FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,065
Brexit kumng'oa Waziri Mkuu Uingereza?
(Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi Theresa May)
Waziri Mkuu wa Uingereza hii leo atakabiliana na kura ya wabunge kutokuwa na imani na uongozi wake.
Akiongea nje ya ofisi yake jijini London, Bi May amesema: "Itanilazimu kupambana na kura hiyo kwa kila uwezo niliokuwa nao."
Ametahadharisha kuwa, Waziri Mkuu mpya (iwapo yeye) ataondoshwa anaweza kuchelewesha ama anaweza kuchelewesha ama kuvunja mchakato wa Uingereza kujitoa kwenye Umoja waUlaya (EU) ifikapo Machi 29, 2019 maarufu kama Brexit.
Wabunge wa chama tawala cha ndio wanaotarajiwa kupiga kura hiyo baadae leo kati ya saa tatu na tano usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Matokeo ya kura hiyo yanatarajiwa kutangazwa mara tu baada kumalizwa kupigwa kura.
Mhariri wa siasa wa BBC Laura Kuenssberg amesema kucheleweshwa kwa Brexit ndio karata ya turufu ambayo wafuasi wa Bi May watakayoitumia kushawishi wabunge wasimng'oe madarakani.
Akina nani wanataka kumng'oa Bi May?
Baadhi ya wabunge wa chama tawala cha kihafidhina wamepigia chapua kura hiyo kwa kile wanachokiamini kuwa Bi May ameshindwa kutekeleza matakwa ya wananchi walioamua kujitenga na Ulaya kwenye kura ya maoni ya mwaka 2016.
Bi May alijiamini kuwa alishalituliza kundi hilo la wabunge mwezi uliopita.
Hata hivyo, hatua yake ya kuahirisha kupigiwa kura na bunge makubaliano aliyoyafikia na viongozi wengine wakuu wa EU umewapa nguvu wapinzani wake ndani ya chama.
Kunahitajika uwepo wa wabunge 48 tu kati ya 315 wa chama tawala wanaotaka yeye kung'olewa ili kura hiyo iitishwe, na idadi hiyo tayari imeshavuka.
(Jacob Rees-Mogg: Kwa maslahi ya taifa inabidi (Bi May) ang'oke madarakani)
Jacob Rees-Mogg, ambaye amejitokeza hadharani akaitaka Bi May atoke madarakani amesema: "Mipango ya Theresa May itaiangusha serikali kama itatekelezwa. Lakini chama chetu hakiwezi kuvumilia hilo."
"Wabunge wa Conservative sasa inawapasa kuamua kama wanataka kwenda kwenye uchaguzi chini ya uongozi wa Bi May. Kwa maslahi ya taifa inabidi aende tu."
Kwa nini wanataka kumng'oa?
Wabubge hao hawakubaliani na na makubaliano aliyoyaingia na EU wakiamini yataendelea kuifunga mikono Uingereza na kushindwa kujipambanua nje ya mipaka yake na duniani kwa ujumla kwa kutafuta ushirikiano bora wa kibiashara.
Hasira kali zaidi zipo kwenye mustakabali wa mpaka wa kisiwa cha Ireland chenye nchi mbili. Kusini kuna Jamuhuri ya Irelan ambayo ni mwanacha wa EU wakati Ireland ya Kaskazini ni sehemu ya Uingereza. Hivi sasa mpaka huo upo wazi lakini pale Uingereza itakapojitoa EU mpaka huo utafunguliwa na kubadili kabisa hali ya kiuchumi.
Wabunge hawataki mpaka huo kufunguliwa. Japo Bi May ameahidi kulitafutia ufumbuzi wa kudumu jambo hilo, wapinzani wake wanaamini hawezi kwa sababu viongozi wa EU wamegoma kuingia makubaliano mapya naye.
Je kutakuwa na Waziri Mkuu mpya kama atashindwa kura?
Ndiyo, lakini si leo au kesho.
Iwapo wabunge wa chama chake watamng'oa atasalia madarakani kwa walau wiki sita wakati chama chake kikimsaka mrithi wake.
Kama watajitokeza wagombea wengi wabunge wa Conservative itabidi wawapigie kura na kubaki na wawili ambao majina yao yatapigiwa kura na wanachama wa chama hicho ili kupata kiongozi mpya.
Ni muhimu kuelewa kuwa, Bi May kura atakayopigiwa ni ya kuvuliwa uongozi wa chama. Ili uwe Waziri Mkuu Uingereza inabidi uwe kiongozi wa chama chenye wabunge wengi. Hivyo mrithi wa Bi May katika uongozi wa chama atakuwa Waziri Mkuu mpya bila kufanyika kwa uchaguzi mkuu.
Je anaweza kushinda kura hiyo?
Ili ashinde kura hiyo, na kubaki na wadhifa wake ndani ya chama na serikali, Bi May inabidi aungwe mkono na wabunge zaidi ya nusu wa chama tawala.
Iwapo wabunge 158 kati ya 315 wa chama chake watasema wana imani naye basi atakuwa salama.
Tayari mawaziri wake wote wameshasema kuwa wanamuunga mkono, kwa ujumla mpaka sasa kuna wabunge 158 ambao wameonesha kumuunga mkono. Hata hivyo kura hiyo ni ya siri na matokeo yanaweza kwenda upande wowote, na hivyo ni ngumu kutabiri.
Iwapo atashinda, Bi May atakuwa na uhakika wa kusalia uongozini kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi kabla ya jaribio kama hilo kuruhusiwa kufanyika.
Iwapo atashindwa basi atafungasha virago, na hataruhusiwa kugombea kwenye uchaguzi wa ndani ya chama utakaofanyika. Na iwapo atapata ushindi mwembamba basi inatarajiwa pia atajiuzulu kwa kukosa kuaminiwa na wengi ndani ya chama chake.
Nani anatazamiwa kumrithi atakaposhindwa?
(Kutoka juu kushoto kwenda kulia: Jeremy Hunt, Boris Johnson, Dominic Raab, Michael Gove, Sajid Javid na Amber Rudd)
Wanaotajwa zaidi ni Waziri wa Mambo ya Ndani Sajid Javid, Mambo ya Nje Jeremy Hunt, Mazingira Michael Gove na waziri wa Kazi na Pensheni Amber Rudd.
Nje ya baraza la mawaziri ni waziri wa zamani Brexit Dominic Raab na David Davis na waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Boris Johnson.
Chama cha Labour kinasemaje?
Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Labour Ian Lavery amesema kura hiyo ni matokeo ya: "udhaifu wa Theresa May na kushindwa kabisa kuingoza serikali yake kwenye wakati muhimu kwa nchi."
Bw Lavery pia ameongeza kuwa mabishano ndani ya chama tawala kinafanya maisha ya watu na kazi zao kuingia kwenye lindi la hatari.
Chama cha Labour kimekuwa kikipata msukumo kutoka ndani na nje kwa washirika wao wa upinzani kuitisha kura ya kutokuwa na imani na serikali ya Bi May. Hata hivyo matokeo ya kura hiyo yanaweza kuipelekea Uingereza kwenye Uchaguzi mkuu na uongozi wa Labour unaonekana haupo tayari kwa hio kwa sasa.
Chanzo: BBC