa na kukubalika ni nguvu ya hoja.

Chambua hoja zangu kwa kutumia nguvu ya hoja na siyo nguvu za hisia.

Kama unadhani sina hoja, unaweza kusoma tu na kuondoka!
 
Kumbe bado mnapenda misaada eeh?sasa kujitia kwamba hamtaki misaada tena eti tunaweza kujitegemea mlikuwa mnamaanisha nini?nyinyi watu bado hamjawa na bongo za kuweza kujitegemea,kumbukeni kuwa sifa yetu kuu kutokujua namna ya kutengeneza fedha, ila tunapenda sana kutumia tena ktk wrong priorities.
Inashangaza siku mbili zilizopita tuliambiwa UK imekata misaada kwa Tanzania kumbe ulikuwa ni uwongo!

Don’t bet on it, UK na Marekani wametoka mbali na huwa wanashikamana kwenye maslahi lakini kumbuka pia kuna nguvu za makampuni katika diplomasia ya Tanzania kama Exxon Mobil, BG Group na Norway´s Statoil ambayo yamewekeza pesa nyingi nchini kwenye gas achilia mbali yale ya madini kama ACACIA. Baadhi ya haya makampuni yanalipa pesa nyingi kama kodi nchini UK na kwa maana hiyo, yanakuwa na bargaining power katika meza ya maamuzi katika serikali ya UK. Kuendelea kuwepo kwa haya makampuni nchini unafuta uwezekano wa Tanzania kuwekewa vikwazo vya kiuchumi. Ieleweke kuwa kukata misaada ni tofauti na kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.

This is diplomatic war between USA and UK, bear also in mind, the relationship between Obama administration and UK government under Cameron have been strained since the President criticized the UK Prime Minister for getting distracted during the crisis in Libya and turning it into a shit show.

Kwenye sakata hili tutaona na kusikia mengi kadri viongozi wa Western Countries wanavyomtingisha Rais Magufuli ili wafahamu msimamo wake kiuchumi.
 
Kumbe bado mnapenda misaada eeh?sasa kujitia kwamba hamtaki misaada tena eti tunaweza kujitegemea mlikuwa mnamaanisha nini?nyinyi watu bado hamjawa na bongo za kuweza kujitegemea,kumbukeni kuwa sifa yetu kuu kutokujua namna ya kutengeneza fedha, ila tunapenda sana kutumia tena ktk wrong priorities.
Tunapenda misaada na nani? Hii ni hoja yangu na mtazamo wangu pekee.

Ni wapi nimesema ninapenda misaada?

Umetumia kigezo gani kinachotambulika ukafahamu kama sina bongo za kujitegemea?
 
Kina kitu ambacho hakijaeleweka vizuri hapa. Msaada uliositishwa ni ule ambao UK inachangia kwenye bajeti ya Tz kwa kushirikiana na nchi zingine wafadhili (kwa utaratibu wa multilateral agreements). Misaada inaotolewa moja kwa moja na kusimamiawa na serikali ya UK kwa ajili ya kufadhili miradi (hasa ya kijamii) ndio inayozungumziwa kwenye hii story ya gazeti la Telegraph. Kadhalika, misaada inayotolewa na serikali ya Marekani nje ya utaratibu wa MCC kama inayofadhili miradi ya afya/ukimwi haiyaguswa. Hii inahusisha pia misaada ya moja kwa moja kutoka kwa wafadhili wengine (kwa utaratibu wa bilateral agreements).
 
Back
Top Bottom